Kweli Tanzania inahitaji Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya?

Ningu

Member
Feb 5, 2011
75
10
Hesabu rahisi zinaonyesha toka uchaguzi mkuu Oct 31, 2010 mapa leo ni siku 117 na mikoa kama Geita, Katavi, Njombe, Simiyu, Dar to mention a few haina wakuu wa mikoa na inaendelea salama.

Ili kupunguza matumizi ya kodi zetu, kuna haja kweli ya kuendelea na kada hii?

Nadhani ni muda mwafaka wa kuangalia ni jinsi gani tunajitawala na kujiletea maendeleo!

Na Reginald Miruko, Mwananchi (email the author)

Alhamisi, Aprili 18, 2013

Dodoma. Serikali ya Chama cha Mapinduzi haitaachana na mfumo wa uongozi unaowatumia wakuu wa mikoa na wilaya, kwa sababu nafasi hizo ni muhimu katika kutawanya madaraka ya Rais.

Hayo yalielezwa bungeni juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Ghasia alisema CCM inayotawala inaona mfumo huo ni muhimu, labda iwapo watu wengine wanaoupinga wakishika madaraka wanaweza kuuondoa, jambo ambalo hata hivyo hadhani kama linaweza kutokea.

Vilevile Ghasia alisema watumishi kadhaa wa halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria na nidhamu.

Alisema aliyekuwa mkurugenzi mtendaji suala lake limefikishwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), mweka hazina amefukuzwa kazi na Ofisa Mipango amepewa onyo kali.

Kuhusu maombi ya wabunge wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (Temeke) na Idd Azzan (Kinondoni) waliotaka mkoa huo ugawanywe na kupata wilaya zaidi, Ghasia alisema suala hilo linapaswa lianzie kwa wananchi wenyewe na Serikali italifanyia kazi.

Chadema kimekuwa kikipinga kuwapo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa sababu hawatumikii wananchi zaidi ya mamlaka (Rais) iliyowaweka.

Awali, wakuu wa wilaya hawakuwamo kwenye Katiba, lakini baada ya suala hilo kuibuliwa na Mbowe, Serikali iliamua kufanya mabadiliko na kuwaingiza kutambulika kikatiba.
 
uko sawa mkuu hata wakuu wa wilaya hawahitajiki nadhani katibu tawala wa mkoa anatosha,
 
Hata ukienda wilayani ni yale yale tu; Mkuu wa wilaya, afisa tawala, mkurugenzi wa wilaya na mbunge wana kazi gani wote hawa si bora abaki mbunge na mmoja kati ya hao?
 
Ndiyo sababu tunahitaji chama mbadala wa kuthubutu kuondoa mazoea mabovu ya kiutendaji katika serikali, 'change we need!..'
 
tunahitaji wakurugenzi wa wilaya tu, watakao wajibika tamisemi baada ya kuajiriwa kwa interview na si kuteuliwa kama ilivyo sasa. wakuu wa wilaya na vitengo vyote katika ofisi za mikoa are totally useless. Ni vituo vya kufuja pesa za umma tu.
 
Wakuu wa wilata na maafisa tawala wa wilaya hawahitajiki.Wilayani abakie mkurugenzi wa wilaya tu.Wengine hao wanatumia bure tu kodi zetu kwani wanafanyakazi za kujirudiarudia tu.Tunahitahi vingozi wachache na wenye ufanisi.Maana tunaona wakuu wa wilaya wengi ni kama vyeo vya kupewa asante tu.Jamani tuige mifumo wa nchi za wenzetu.
 
Hilo la mkuu wa mkoa sawa! Lakini kwa kupunguza matumizi ya kodi? inabidi tujue kama punguzo linapelekwa kwa huduma za jamii au matumbo ya waheshimiwa wachache na nyumba ndogo zao? Just thinking aloud!
 
Ni kweli hakuna haja ya kuwa na ho ma RC hata kidogo.
Hata hivyo kama ukikumbuka chanzo cha kuanzishwa kwa RC post ilikuwa ni kuwatuliza wanajeshi na kuogopa baadhi ya mikoa kujitenga kipindi kile, hivyo ilikuwa ni kwa security reasons ndio maa unaona wengi huwa ni makannali fulani au wanjeshi wastaafu.
Wakati wa sasa na zamani si sawa tena, ndio maana katika hiyo katiba mpya moja wapo tutakalopenda kuangalia ni kutoa hizo nafasi zote kabisa pamojana DC zote hizo nafasi zimeshakuwa ni ulaji tu wa kisiasa zaidi.
Je wakitoka tutapenda hizo nafasi ziweje??
je zisiwepo kabisa?
au kuwe na magavana watakaokuwa wanateuliwa na wananchi ambao wanaweza kuwajibishwa na wananchi waliowachagua??
au amaoni yenu ni yapi?
Hesabu rahisi zinaonyesha toka uchaguzi mkuu Oct 31, 2010 mapa leo ni siku 117 na mikoa kama Geita, Katavi, Njombe, Simiyu, Dar to mention a few haina wakuu wa mikoa na inaendelea salama. Ili kupunguza matumizi ya kodi zetu, kuna haja kweli ya kuendelea na kada hii?
Nadhani ni muda mwafaka wa kuangalia ni jinsi gani tunajitawala na kujiletea maendeleo!
 
Jamani watanzania wenzangu kuna umuhimu gani wa kuwa na wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini?kwanza ni zipikazi zao?kama ni maswala ya kusimamia maendeleo kuna wakurugenzi wa miji na halmashauri wanatosha, kama tulirithi haya mambo kwa wazungu sasa yafike mwisho.
 
