muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Ilikuwa jioni na ikawa asubuhi atimaye muda ukawadia kwa watanzania kujua mbivu na mbichi, tukumbuke baada tu ya kamati ya kwanza kutoa taarifa zake, mh. Tundu Antipas lisu alitoa povu sio la nchi hii kuwa sasa serikali ilichokifanya itapoteza mahusiano ya kidiplomasia na itashtakiwa na haitabaki Salama kwenye haya masuala ya makinikia.
Mheshimiwa huyu alitoa hoja nyingi akihusisha mikataba iliyoingiwa na kesi ambazo zitasikilizwa huko ughaibuni alisisitiza serikali haiwezi kushinda kesi hizo na tutawalipa fedha nyingi hawa ambao sisi tunadhani ni wezi.
Ingawa anakiri kuwa wametuibia kwa miaka mingi.
Kwangu kwa uwezo wangu wa kawaida nilimuweka mheshimiwa huyu upande ambao lazima uchukuliwe kama angalizo tu wakati serikali inaendelea kumfukuza mwizi kimyakimya.
lakini kinachoelekea ni kwamba kuna ukosefu wa uzalendo, kuna watu wapo kwa ajili ya upinzani kwa kila jambo linalofanywa na serikali, watu hao hawapo kwa ajili ya hoja ya kujenga nchi bali ni kubisha na kupambana na maendeleo yanayopangwa na serikali yakwame ili ipatikane kick ya kuongea kwenye majukwaa.
Muda mrefu nilipenda kuona uzalendo kwanza lakini yale yalioombwa muda mrefu pia mheshimiwa Rais wetu amesikia na amerudisha mikataba ya kisheria bungeni kwa ajili ya kujadili na kufanya marekebisho ambayo kwa kiasi flani inaweza kuwa tija kwa taifa.
Ombi langu ni moja tu hiyo kamati wangejaa wanasheria mchanganyiko toka vyama vyote, wachumi wa vyama vyote, sionagi tija sana nikiwa nasikia ndiyooooooo bungeni kwa sifa za wawakilishi waliopo mule ya kusoma na kuandika, tunaweza tukawa tunatwanga maji kwenye kinu ingawa naamini kuna vichwa makini na kwa uzalendo waliokuwa nao na wakiweka pembeni uvyama tutapata mikataba mizuri na sio ya kinyonyaji kama hii.