Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,097
- 43,309
Na. M. M. Mwanakijiji
Watu wanapopata ajali na kuumia au kuangamia katika ajali hizo sisi tulio hai na tunaofanikiwa kufika kwanza katika eneo la ajali tuna jukumu la pekee la kuwaokoa walionusurika na kuhakikisha wako salama na kuwaepusha na majanga zaidi. Lakini zaidi sana tunalo jukumu la kimaadili la kuwahifadhi na kuwasitiri ubinadamu na utu wao wale ambao wamefariki katika ajali hizo badala ya kuanza kuwapiga picha katika saa ya mauti yao na kuzisambaza kama vile ni udaku.
Kinyume na hili kwa muda sasa jamii yetu imekubali na kuanza kuvumilia vitendo vya kukufuru miili ya marehemu kwa kupiga picha miili iliyopondwa na kuvunjika katika ajali kwa ajili ya aina fulani ya burudani na udadisi wa macho. Makala hii ni nzito* na ina lengo la kugusa dhamira; kuendelea kuisoma kunaweza kukuumiza hisia, kukupa mashaka na kukuondolea hamu ya chakula na kukupa wasiwasi. Tafadhali soma kwa tahadhari. (Wahariri wanaruhusiwa kuitumia jinsi ilivyo bila kubadilisha jina la mtunzi na kuhakikisha barua pepe mwishoni mwa makala inatokea).
* Natamani ninayoandika kwenye makala hii yangesemwa kwa namna fulani na viongozi wetu wa juu wa serikali au dini. Ni mzigo mkubwa kwangu.