Jana ilitokea nikawa naangalia kipindi cha TV (TBC1), nadhani kinaitwa Tuambie or Niambie sikumbuki sawa sawa. Kipindi kilikuwa kinahusu sheria hii mpya ya uhalifu wa mitandaoni na studio kulikuwa na wageni watatu (Mwanasheria kutoka Wizara ya Mawasiliano, Mratibu wa mambo ya mtandao kutoka polisi na mgeni mwingine mmoja).
Akatokea mwananchi mmoja akapiga simu akauliza hatua ambazo anatakiwa kuzifuata ikiwa atapata ujumbe wa kuudhi au matusi kwenye simu yake. Akasema kwa mfano wakati wa campaign za uchaguzi wa mwaka huu ikitokea akapata ujumbe wa kuudhi kwamba "Chagua CCM" achukue hatua gani kushughulika na ujumbe huu wa maudhi kwake ?!
Yaani imefikia hata ujumbe wa campaign wa CCM wengine wanachukulia kwamba ni ujumbe wa kuudhi (kama matusi vile)!.
Kweli watu wana hasira na CCM !