Kweli Tanzania tumefikia hapa?

Kweli Tanzania tumefikia hapa?

usawa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2014
Posts
454
Reaction score
154
Tunapewa huduma mbovu za bima ya afya kupitia Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF), huku kuna hela tunakatwa kazini. Kuna umuhimu wa serikali kuwalipa wahusika hela yao ya afya mkononi ili wakiumwa waende hospitali kujitibu wenyewe kuliko kukabiliana na kile ambacho huwa wanakutana nacho kwenye mfuko huu.

Kinachoshangaza zaidi ni kwamba viongozi wetu na wa mfuko huu wanajua huduma mbovu zinazotolewa lakini wamenyamaza. Kuna mambo mengi mabaya yanafanyika ila hili la bima ya afya limezidi.
 
Watanzania kwa kulalamika, mko vizuri. Sasa kuna nini cha kulamikia hapo?
 
Sisemi hakuna shida na hospitali zilizoidhinishwa na mfuko lakini kwa asilimia kubwa mfuko umesaidia wengi. Ukishindwa hospitali moja unahamia nyingine. Zipo baaadhi ya hospitali wana care kwa bima hiyo hiyo vizuri. Ni uchaguzi mbovu wa hospitali ndio unakufanya ulalamike.
 
Hii kitu inaitwa Bima ya Afya ya NHIF ni majanga. Kumbuka wafanyakazi wengi wa serikali wako kwenye hii bima ya afya. Cha ajabu baadhi ya hospitali za wahindi kama Agha Khan, Buruhani na Hindu Mandal ukienda na kadi ya NHIF inayoonyesha wewe unafanya kazi serikalini basi hawakupi huduma, wanadai cash ndio utibiwe. Ukiwa mfanyakazi wa shirika kama TANESCO unapewa huduma kwa kutumia kadi. Sasa unajiuliza hivi serikali imefikia hatua inadharaulika kiasi hiki? Kwamba wafanya kazi wake wananyimwa huduma?

Mleta mada has a point to make.

Tiba
 
Watanzania kwa kulalamika, mko vizuri. Sasa kuna nini cha kulamikia hapo?

yupo sahihi kulalamika, wafanyakaz wanakatwa hela kila mwez lkn ukienda hospital wanakwambia hakuna, wanakuandikia then wanasema ukanunue, huu ni uonevu mkubwa.
 
Inawezekana umepata usumbufu mkubwa kutokana na hicho ulichokisema, ,lkn kwa sasa bima ya afya NHIF imekuwa ni mkombozi mkubwa sana hasa kwa vipimo ambavyo pengine tungeshindwa kuvilipia , kutokana na vipato vyetu , ni kweli kuna baadhi ya hospital ambazo bado zinatoa huduma mbaya kwa wagonjwa wa bima , lkn pamojaa na yote kuna hospitl ambazo ukienda unaoneakana lulu hasa pale unapokuwa na bima, hii ni kwa sbb ya motisha mbalimbali zinazotolewa kwa madaktari pamoja na manesi wanaofanya kazi za bima kwa ufasaha na kwa kuhudumia mgonjwa vzr.

Angalizo au pengine maoni kwa watu wa bima , ni kusisitiza na kuelimisha wagonjwa wa bima lkn pia kutembelea hospital na vituo vya afya kuona ni namna gani wagonjwa wanapewa huduma

Na sisi wapewa huduma pia kuwa na utaratibu na subra , kwani haimaanishi kwamba kuwa na na bima ni kukiuka taratibu za hospital husika mfano kuwa katika foleni na kutokushuku kwamba pengine unatendewa hivyo sbb una bima .
 
tatizo nyie mnaenda kwenye vijidispensari eti unategemea upate dawa..hebu nenda kwny mahospitali ya maana kama vile regency,tmj, uone huduma utakazopewa kwa hiyohiyo bima nadhani utakuja kubadilisha mada hapa
 
Unamuongelea mwanachama wa NHIF aliepo wapi? make hao regency/tmj hawapo sehemu zote hapa Nchini wakati wanufaika/wanachama wa NHIF wapo Nchi nzima!
Ebu jaribu kwenda hospitali za huko wilayani ukaone unyanyapaa wafanyiwao wanufaika wa NHIF... hata nesi tu hakuthamini ikiwa utakuwa mwanachama wa NHIF.
 
nimeenda hospitali kubwa za mkoa nkafanyiwa hvyo.....
 
Mleta mada punguza jazba, lkn pia jaribu kufanya uchunguz kabla ya generalization. Kuna baadhi ya Mikoa ukiwa na bima ya afya utahisi wewe ni Malaika lkn pia kuna baadh ya sehem ukiwa na bima ya afya hupat huduma stahiki.
 
usawa wa kulia

'To generalize is to be an idiot', unaposema mnakatwa fedha halafu mnapewa huduma mbovu, ni wewe na nani? Wa wapi? Toka lini? Huduma gani mbovu uliyopata? asehemu gani ulikopatia hiyo "huduma mbovu"?

