Kwenu Bodi ya Mikopo (HESLB)

Natafuta kiki

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
911
1,284
Poleni na majukumu ya kujenga taifa: Sisi wanafunzi tuliosoma Chuo kikuu cha Sekomu kilichopo Lushoto Tanga tuliomaliza mwaka 2015; tunayo masikitiko makubwa kwa tuliyofanyiwa na nyinyi bodi pamoja na chuo cha Sekomu.

1. Mwaka wa masomo 2013/2014 na mwaka wa masomo 2014/2015 bodi mlitukata hela ya ada kwa wanafunzi wote bila sababu. Tukamtuma kiongozi wetu yaani waziri wa mikopo kufuatilia jambo hilo na tunashukuru mlimpa majibu kuwa mtarudisha hizo fedha za ada kwa miaka yote miwili.

2. Kwa miaka yote hiyo sisi wanafunzi tuliendelea kulipa ada mliyotukata bila sababu na tunamshukuru Mungu alituwezesha tukamaliza madeni yote.

3. Mwaka 2015 mwezi July tulihitimisha/ kumaliza masomo yetu kwa ngazi ya shahada ya kwanza.
Baada ya sisi kuondoka mwezi Octoba tukapewa taarifa kuwa mmerejesha fedha mlizokata. Hivyo chuo kikabandika majina ya wanafunzi wote waliorejeshewa hizo fedha na kututaka twende chuoni kurudishiwa fedha kwani ada tulikuwa tumemaliza na kufanya UE.

Kwa kuwa tulikuwa tunatokea sehemu mbalimbali za Tanzania kila mtu alikuwa anaenda kwa wakati wake chuoni kuitikia wito.

Cha ajabu tulipokwenda chuo kikaanza kutupa sababu zisizoeleweka mfano chuo hakina fedha kwa sasa; wengine wakienda wanaambiwa leteni risiti zote za kila muhula ili hali hawakuwaambia waende na risiti; hata kama risiti mtu hana mfumo wa malipo ulikuwa unafanyika au kuhifadhiwa kwenye system yaani mfumo wa computer. Hivyo ilikuwa rahisi tu kucklik jina data zote zinajionyesha.

Wamefanya hivyo mara nyingi na kutuzungusha kiasi kwamba mtu anatumia nauli kwenda na kurudi mfano kutoka Mtwara to Tanga au Mbeya to Tanga tumepoteza nauli zetu bila mafanikio. Hata tulipopeleka risiti kama walivyotaka bado wakatuambia chuo hakina fedha.

OMBI KWENU BODI YA MIKOPO:

1. Tunaomba mfuatilie hizo hela mlizorudisha zilitumikaje maana wahusika wahakusaini popote kama zimepokelewa.

2. Kwa kuwa hela zipo Sekomu na hawataki kuwarudishia wahusika waambieni warudishe huko bodi ili mtupunguzie deni maana deni ni kubwa.

3. Hatua stahiki za kinidhamu kwa wote waliohusika zichukuliwe kwani huu nao ni ufisadi na uhujumu uchumi wa nchi.

Nawatakia kazi njema.

N. B
Hili suala tumefuatilia kutoka mwaka 2015 hadi kufikia leo bila mafanikio hivyo tumeamua kuwapa taarifa ili mtusaidie kwani baadhi wameajiriwa mnawakata fedha ambazo hakuzitumia toka kwenu.
 
Hicho chuo kimezidi Uhujumu...sishangai kwa nn kimeendelea kufungiwa wakat wenzake wamefunguliwa,
Yaani kesi zao ni za pesa pesa tuu..
Huyo mkuu sijui Munga huko naskia ana jeuri si yaki toto, Ila KKKT......
 
Hivi mmewaandikia HESLB barua rasmi? Andikeni barua tatu. Moja kwa HESLB moja kwa permanent secretary Wizara ya Elimu na moja kwa waziri mkuu. Kila mmoja wenu aandike barua yake kuelezea madai yake mwenyewe msijumuishe. Hata kama wamezila watakopa wawalipe. Nishawahi kutana na ishu kama hiyo na tulilipwa pesa zetu. Kuweni serious ikibidi tafuten hata wakili wa kusimamia swala lenu ata awape ushauri wa kisheria jinsi ya kuliendea hilo swala.

Sent From Galaxy S9
 
Umeongea vzr Dada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mmewaandikia HESLB barua rasmi? Andikeni barua tatu. Moja kwa HESLB moja kwa permanent secretary Wizara ya Elimu na moja kwa waziri mkuu. Kila mmoja wenu aandike barua yake kuelezea madai yake mwenyewe msijumuishe. Hata kama wamezila watakopa wawalipe. Nishawahi kutana na ishu kama hiyo na tulilipwa pesa zetu. Kuweni serious ikibidi tafuten hata wakili wa kusimamia swala lenu ata awape ushauri wa kisheria jinsi ya kuliendea hilo swala.

Sent From Galaxy S9
Shukrani kwa ushauri wako tutajaribu kufanya hivyo hawa jamaa ni majipu ndio maana lichuo lao limefungiwa
 
Back
Top Bottom