Kweli Watanzania wameichoka CCM

Kweli Watanzania wameichoka CCM

Kuna vijana juzi walipeana adhabu kama mmoja atashindwa kutimiza majukumu waliyowekeana, moja ya adhabu yao ni kuvaa Tshirt na kofia ya CCM kwa siku nzima ama fine ya 100,000/-.

Cha ajabu vijana wengi walikubali kulipa hiyo fine.

Duuu,ebwanae waacha hiyo ni hatareeeee
 
ah hahaha haaaa hahaaaa, ni kweli maana sheria haijatafsiri kitu kibaya ni kwa kiasi gani
hivyo yoyote anayeona hajafurahishwa nacho anaweza akashitaki

Ni kukubaliana tu mkuu,kama kwenye simu yako kunaingia msg husiyohitaji kutoka mtandaoni ni safari mahakamani
 
naona watu wangombana na neno ccm, eti ilaaniwe ccm, wewe unadhani hapo nani atalaaniwa ni neno ccm au ni watu waloko ccm
 
Ungetusaidia kama ungetuwekea jibu walilomptia huyo muuliza swali, ili tuweze kufahamu hatua za kuchukuwa pindu tutakapopata huo ujumbe wa kuudhi wa CHAGUA CCM.

Mkuu,vita haina macho ukipata ujumbe kama huo ni kwa pilato tu
 
Issue sio ubora, issue ni fedha zilizotumiwa kujenga zimetoka wapi?.........Jibu ni Mkopo.......Kama ni mkopo, uliidhinishwa na bunge kama sheria inavyosema?

Jibu ni hapana, kwa nini hazikuidhinishwa? Jibu ni kwamba mikopo ni aina mpya ya UFISADI, no body knows how much kimekopwa, kwa ajili gani na kutoka vyanzo vipi........Deni la taifa sasa lipo kwenye Tsh trilioni 30+. kwa mwendo huu CCM itaikabidhi nchi kwa waliowakopesha muda si mrefu.

Duu mkuu ndio tunauzwa kama watumwa?
 
Porojo ....
kaka wewe unaishi Tanzania ipi? Fanya jaribio chanya, Chagua mkoa wowote ule, kisha chagua kijiwe chochote kile chenye vijana 10 na kuendelea - fika pale anza kujieleza kwamba wewe unatoka Lumumba!! na lengo lako hasa umefika pale kutafuta wanachama wapya wa CCM hasa vijana - Yatakayokupata hapo uje humu utupatie ushuhuda.

Ushauri: nenda ukiwa umevaa helmet kabisa.
 
Chama kimoja kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 lazima kitachukiwa hata kama kitajitahidi kutenda mema. Watu wangependa waoine mabadiliko. CCM kinaweza kikajinasibu kwa kujenga barabara nyingi za lami, lakini swali zina ubora kiasi gani. Kabla hatujapongeza juhudi hizo za serikali tujiulize, je barabara hizi zimejengwa kwa pesa zetu au kwa mikopo? Kama kwa sasa deni linakaribia trillion 40 kutoka trillioni 7 wakati serikali ikiingia madarakani hatuna sababu kubwa ya kupongeza. Baba akijenga nyumba nyingi kwa fedha ya kukopa kutoka benki watoto wake hawana sababu ya kushangilia kwani iko siku akishindwa kulipa deni zitapigwa mnada. Huwezi kushangilia kujenga nyumba nyingi za kisasa wakati hati za nyumba hizo hunazo. Nyumba ni hati, kama huna hati nyumba hiyo si ya kwako. Tutafakari.

Umenikumbusha jana jioni/usiku niliona kipindi cha bunge akichangia mbunge mmoja wa CUF Zanzibar/Pemba. Nilicheka sana maana alikuwa akikazia kaulizake kuwa CCM imechokwa sana na hata watalofanya haisaidii, yaani wakijenga barabara na wakiacha kujenga ni sawa, alimradi chochote watakachofanya hata kiwe chema jibu ni kuwa wamechokwa. Niliwaangalia wabunge wa CCM wakiwa wamekodoa mimacho wakitabasamu kwa tahayari, loh mwaka huu sipati picha kitakachojiri
 
Hasa nikiangalia hawa ccm huko dodoma jinsi wana michango ya hovyo natamani nilale kesho niamke nikute ndio siku ya kupiga kura
Na siku hiyo ni tiki kwa ukawa kuanzia rais hadi diwani

Na wakijirigo wakaweka na karatasi za chenge ni HAPANAAAA
 
kaka wewe unaishi Tanzania ipi? Fanya jaribio chanya, Chagua mkoa wowote ule, kisha chagua kijiwe chochote kile chenye vijana 10 na kuendelea - fika pale anza kujieleza kwamba wewe unatoka Lumumba!! na lengo lako hasa umefika pale kutafuta wanachama wapya wa CCM hasa vijana - Yatakayokupata hapo uje humu utupatie ushuhuda.

Ushauri: nenda ukiwa umevaa helmet kabisa.
Mngekuwa na akili timamu mngejiuliza kwanini CCM inaendelea kuchaguliwa na watanzania licha ya propaganda zote hizi!
 
Ama kweli siasa za Tanzania zimebadilika sana na mwamko wa wananchi wa kawaida sasa ni mkuba kuliko kipindi chochote tangu uhuru. Huweziamini nimemsikia mama mmoja mtu mzima mchana huu akitoa kauli hii:
UKIONA KIJANA WA LEO ANASHABIKIA CCM, UJUE AKIJA KUZEEKA LAZIMA AWE MCHAWI!!
Huu ni mfano mmoja tu wa jinsi watu leo walivyo na chuki na chama tawala!! Hatima ya hali hii ni nini?
 
thats true. jitu limejaa shda, ila linasema ccm ndio wa kututawala
 
Mnunulie mwanao mdogo kitu anachokipenda sana kama vile baiskel au mdoli mwambie zawadi yako mwanangu. kesho yake umuibie ukafiche mbali naye, alafu akianza kutafuta mwambie ccm wamekuibia mwanangu ili akue akielewa kwamba ccm ni adui namba moja wa maisha yetu.WATUMIE WAZAZI WOTE PLZ.
 
Huyo mama naomba namba yake anafaa kulia 0712
 
Back
Top Bottom