Kweli Mh.Makamba anafurahisha!

CCm tutawashitaki kwa kukiuka mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto uliokubaliwa mnamo mwaka 1989 na kusainiwa na kuridhiwa na Tanzania mnamo mwaka 1990 katika kipengele cha 1,33,34,36,39 vinaleza kwa uwazi umuhimu wa kumlinda mtoto kutokana na ukatili uonevu na unyanyasaji,kipengele cha 1 kinaeleza kabisa heshima ya mtoto leo hii watoto wanatundikwa kwenye mazoezi karibu wiki mbili zimepita wanashinda juani hakuna choo wapewi chakula wamekoseshwa masoma hawapumzishwi na pia hawana itikadi kwani hawajafikia umri wa miaka kumi na nane,mkataba unakatazwa kuwatumia watoto kwenye matangazo wanachofanya CCM na serikali yake wanachofanya ni kuwatumia watoto kutangaza CCM kinyume cha hata sheria y a mtoto ya Tanzania ya mwaka 2009.
Wazazi na walimu pi wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuridhia CCM kuwatumia watoto kwenye matangazo ya CCM kuwadhalilisha kwa kuwavika kofia kubwa kuliko vichwa vyao kwa maana hivyo kuwatesa sana na mifulana ambayo iko kama magauni
Makamba na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma lazima wafungwa kwa kuwahonga watoto kesho pilau na maji kama walikuwa wanawajali kwa nini walikuwa ha wawapi pilau watoto wakati wa mazoezi
hata kwenye ripoti ya watoto inayopelekwa na wanarakati itabidi iorodheshe kiwango cha ukatili kwa watoto na uvunjifu wa haki za watoto kwa kiwango cha juu na serikali ya Tanzania kupitia chama chake
kwa kifupi CCM hawajifunzi kabisa
 
Ningekuwa na uwezo ningeongeza neno MAKAMBA kwenye lugha yetu ya kiswahili liwe na maana ya POROJO, ROPOKA, PAYUKA, n.k.
 
Mi naona kama mzee yuko sawa, ameona wale vijana ni njaa tu ndo zimewapeleka pale na dawa ya njaa ni msosi. Mtu mwenye akili na shibe yake angerusha ngumi baada ya kuambiwa huo udhalimu
 
Huu ndiyo mwanzo mwisho wa ccm... Kwenda kwa watoto kuwapa pilau ni aibu..

Hapo unaweza kuona kuwa sasa mwelekeo hakuna ccm zamani walikuwa wanawachukua vijana.. Sasa vijana wameshawashtukia wanawakimbilia watoto.. Hii ni janga kubwa sana na aibu..

Tena nasikia kuwa hawa watoto ni washule na ni amri imetolewa shuleni kuwa watoto wote waje leo kwenye maadhimisho yao.

Watawapa pilau na juice za azam leo ila maisha yao yatakuwa magumu sana siku za mbele..
 
Sasa hivi asubuhi hii malori yanasomba watu kutoka vijijini kuleta uwanja wa jamhuri hapa Dodoma. CCM imekwisha, kilichobaki kinawaunganisha ni kwa sababu wameshika dola, nje ya dola hakuna CCM.
 
SISIEM imepata mkunaji, bonge la buludani ndani ya chama, hakuna kama Makamba. Hatuitaji MC. Sasa mnataka nini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom