Ralphryder
JF-Expert Member
- Nov 16, 2011
- 5,599
- 1,798
hahahahaha...mie nilkua na mpira wasiponipanga tu nilikua naondoka nao nyumbani
UNavaa Chachacha ndio mjanja sana shule au kiatu kimeandikwa Zamoyoni Mogela sijui kama wachezaji walikuwa wanapata hata senti kutokana na viatu vile!
enzi hizo ukitembea kifua wazi unaitwa gangwe..watoto wakikoromeana kidogo unawahi kuchota michanga na kuwageukia mmoja mmoja"puta,tia dole,vuka mstari"anayegoma kuputa kaogopa na ugomvi unaisha hapo hapo...
mnapinga bong'oa ukiinama unachukua bonge la shuti la ******..
unanyimwa namba mpirani ukicheza kilazima watu utawasikia"nyama huyo"hapo ukigusa mpira unastukia tama chini...
Kitaani tulikuwa na gari la kamba kuubwa hilo, mie nilikuwa napenda kuwa konda,
ilikuwa nikitoka kucheza mpira na kuskia kuwa mdingi karudi home najifuta miguu kwa mate kuepuka mboko...
pia kulikuwa na sinema za mabox
kulikuwa na mchezo wa baba na mama mnajipikilisha kwenye vifuu vya nazi duh...enzi zile...
kulikuwa na mchezo wa baba na mama mnajipikilisha kwenye vifuu vya nazi duh...enzi zile...