ELI COHEN
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 9,375
- 28,484
Matangazo yenye taswira za ngono au binti kujiweka kuvutia matamanio ya ngono lazima yaruke na akili za watu, kuweka attention hapo na hata kuishia kununua bidhaa ambayo imetangazwa.
Mara nyingine inatumika kama propaganda ya mamlaka ili kuwapunguzia scrutiny, ili kuwatoa watu katika jambo flani nyeti la taifa na kuwapatia skendo ya utupu utupu, unashangaa vijana wote wanaishia ku-discuss na kushare skendo na kupunguza umakini wa lile swala.
Mabinti wenye skendo za mjini mjini, makalio makubwa na walio taswira ya utupu utupu wanaishia kufanikiwa kifedha siku hizi, kwa maana SEX APPEAL YAO INAUZA, kama sio kupata mabwana mataita wataishia kuuza bidhaa za makamouni au kutumika kama propaganda kuzabaisha watu