Kweli ndoa ndoano

dagaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
290
Reaction score
382
Habari wapendwa,

mimi ni mdada wa miaka 29 nimeolewa nina mume na mtoto wa mwaka mmoja na miezi 7, tatizo kubwa sana, jumapili ya juzi mume wangu alinipiga na akanivuta nywere na kuniweka alama kwa titi langu la kushoto, ila chanzo kilikuwa ivi, mi nilikwenda bagamoyo kwa picnic ya ofc, niliporudi jioni, mimi na mume wangu tukaenda kuchukua maziwa harafu mume wangu akasema leo nina hamu ya kuku choma tukale dada asipike apike cha mtoto yeye tutambebea take away, tumekula vizuri wakati tunarudi akawa anakimbiza gari nikamwambia d usikimbize gari harafu nikapunguza sauti ya redio, akaanza unajua usiniletee dharau, nikamwambia kukwambia usikimbize ndo dharau kama vip nishushe uende mwenyewe, akaanza unajua we unijua, ****** wewe, ******** hunijui kabisa, uku amenivuta nywele na kunikaba shingo, mi kimia, nitakuuwa wewe uku anakimbiza gari kwa nguvu, nikamwambia mume wangu tatizo nini, kwani haya yote yametoka wapi, anasema usiniletee dharau zako, kweli hasira ilinikamata nikaanza kulia uku naona titi la kushoto damu inatoka ni kaanza kumjibu nikamwambia ugomvi umeununua wewe, na hapo sasa akapaki gari mbele ya nyumba na gari lina tinted, tuliwa ndani ya gali akaendelea kunishika kabali, akaniambia ukishuka kapaki vitu vyako nikupeleke masaki, masaki ndo kwa wazazi, mi nikamjibu hukunitoa usiku ulinitoa mchana so kukicha nitaenda mi namwangu na dada, kasema uende mwenyewe nikasema siendi, baada nikaingia ndani, nikaingia moja kwa moja chumbani nikaanza kulia tena sana na kwa machungu mimi mume wangu leo ananitukana matusi ya kila aina na kuninyanyapaa kama m2mwa kweli nililia sana tena sana na kwa machungu, baadae akaja akasema umeshafunga mizigo nikamnyamazia akasema unisikii akaninyanyua kichwa akanishika mikono kwa nguvu na kunitoa alama kiasi fulani inaumiza sana tena sana, wakatia anaongea na kuniumiza mi kimia, baadae akaja ujapaki bado nikamwambia kaa chini tuongee, akakaa, nikamuuliza kwani tatizo nini jamani make sielewi tatizo we kuwa na amani niambie, akasema unajua ujanipa haki yangu muda(tendo la ndoa) haya mambo yote ya una kiburi yote ni uongo main point ni hiyo, tatizo nini? mi kimia make nilikua na hasira, nikamwambia ni kweli na sikujibu sasa ivi coz nina hasira, akasema ok ijumaa basi, na akasema mi nakupenda sana sema tatizo ni hapo. upande wangu kuusu mashitaka ni kweli uwa nambania, chanzo kikubwa ni mtoto bado mdogo na kingine mume wangu aniandai powa ye akipiz mi nakuwa bado kabisa na si kwamba nina mtu wa kunikuna nje sina, na sasa tuko powa tunacheka ila mi bado rohoni kama nimeadhirika kimawazo kwasabu nikikumbuka unyama alionifanyanyia na matusi aliyonitusi wakati mwingine nalia mwenyewe na kunifanya sasa nami nianze kuweka akiba ya mimi kama mimi, make nyumba tunayoishi ni yetu tumejenga, ila nilivyokuwa nafukuzwa kama mbwa, na navyo sema sasa nimeshaanza kutafuta kiwanja cha bei rahisi ili nami niwe na aset yangu kama mimi, na ijumaa mi nitampeleka dinner then nilikua nafikilia nimueleze kila kitu kwamba tendo la ndoa ni haki yake ila na yeye nitamwambia mapungufu yake yote ya kutoniaandaa ipasavyo, hii nimeiandika umu najua watu wazima wana uzoefu wa ndoa kuzidi mimi na wanaushauri nimepeni mawazo yenu mazuri, make mimi kama mimi japo nampenda mum wangu lakini.....
 
Aisee usije ukajaribu kumwambia kwamba hakuandai vizuri hapo ndio utaharibu kabisaa bora ukiwa ktk majombozi ndio umwambie bado kwanza usiingize mshedede tuendelee na foreplay...
 
Duh Mi kimia.......?:confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:
 
Pole kwa kukabwa na kupigwa kidogo.

Hivi ulichezwa unyago?Ulifanyiwa kitchen party kabla hujaolewa?Ulijua wajibu wa mke ndani ya nyumba?

Mpaka una mtoto mdogo inaonekana kabisa umekaa na tatizo hilo na mumeo kwa muda mrefu bila kuchukua hatua thabiti za kulimaliza mpaka yeye kaona kuwa unambania haki yake ya ndoa ndio wewe unastuka!Unafikiri mwanaume kama unambania chakula cha usiku ambacho ni haki yake,unadhani atafikiria nini kama si kudhani una mtu ambaye anakusugua kiasi kwamba huna hamu nae.

