Kweli Tanzania inahitaji Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya?

Sera ya Majimbo hiyp, haitufai kwa sasa.


Ndugu, hitimisho lako lingesaidia mjadala kama ungeisumbua akili yako kuweka angalau premises ama sababu angalau tatu kushadadia hoja yako.
Jiulize,kwa mfano nami nitumie staili yako kwa kutoa kauli ''sera ya majimbo inafaa kwa nyakati hizi'' na nikaishia hapo bila kuweka ufafanuzi wowote...Baada ya muda akatokea na mwingine huku akirejea kauli yako ya awali.Unadhani kutakuwa na majadiliano hapo?
Jiepushe na kile kinachofahamika kama ''intellectual laziness''!
 
Hii itakuwa tz tu na lazima uwe umelewa au umevuta kumuelewa huyu tobo lisu

naanza kuhisi jf imevamiwa kwa kiasi kikubwa sana kuliko hapo awali, sidhani lugha kama hii inaweza toka kinywani mwa member wa inayoitwa JF The Home of Great Thinkers'' hope its now sound like The home stupid Language.....
Kwani hata hukubariani na jambo kutoa lugha kama hiyo ni halali kwa mtu uloenda shule ukaelimika? Tujirekebishe wadau
 
Hoja ni nzuri, ila nionavyo mimi ni bora kuwaondoa kabisa wakuu wa mikoa (kusave pesa za walipa kodi), halatu tubaki na wakuu wa wilaya ambao ndo watachaguliwa na wananchi kama lisu anavyoshauri
 
Kwani wabunge wanaochaguliwa na wananchi mpaka sasa wamedhihirisha kuleta maendeleo gani kwa wananchi zaidi ya kutetea maslahi ya vyama vyao?
Rais ni lazima awe na wawakilishi katika mikoa na wilaya. Hawa ndio watu ambao kila asubuhi wanawajibika kumpa Rais hali ya usalama katika maeneo yao. Hata ukisema wakuu wa mikoa na wilaya wapigiwe kura, bado rais atahitaji watu wengine kwa kazi hiyo, hata kama hawataitwa wakuu wa mikoa au wakuu wa wilaya.
 
Ukishakuwa na RAS, DAS na DED huan haja tena ya kuwa na RC na DC
Hakuna siasa hapo ni kazi tu
 
jamani kwa wananchi wa kawaida wanafahamu dadizo la MA-DED na Ma-RAS kwa mfumo wowote ule wa chama kitakachokuwa madarakani madc na marc ni muhimu ni kuliko hao wa halmashauri ambao wengi wao ni wezi waliokubuhu wa mali za umma

Kwani hao ma dc ndo siyo wezi? Sema sehemu za kula kwao ni finyu sana hawana mafungu. Mi miongoni mwa mafisafi hawa.
 
Yawezekana hukubaliani na hoja za Lissu ,lakini kamwe hiyo haikupi uhalali wa kutoa lugha chafu.
Jisikie aibu kutamka maneno yasiyo na staha kwa wanadamu wenzako.
Vinginevyo hapa si mahali mwafaka kwako.
Kama huwezi kuhimili mikiki ya kuwa hapa,kaa barazani ,piga umbea na wambea wenzako.
Ona aibu.

nimeipenda
 
We dont need Dc and the company scratch them off.
Tunahitaji mkuu wa mkoa tua atakaechaguliwa na wananchi na wabunge, mameya na wenyeviti wa manispaa thats it. Tukibakiza ofisi ya mkuu wa mkoa na watendaji wachache na kufuta vyao kibao kutokana na mahitaji ya mkoa. Hatuhitaji wakuu wa wilaya, wakati tuna mameya na wavyeviti wa manispaa. Kila manispaa itawajibika kwa mkuu wa mkoa kama kiongozi mkuu. Tutapunguza kwa kiasi kikubwa sana matumizi yasiyoyalazima na kufanya mkoa uishi kutokana na mapato yake.

Mkoa lazima uwe na vyanzo vya uchumi na TRA wachukue kodi yao kwa ajili ya miradi mikubwa ya kitaifa kama barabara za kuunganisha mkoa kwa mkoa wilaya kwa wilaya, umeme, na kusaidia baadhi ya taasisi za mkoa ambazo zitaonekana zinafaa kutokana na katiba. hii ndio njia pekee ya kuendelea kwa mtaji huu wa mkuu wa mkoa, wialaya, nk kuwajibika kwa mtu mmoja Raisi na kutolewa sehemu zisizojulikana ama kwa mapenzi au ushikaji wa Raisi bila kujali uwezo na elimu, utashi nk hatuwezi kuendelea hata cm moja
 
We dont need Dc and the company scratch them off.
Tunahitaji mkuu wa mkoa tua atakaechaguliwa na wananchi na wabunge, mameya na wenyeviti wa manispaa thats it. Tukibakiza ofisi ya mkuu wa mkoa na watendaji wachache na kufuta vyao kibao kutokana na mahitaji ya mkoa. Hatuhitaji wakuu wa wilaya, wakati tuna mameya na wavyeviti wa manispaa. Kila manispaa itawajibika kwa mkuu wa mkoa kama kiongozi mkuu. Tutapunguza kwa kiasi kikubwa sana matumizi yasiyoyalazima na kufanya mkoa uishi kutokana na mapato yake.