Hawa ni viongozi wa kisiasa na kwa nchi ambazo hazina majimbo hawa ndiyo wawakilishi wa serikali kuu. Wakurugenzi wa Halmashauri ni wataalam ambao kwa set up yetu wako chini ya Local Government. Bado kuna haja ya kuwa na viongozi wa kiserkali (serikali Kuu) ambao ndiyo wsimamizi wa shughuli za kiserikali huko mikoni na wilayani. Kinachohijika ni ku-redefine upya majukumu yao na kuwasimamia kwa karibu ili ikiwezekana nao wawe na performance agreements upon which to assess their performance in the course of the year under review.
 
Nizipi sifa za mtu kuwa mkuu wa mkoa/wilaya kwani wapo wenye uwezo mdogo sana kiakili na kielimu wapo walioshindwa kuchaguliwa na kundi dogo tu watu katika chama na sasa wamepewa mikoa yenye majimbo 6 hadi 7 je huyu atakuwa na uwezo wakuongoza kwel?
 
Awe mwanachama wa sisiemu na mtu wa kujipendekeza kwa mag.amba

Mfano mzuri ni Risasi Mwaulanga anytime atakula ukuu wa wilaya
 
Hivi karibuni serikali itatoa majina ya wakuu wa mikoa kufuatia hii ya wakuu wa wilaya iliyotoka leo. Mmekuwa mashahidi kwamba wakuu wa wilayo wengi wameteuliwa kutimiza lengo la fadhila na kupeana ulaji-siyo kazi vivyo hivyo tunawategemea wakuu wa mikoa watakuwa. Napendekeza vyeo hivi kuwa na interview toka utumishi kulenga uwajibikaji na hili nafasi pekee ni kulisema ktk katiba mpya...ikishindikana bora tufute rasmi ktk katiba yetu. Nchi yetu maskini inatupasa kuwa na vyeo vyenye tija. Wanasheria mnaweza kunisaidia kuliweka vizuri hili niweze kulifikisha kwa tume ya katiba
 
Nimekuwa nikiwaza juu ya uteuzi wa wakuu wa wilaya, mikoa, ambapo kwa kiasi kikubwa CCM imewafanya kuwa watendaji wake, japokuwa wanapaswa kuwa watendaji wa kiserikali. Ni wazi kwamba CHADEMA wakichukua madaraka watafanya mabadiliko makubwa katika uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa. Hivyo tunajiingiza katika tatizo na gharama zisizo na ulazima.

Kimsingi kazi ya watu hawa ni uhamasishaji tu wa mipango ya maendeleo.

Hili suala lazima liangaliwe kwa makini katika katiba mpya. Eidha wasiwepo kabisa au basi tuweke bayana kwamba uteuzi wao haupaswi kuwa na tabaka lolote la kisiasa, kitu ambacho ni vigumu kutekeleza.

Wakurugenzi wa mikoa, wilaya, wanatosha kabisa kuhamasisha na kusimamia maendeleo katika wilaya na mikoa, lakini hata kwao pia tuwe makini wasiteuliwe kisiasa!
 
Ndugu wana JF kila mara najiuliza hivi ni nini kazi za mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya katika kumletea mwananchi maendeleo. Nimefuatilia sana lakini sioni umuhimu wa hawa wateule wa rais zaidi ya kuwa wapambe na vikwazo vya maendeleo. Kama kuna mwenye kujua anjuze kazi za hawa mabwana tafadhali naomba anisaidie maana nimefuatilia nimeshindwa.

Mara nyingi nimekuwa najiuliza kuhusu kazi za wakuu wa mikoa na wilaya na umuhimu wa wao (kiuchumi, kimaendeleo, n.k) lakini nashindwa kupata jibu juu ya uwepo wa hivi vyeo vya kikoloni.

Nimejaribu kujisomea vitabu mbalimbali vya siasa na uraia lakini sijakutana na topic ambayo inazungumzia kazi na majukumu ya wakuu wa wilaya na mikoa; mbali na kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba wao ni wakuu wa ulinzi na usalama kwenye wilaya zao na mikoa yao. Hiki nadhani ni cheo bandia cha kisiasa walichopachikwa ili waonekana kwamba kuna kazi wanafanya. Ikiwa hawa watawala wamekasimiwa kuwa wakuu wa ulinzi na usalama kwenye maeneo yao ODC na RPC wao wanafanya kazi gani?

Kazi za wakuu wa wilaya na mikoa ninazozijua ni hizi hapa:
1. Kupokea na kukimbiza mwenge;
2. Kuwapokea viongozi wa kitaifa wanaotembelea kwenye maeneo yao ya utawala;
3. Kualikwa kama wageni rasimi kwenye sherehe na makongamano mbalimbali; na
4. Kuwakandamiza watu wote wanaoenda kinyume na maagizo ya wakubwa.

Haya majukumu ni ya kipuuzi kabisa. Kazi hizi (ambazo ni useless and unproductive ijapokuwa zinakula pesa nyingi za umma) zinaweza kufanywa na mkurugenzi au mbunge bila kuleta athari yoyote katika utendaji wao. Kuendelea na vyeo hivi vya kikoloni ni kuwakomoa wananchi wanaogharamia mishahara na maisha ya wakuu wa mikoa na wilaya. Kila siku serikali inalia haiona fedha kumbe inazo fedha za kuchezea kwa kuwalipa watu ambao hawana kazi.

Kama kuna mtu ambaye alisoma elimu ya siasa, atuelimishe kuhusu kazi za hawa jamaa na umuhimu wa kazi zao katika kukua kwa uchumi na pato la taifa.

Tazama video hii hapa inayothibitisha kwamba vyeo hivi vimeishapitwa na wakati:

Skia hii kitu kutoka kwa Jenerali Ulimwengu na mchakato wa katiba 2011 - YouTube

yield.gif
 
Back
Top Bottom