Kwa kuwa umesema kuwa unataka kukaa nae na uzungumze nae basi isiwe nje ya nyumbani kwenu maana mambo ya chumbani hamuwezi kuyazungumza hotelini,jipange na jiandae kwa kuweka mazingira ya kuzungumza nae na hata baada ya kuzungumza nae mnaweza kula chakula cha usiku huku mkijaribu kufanya mabadiliko ambayo wewe unayataka.

Usiweke kinyongo kwa mumeo na elewa kuwa hasira zote alizokuwa nazo sababu yake keshakwambia hivyo kujitenga na kufanya mambo kimya kimya bila yeye kujua italeta mgogoro mwingine ambao utakuwa mkubwa zaidi ya huu.
 
Bado mnapendana, inawezekana hamuongei mara kwa mara kuhusu mahusiano yenu.
Ni vibaya kukupiga lakini pia namuona kama muelewa pia ndio maana akakubali kukusikiliza japo ana hasira.

Salini pia.........sioni tatizo kubwa sana mpaka sasa.
 
mmmh.....bado nipo nipo kwanza.......
 
pole sana bwana
na wewe kwa nini umnyime mwenzio k
mdatishe mumeo mama ohooooo!
bora hata amekuambia ukweli , wengine wanahama nyumbani kabisa unaachwa na k yako inadoda
 
dagaa toka lini akagoma kupikwa ili aliwe???? Ok, kwanza dada yangu unafanya makosa makubwa sana kumbania mumeo unyumba, nadhani hilo hata wewe umelishaligundua. Hebu lirekebishe kwanza hilo.

Kuhusu mtoto, wote tumepita huko lakini ni lazima utumie uzazi wa mpango ili kuepuka kupata mimba zisizotarajiwa. Kuhusu kumharibu mtoto, hilo nakataa kwa sababu kama umempa unyumba mumeo, baada ya kumaliza nenda kaoge. Hapo hata kama mtoto akitaka nyonyo unaweza kumnyonyesha bila ya shida yoyote na miaka nenda rudi hutasikia mtoto kaharibika. Cha msingi baada ya kutumia uzazi wa mpango ni usafi kwa mustakabali wa ndoa yako.

Tatu na mwisho, kuhusu mumeo kutokukuridhisha hilo ni suala linaloongeleka japokuwa unahitajika kuwa makini sana katika kumwambia ili asione unamdharau kuwa hajui majambozi. Mwambie kiustarabu, siyo kama unamnanga vile, kwa mfano kama anaenda round moja yupo hoi unamwambia mume wangu naomba leo unipe kama vitatu hivi, nimemiss mautundu yako.

Mkiwa katika mchezo unaweza kumwambia unajua mume wangu yaani mimi safari moja tena hizi za haraka haraka huwa unaniacha mume wangu, naomba basi uwe unaniandaa vya kutosha ili angalau tufike pamoja. Hapo ataelewa kuwa anahitaji kukuandaa ili mfike pamoja badala ya yeye kukutumia kama chombo cha kujistarehesha.
 
kwanza sijui una miaka mingapi au elimu kiasi gani ila uandishi wako mi KIMIA.
pili tatizo ni MAWASILIANO kati yako na mme wako,hivyo inaonekana kila mmoja wenu anabeba mzigo wa "kutoridhika " kwenye moyo wake na mwisho wake hutokea kama yaliyokupata wewe,,
kwa hiyo mimi nakushauri ukae na mme wako MUONGEE,na msiishie kuongea suala hilo tu pia fanyeni KUZUNGUMZA iwe sehemu ya mahusiano yenu,
 
Dagaa pole sana kwa yote yaliyokukuta. Kitu cha kwanza nataka nifahamu kwa nini akina mama mnakuwa wagomvi sana akina baba tunapoendesha magari, mimi kwa kweli nakuwa sina raha nikiwa na mamsap barabarani, nji nzima anaongea tu, mara kidogo umgonge mwenye bodaboda mara njia nzima kanuna hata sielewi ni nini. Dagaa kweli mwanaume kunyimwa unyumba roho inauma sana hata mimi hasira hunishika sana, wife na yeye ana mtoto mdogo hana mwaka lkn huwa simpigi, nambembeleza na kumsifia ht 2hrs mwishoni utasikia fanya fasta hapo anakuwa amefanya kosa kubwa ujuzi wote ntaufanya mpaka ataomba round nyingine lkn. Kwa akina mama wengine wanakosa hamu ya tendo la ndoa kabsaa. Chakufanya dagaa ukimtoa out usimwambie hayo mapungufu yake ila mkirudi home mpe game halafu wewe ndo uwe champion muelekeze unavyotaka wewe huku ukimsifia sifia na kumhakikishia kwamba unampenda sana
 
We dada wewe lazima uwe good storyteller....yaani mi kimia....nakosa maelezo

Kumbe wanaume mkikosa ile kitu amani inatoweka duuh wenzetu hawa wengine ni matatizo. Ndugu yangu uamuzi wako wa kutoa kimia ni kitu muhimu. Mueleze matatizo ajirekebishe au umsaidie unajua madhara yake baadae kuwa ndoa amani itatoweka kabisa. Mtu asikwambie kuwa issue hii izungumzwe kunako 6x6, utaharibu kila kitu.

