Kweli watanzania wamepoteza maadili na utu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli watanzania wamepoteza maadili na utu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 30, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji
  Watu wanapopata ajali na kuumia au kuangamia katika ajali hizo sisi tulio hai na tunaofanikiwa kufika kwanza katika eneo la ajali tuna jukumu la pekee la kuwaokoa walionusurika na kuhakikisha wako salama na kuwaepusha na majanga zaidi. Lakini zaidi sana tunalo jukumu la kimaadili la kuwahifadhi na kuwasitiri ubinadamu na utu wao wale ambao wamefariki katika ajali hizo badala ya kuanza kuwapiga picha katika saa ya mauti yao na kuzisambaza kama vile ni udaku.

  Kinyume na hili kwa muda sasa jamii yetu imekubali na kuanza kuvumilia vitendo vya kukufuru miili ya marehemu kwa kupiga picha miili iliyopondwa na kuvunjika katika ajali kwa ajili ya aina fulani ya burudani na udadisi wa macho. Makala hii ni nzito* na ina lengo la kugusa dhamira; kuendelea kuisoma kunaweza kukuumiza hisia, kukupa mashaka na kukuondolea hamu ya chakula na kukupa wasiwasi. Tafadhali soma kwa tahadhari. (Wahariri wanaruhusiwa kuitumia jinsi ilivyo bila kubadilisha jina la mtunzi na kuhakikisha barua pepe mwishoni mwa makala inatokea).

  * Natamani ninayoandika kwenye makala hii yangesemwa kwa namna fulani na viongozi wetu wa juu wa serikali au dini. Ni mzigo mkubwa kwangu.
   

  Attached Files:

 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Global Publisher nadhani mnastahili kusoma hii kwa umakini.

  Tabia yenu ya kuchapisha picha za watu waiopatwa na umauti katika ajali mbalimbali inachefua na inaondosha kabisa misingi ya Utu.

   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  watu wengi wamekuwa na tabia hii ya kukimbilia na kupiga picha miili ya marehemu na wakati umefika naamini lazima tuachane nayo na kuanza kuonesha utu na ubinadamu. Sijui ni wangapi kati yetu wangeona ni jambo la kawaida ndugu yao aliyepatwa na ajali (awe mama, baba, dada, kaka, mtoto n.k) apigwe picha katika eneo la ajali na watu wenye udadisi na kuchapwa katika magazeti mbalimbali. Siku si nyingi tutapoteza kiongozi au viongozi katika ajali na watu watakimbilia kuwapiga picha katika ajali hilo na watawala watakuja juu kudai kuwa "ni ukosefu wa maadili" lakini sasa kinapofanyika kwa hawa kina Pangu Pakavu hakuna mtu anasema lolote lile.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilijua ni mada ngumu na nzito.. pole.
   
 5. m

  mapambano JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijafungua attachment, lakini nafikiri ujumbe nimeupata. Bora umeiweka hapa, kwa kweli nimeona picha nyingi tu zakuzalilisha badala ya kuhabarisha. Habari zina maadili yake, tatizo wengi wao elimu ya mambo ya habari hawana.
   
