mito mingi
Senior Member
- Dec 21, 2014
- 196
- 111
Nakumbuka wakati huo nakuja mjini daresalam kutafuta maisha wakati huo mwanamuziki anae wika alikua ni mumini mwinjuma na kibao chake cha mgumba.Niko kwenye basi kibao hicho kinapigwa mwishoni kwenye kibwagizo"mkulima ameuza jembe sasa kakimbilia mjini,amejipachika uganga kumbe ni tapeli tu".Nakumbuka mbali ndio nimetoka bush nakuja kwa blaza mwenyewe ana chumba na sebule mwananyamala amepanga,kwenye basi nawaza mengi nikifika dar itakuaje?Mungu si asumani sasa nina mke watoto wawili nyumba gari tatu na kila aina ya mahitaji ya daresalam.