Mkoa lazima uwe na vyanzo vya uchumi na TRA wachukue kodi yao kwa ajili ya miradi mikubwa ya kitaifa kama barabara za kuunganisha mkoa kwa mkoa wilaya kwa wilaya, umeme, na kusaidia baadhi ya taasisi za mkoa ambazo zitaonekana zinafaa kutokana na katiba. hii ndio njia pekee ya kuendelea kwa mtaji huu wa mkuu wa mkoa, wialaya, nk kuwajibika kwa mtu mmoja Raisi na kutolewa sehemu zisizojulikana ama kwa mapenzi au ushikaji wa Raisi bila kujali uwezo na elimu, utashi nk hatuwezi kuendelea hata cm moja

NI kweli kuna kila sababu ya kuwaondoa hawa viongozi wa fadhila wakuu wa wilaya wakina Nape.

Mimi sioni kazi yao wanayofanya zaidi ya kutumia fedha zetu za kodi.
 
Hakuna haja ya kuwa na vyeo hivi kwani havina tija na vinadumaza maendeleo ya nchi kutokana na matumizi yake makubwa ya ofisi zao. Kazi za maDC zinaweza kufanywa na District executive directors na kazi za MaRc zinaweza kufanywa na Regional Administrative secretaries. MaDC na MaRC ni mzigo wanaotwishwa wananchi kwa sababu ya kuwapa vyeo wapambe wa wanasiasa!! Kutaka wananchi ndio wawachague MaDC na MaRC ni kuwasumbua wananchi kwani wanachagua madiwani na wabunge kama wawakilishi katika sehemu zao!

Lengo la serikali yoyote duniani ni kutoa ajira nyingi iwezekanavyo na ukuaji wa serikali unapimwa kwa kiwango cha matumizi Bulesi hili nalo unasemaje?
 
Last edited by a moderator:
Ukishakuwa na RAS, DAS na DED huan haja tena ya kuwa na RC na DC
Hakuna siasa hapo ni kazi tu
Umemsahau mwenyekiti wa halmashauri/meya wa mji/jiji. Ningeelewa iwapo huyu ndo angechukua nafasi ya DC. Upatikanaji wake ungekuwa tofauti kidogo....apigiwe kura na wilaya nzima husika na sio kata moja halafu ati madiwani watuchagulie huyu mtu. Vyombo vya ulinzi na usalama vitoe ushauri kwake juu ya mambo ya kiusalama wilayani. DED kwa upande wake ni vyema awepo na majukumu yake, na bado aendelee kusimamiwa SIO kuwajibika kwa DC huyu niliyemuelezea upatikanaji wake!
 
Mfumo wa sasa wa Wakuu wa mikoa na Wilaya sio mzuri kwasababu zifuatazo

1. Uhamisho: Mfumo wa sasa ni kwamba Viongozi hawa wakifanya vizuri wanahamishwa kwenye wilaya au mikoa mikubwa na yenye maendeleo. Hii inasababisha wale viongozi wasio na utekelezaji mzuri au uzoefu wawekwe kwenye sehemu ambazo ndiyo zinahitaji viongozi wazuri zaidi.
2. Mapenzi: Viongozi wengi wamepangiwa mahali pa kazi ambako hawana mapenzi nako na wanajaribu kila siku kutafuta mbinu za kuhama. Hii inasababisha hawa watu kujihusisha na siasa zaidi na kujuana kuliko kusaidia sehemu ya kazi.

Matatizo haya yanaweza kutatuliwa kwa kuwaajiri watu Local wenye uwezo, mapenzi na wenyeji wa mikoa hiyo. Itafanya hawa watu wafanye kazi kusaidia nyumbani badala ya kutafuta transfer.Vilevile ingekuwa vizuri hawa watu wawe wanachaguliwa na wananchi wao. Hii itasaidia kuwafanya hawa watu wasaidie zaidi kwenye maendeleo.
 
mkuu, katika mfumo wa kidemokrasia wakuu wa wilaya na mikoa hawaitaijiki kabisa kwa maana kwenye demokrasia nakuunga mkono uongozi utokane na wananchi wenyewe kwani wananchi wenyewe wanao uwezo na hekima ya kumchagua ni nani anafaa kusimamia maendeleo yao ya kila siku na siyo kuchaguliwa na mtu aliyeko dsm ambaye hajui lolote kuhusu wilaya usika.

kama ulivyokiri wewe mwenyewe kuwa wegi hawana mapenzi na pale wanapopelekwa kwahiyo utaona kuwa hakuna mwenye mapenzi popote atakapopelekwa kuliko wale wawaoishi mahala usika.

nini cha kufanya.
hata kama utaonekana umuhimu wa kuwepo kwa wakuu wa wilaya au wa mikoa basi wananchi wa eneo usika ndio wanajua nani anafaa na nani hafai kwahiyo wapewe mamlaka ya kuchagua na kufukuza na siyo mtu anayeongoza kwa kutumia remote control kutoka dsm. wakati wa kuchaguliwa viongozi umekwisha kwani msingi mkubwa wa kuwa na wakuu wa wilaya na mikoa asili yake ni ya kikoloni ili mkoloni hawezi ku control himaya zake kwahiyo alikuwa hawezi kuchagua mtu wa eneo usika kwa maana asingeliwakilisha maslahi yao na ndio maana walikuwa wakituma watu wa mbali kama anavyofanya jk hivi sasa.
 
Back
Top Bottom