Kuhusu kujiwekeza ni muhimu, mwanamke pesa yake isiishie kwenye mabotique au saloon. Save for the rainy days.
Ubarikiwe.
 
pole sana dada ynagu...ndoa ndoano.....

unajua sisi wanaume bwana huwa tunadhani mwanamke ni chombo cha kutumia kikiwa ndani..na cha ajabu sana huwa hautna muda wa kuwaandaa wenza wetu ili nao wafurahie tendo la ndoa...tukijisikia tu tunarukia juu wla humpi style nzuri nzuri...wewe ni kurukia juu tu unamaliza haja zako, ukijisikia unataka kuendelea na cha pili tena hivyo hivyo...hii huleta matatizo sana kwa familia zetu sometimes...

Dada yangu mimi naweza kukushauri tu usimnyime unyumba mumeo ila kabla ya kufanya chochote wewe anza kumpa romance halafu akitaka kukurukia mwambie "subiri kwanza D" then ongeza manjonjo mengine kama yale mlikuwa mnafanya kabla hamjaoana hadi usikie na wewe upo tayari....ndipo wewe mwenyewe chukua machine yake uingize maana atakuwa hoi kweli najua...mpe style za ukweli hadi siku ingine tena asitake kurukia rukia...
 
pole sana...ila kati ya vitu vinavyochangia ndoa nyingi kuvunjika ni tendo la ndoa hasa kipindi mwanamke akiwa katika uzazi kwa hiyo jitahidi sana kumpa mume wako tendo la ndoa sivyo ndoa yako ipo mashakani sana...

kwa wale wa kwetu sometime wanasema wee kula ukimaliza funika ili mradi tu mume aridhike ili kudumisha ndoa
 
Story ni nzuri ila nashiwishika kuona kama vile hiii ni hadithi ya kutunga, kwa sisi wenye ndoa kweli haiwezekani yaani ghafla tu kati kati ya maumivu na uchungu halafu msuluhishe ghafla;
Je ugomvi hasa hapa ni upi, moja, ni wewe kwenda Picnic bagamoyo maana mwanzoni nilidhani ndio msingi wa ujumbe, Pili, kumjibu kuwa apunguze spidi ya gari? maana hapo ndio ulianza kupigwa, tatu, je ni huko kumnyima haki yake ya ndoa?? Maana hapo mlipatana ( kwahio pale ambapo unadhani ndio ugomvi ungetokea naona ndio upendo umetokea) Kha!!!

hii story umehadithiwa na mtu na wewe ukakimbilia kuja hapa, ok ndoa haina formula Dada, all you need is to Pray Hard and work hard suala sio Masaki au Mbagala, suala ni how mnachukuliana nyie wawili. Have a blessed day
 
wakati anakukaba hakukuwa na wembe karibu umtie maumivu akili imkae sawa?

mumeo amekomaa kiakili?
 

Hili ni janga la taifa...
 
MAWASILIANO KATIKA NDOA.....Huwezi kuishi na mwenzio pasipo mawasiliano yanayoendelea.Hata kama hakuridhishi, why dont you just throw it on his face...Toa mwongozo wa nini kifanyike badala ya kumbania....
Wanaume wengi wanaweza kuvumilia pasipo kusema kero zao japo kwa kufanya hivi wanatengeneza "a timing bomb na matokeo yake ndiyo kama haya!!!
 
Dagaa acha upuuzi wako wako WA KUTAKA HAKI SAWA!!!!!!!!! Hizo redioni tu! GO WITH THE FLOW! Jishushe tu, mwambie nimekosa, nisamehe sweetie! LING'ONGE TU kwanza hadi hasira zako zipoe kwanza. Jifanye umesahau na wewe ndo mkosefu. ITS GOOD FOR THEIR BIG EGO! Halafu it will spare you the DRAMA ya kuanza vikao na wazazi na washauri. Come to think of it cleary mwenzio alikuwa na HASIRA zake na wivu kuwa huenda kwenye hilo PICNIC UMEMEGWA LIVE BILA KUNASA NA The Boss!!!!!! Au mtu tu alituma SMS kukuharibia tu aone itakuwaje umezidi HASHUO ofisini kwenu.
Yalishatokea, omba msamaha hata wa kinafiki yaishe upumue kidogo.

La kuchukua KIWANJA nalo nenoooooooo! We jibweteke tu, kile chumba ulichoacha kwenu kishapata mpangaji! Na sio kujenga kisiri tu, HATA KUWAENDELEZA KWENU ZAIDIII YA KWA MUMEO BIBI WEWE!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…