 6. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji sio tu kupiga picha ni ata kutangaza vifo vya watu bila ridhaa ya wanafamilia.. Mimi binafsi naona kuandika habari ya marehemu hapa JF au kwenye magazeti bila kuwa na ridhaa ya wanafamilia waliobaki sio vizuri. Maana wakati mwinginie wanafamila wengine hawajui kilichotokea mijitu inaanza kucomment.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unajua ndio maana wenzetu huwa wana utaratibu wa kutotangaza kifo cha mtu hadi "the next of kin" ameshapewa taarifa. Hata hivyo unapozungumzia public figures hilo linaweza lisihusu kwa sababu watu walioamua kuishi maisha yao publicly hata wakati wa mauti wanachukuliwa vivyo hivyo. Tatizo linakuja kwa mtu ambaye siyo public figure ambaye watu wanafanya haraka kutangaza kifo chake wakati hata ndugu wa karibu hawajajulishwa. NI suala la maadili tu.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,644
  Likes Received: 82,365
  Trophy Points: 280
  Tulikuwa tunaliongelea siku moja hili na mwanachama mmoja hapa jamvini. Ilikuwa ni kuhusu safari aliyoifanya. Sasa katika mazungumzo hayo akaniuliza kama ikitokea bahati mbaya nikafa utatangaza JF kwa kutumia jina langu la JF au jina langu la kweli? Basi ukawa ni mjadala mzito sana lakini kama nakumbuka vizuri tulikubalina kwamba kwa heshima ya familia, ndugu, jamaa na marafiki ni bora tu kama kutangaza ni kutangaza kwa jina la hapa JF na si la kweli. Hili la kutangaza mtu aliyekufa kabla ya waliomuhusu kufahamishwa rasmi ni muhimu sana likaheshimiwa. Mpaka hapo wafiwa watakapotoa ruhusa ya kutangaza jina/majina basi vyombo vya habari visiyatangaze majina hayo.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  najiuliza kwanini tumekuwa na haraka ya kukimbilia kuwapiga picha marehemu badala ya kuwasitiri?
   
 10. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hali hii inajidhirisha pia jinsi tunavyosafirisha miili, kwenye pickup Landrovers na miili mingine ikiwa wazi. Sidhani kuwa hata siku moja serikali yetu imeshafikiria kununua magari ya kubebea maiti kama hili hapa:

  [​IMG]
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,831
  Likes Received: 20,846
  Trophy Points: 280
  labda ndio matukio jamii yetu inapenda kuona?nasema hivi kwa sababu umeona jinsi watu wanavyokusanyika ikitokea ajali?mtu akigongwa lazima azungukwe na kundi la watu na sio kama wameenda pale kuokoa,la hasha wanaenda kuona tu kama sinema,sasa mwenye camera atapiga/atarekodi after 10 mins unaiona kwenye blog zilizochipuka kama uyoga.
  watu wakisikia milio ya bunduki wanakimbilia wakaone nani kapigwa risasi bila kujali kufanya hivyo wanahatarisha hata maisha yao.
  nafikiri watu wengi wanapenda sana kuona matukio kama haya ndio maana magazeti na blog zisizojali zinapost hizo picha na watu wananunua.
  having said that,sipendi kabisa hii tabia ya kupiga picha marehemu na kuzitoa hovyohovyo kwenye magazeti,sio ustaarabu kabisa na ni kukiuka maadili ya kazi na kijamii.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  umetoa pointi nzuri kweli nimeona polisi wanabeba miili kama vile mizoga ya ng'ombe. yaani hakuna maadili, heshima wala utu wa aina yoyote ile.
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Unamjua shigongo au unamsikia?
  Maadili anayojua yeye ni kufanya chochote adili au dhalili ilimradi akaunti itune.

  Heko MMM
   
 14. M

  Mikefe Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa mara ya kwanza tuko pamoja Mzee wa kijiji.Kupiga picha wafu si uwangwana.Let them rest in peace.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini kwanini sisi?
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Ulimbukeni wa teknolojia unatufanya tusahau ubinadamu wetu.

  Mie nisingependa kupigwa picha kama nyama buchani, na wala sipendi kuona picha ya mtu mwingine ya namna hiyo, iliyokosa staha za utu na kujaa kutojali.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  yaani kunapicha nimeziona hadi najiuliza hakuna hata mtu wa kukemea? Fikiri picha ya ajali ya Sokoine au wengine waliokufa katika ajali wakati huo zingekuwa zinapatikana papo kwa papo..
   
 18. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,831
  Likes Received: 20,846
  Trophy Points: 280
  kwasababu hatujali,nobody cares in tz.
  haya ni matunda ya kuwa disorganized from home to work place,government,watu,mipango in general ni shambles tu,completely disorganized
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  hilo jibu lako MBBX, lina ukweli sana.. na siku za hivi karibuni nimekuwa nikilisikia kwa watu wengi kweli.
   
 20. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,831
  Likes Received: 20,846
  Trophy Points: 280
  kwanini polisi wabebe maiti nyuma ya pick up wakati kuna ambulance?the answer is short,they dont care!
   
Loading...