Kwenu Waharakati wa Usawa

Kwenu Waharakati wa Usawa

Phyzicer

Member
Joined
Aug 29, 2025
Posts
6
Reaction score
3
Kuna Kitu Sijaelewa bado.

Unakuta Mdada au Mmama au hata Baadhi ya Wanaume wakijenga Hoja kuwa Suala la Malezi ya Watoto na Kusimamia Nyumba ni jukumu la Sawa kwa sawa baina ya wanandoa(yaani Mwanamke na Mwanaume)

Hivyo Ile dhana ya kwamba mwanamke abaki nyumbani alee watoto na atunze mji ni dhana batili na ya Mfumo Dume...

Lakini Cha Ajabu sijawahi kuona Nyumba yenye Msaidizi wa Kazi za Ndani mwenye kulea watoto akiwa jinsia ya Kiume.

Mara zote naona ni ma housegirl ndio wanaachiwa watoto wa wale wanawake wenye mihangaiko ya kushindwa kulea watoto wao.

Hata kwenye zile Daycare sidhani kama kuna Daycare yenye Wafanya kazi wakiume wanaotunza watoto. (KAMA ZIPO NIFAHAMISHWE)..

Au niwaulize wale Feminists jee Kuna ambae atakubali amuachie 'Houseboy' watoto wake awasimamie hadi jioni atakaporudi yeye??

Jee Hili linamaanisha wanawake wanasaikolojia muafaka zaidi ya malezi???
 
Back
Top Bottom