Kweli Sukari haina expiry date?

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
Katika hali ya kawaida Sukari iliyo hifadhiwa vizuri haina e expiary date bali best before date.

Wataalam wa vyakula wamekubaliana Sukari iliyo hifadhiwa vizuri inaweza kudumu kipindi kirefu(indefinitely kwa lugha ya kingereza).

Mtanzania yeyote aliyekuwa na ushahidi wa kisayansi kuharibika Sukari iliyo hifadhiwa vizuri ajitokeza.

Miaka yote hii sijashuhudia sio nyumbani Wala kwa majirani Sukari imemwagwa eti imeharibika.
 
Ukweli ni kuwa sukari inaweza kukaa kwa miaka mingi bila kuharibika, nmefuatilia kwa kirefu mjadala wa sukari Tangu mheshimiwa Rais alipotoa tamko LA kusitisha utoaji vibali vya vya sukari na ofisi yake ita shughulikia swala hilo, baada ya muda si mrefu sukari ikaanza kuadikmika na kupandia bei,
Likatolewa tamko kuwa bei ya sukari kwa TANZANIA nzima ni Sh 1800, tamko hilo halikusaidia hali hiyo badala yake, bei ya sukari ikapaa na ikawa haikamatiki, baada ya muda ikatolewa taarifa ya serikali bungeni kupitia kwa waziri mkuu kuwa serikali imegiza sukari kukabiliana na tatizo LA uhaba wa sukari,

Katika sakata hilo mheshimiwa Rais katika moja ya mikutano aliwatuhumu waagizaji wa sukari kuwa walikuwa wanafanya mchezo hatari kununua sukari ambayo ilikuwa imekaribia ku expire na kuleta nchini, kwa kufanya hivyo Watanzalia walikuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa kwa kula sukari ambayo ilikuwa ime expire au karibu inataka kumaliza muda wake,

Hapo ikabidi nifanye utafiti sehemu mbali mbali ili kujua kama kweli sukari inaweza ku expire au Inatakiwa kutumika muda gani kabla haijafaa kwa matumizi ya binadamu, ukweli ni kuwa sukari haiwezi kuharibika kama imetunzwa vizuri kwa kuepuka unyevu, maana ndani ya sukari hakuna kemikali inayoweza kuharibika,

Hata unyevu ukiwepo na sukari ikaonekana kama uji bado sukari haitakuwa imeharibika au haitafaa kwa matumizi , sukari kupata unyevu ni kwa sababu ni hygroscopic lakini haiitolei sifa ya kuwa ime expire, kuna wakati sukari ninaweza kukaa kwa muda mrefu ikawa mabonge( clumps) pia hii haina maana sukari imeharibika,

Ukweli ni kuwa Rais alishauriwa vibaya kuwa sukari inaweza kuharibika ikizingatiwa yeye ni mwanasayansi wa kemia
 
Acheni kumvua nguo mungu wa ccm, shauri yeni mimi simo, msije mkasema sikuwaambia mapema!
 
Back
Top Bottom