Sasa ;
You should understand hizo kadi zinatofautiana; utaona brown card, green card, hivyo huduma ziko restricted kulingana na aina ya kadi.

Ingawaje unaona fedha unayokatwa ni "kubwa" bado sidhani kama inakidhi matibanu/ huduma za afya unayopata, Say unakatwa 75,000/= or 100,000/=Tshs na una dependants kadhaa! Hivi unafikiri hiyo inatosha hata kwa mwezi (say consultation ya familia nzima)?, sawa naelewa si kila mwezi mtaugua au mtafanya check up!

Umekwisha fikiria vipi kuhusu dawa za milioni tisa hadi ishirini na saba za saratani? vipi kuhusu dialysis? Umekwisha fikiria kuhusu vipimo vikubwa kama MRI na CT Scan, umekwisha fikiria operation hasa ulimwengu huu wa ajali kila leo?

Umefikiria kuhusu watu wenye magonjwa ya muda mrefu na yenye kuhitaji dawa mf. Shinikizo la damu (Hypertension/High Blood Pressure), Kisukari/Diabetes, Magonjwa ya mifupa, figo n.k then ulinganishe na hicho kiasi "kikubwa" unachodhani unakatwa?

I agree with you, kuwa kadi wakati fulani haisaidii (lakini issue hapa si upatikanaji wa huduma kwa kadi, ila ni huduma zenyewe), mfano hospitali ndogo, Vituo vya afya n.k.
Pia kuna baadhi ya dawa huduma (vipimo na dawa) HAVIPASWI kuwa katika sehemu hizo(health centre, hospitali ndogo) na hata kama daktari akiandika utarudishwa tu.

Mfuko wa bima ya taifa (NHIF), huchelewesha malipo kwa vituo vya afya na hospitali (isipokuwa kwa hospitali "kubwa"), sasa ucheleweshwaji huu, humuathiri mteja kwa madaktari/ watoa huduma kuwaepuka wateja/ wagonjwa kwa kuwa pesa yao hucheleweshwa pia.

Sasa restriction, hizi ndizo zenye kuleta usumbufu, lakini it is 'insane' dunia ya leo kukaa bila bima, hasa ya afya.
 
Last edited by a moderator:
Unamuongelea mwanachama wa NHIF aliepo wapi? make hao regency/tmj hawapo sehemu zote hapa Nchini wakati wanufaika/wanachama wa NHIF wapo Nchi nzima!
Ebu jaribu kwenda hospitali za huko wilayani ukaone unyanyapaa wafanyiwao wanufaika wa NHIF... hata nesi tu hakuthamini ikiwa utakuwa mwanachama wa NHIF.
hauko sahihi hukohuko mikoani kuna hosp.kubwa tuu za serikali na binafsi wanatoa huduma nzuri sana kwa wanachama wa NHIF..labda nnyie wenzangu mna bahati mbaya
 
Hii kitu inaitwa Bima ya Afya ya NHIF ni majanga. Kumbuka wafanyakazi wengi wa serikali wako kwenye hii bima ya afya. Cha ajabu baadhi ya hospitali za wahindi kama Agha Khan, Buruhani na Hindu Mandal ukienda na kadi ya NHIF inayoonyesha wewe unafanya kazi serikalini basi hawakupi huduma, wanadai cash ndio utibiwe. Ukiwa mfanyakazi wa shirika kama TANESCO unapewa huduma kwa kutumia kadi. Sasa unajiuliza hivi serikali imefikia hatua inadharaulika kiasi hiki? Kwamba wafanya kazi wake wananyimwa huduma?

Mleta mada has a point to make.

Tiba
Kwa sababu serikali haiwalipi.!!!
 
tatizo nyie mnaenda kwenye vijidispensari eti unategemea upate dawa..hebu nenda kwny mahospitali ya maana kama vile regency,tmj, uone huduma utakazopewa kwa hiyohiyo bima nadhani utakuja kubadilisha mada hapa
Niko Arusha hospitali ya Mount Meru (hospitali ya mkoa) haina dawa kitengo cha bima. unaambiwa ukanunue. msibishe tu hoja za watu
 
NHIF wanazingua sana! mi nafanya kazi kwny company moja ya kusupply madawa kwny hospital sasa ona, unadai ela ya kusupply dawa hospital kwa miezi nao wanakwambia tunadai kwa NHIF kwa miaka so hatutaweza kukulipa coz NHIF hajatulipa kwa mwaka sasa,kuna hospital moja ya private mfano inadai 1.5 billion kwa NHIF sasa hapo ukienda na kibima chako NHIF watakupa huduma kweli na kumuacha mtu anayetoa cash.Tafakri
 
Back
Top Bottom