Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 3,804
- 8,797
Uenda wenye mamlaka wameamua kuziba masikio. Ukweli hali ya maisha ni magumu sana. Nikiwa katika safari za jiji la CPM katika matumizi ya usafiri wa umma japo unamilikiwa na wapemba na wachaga. Nilikaa na mzee wa makamo kama 65 mpk 70 umri wake, mwenye dhamana ya kukusanya pesa akaanza kuitisha wito wake mimi nikatoa 500 yangu hakuna kudaiana baba yangu akatoa Ulimboka mwekundu wa msimbazi 10 konda akasema nitakuletea chenji yako. Basi ni haya makubwa Hicha sijui. Tunaunguruma kona za Goba kuisaka mbezi sijui zile kona zililala na akili ya konda. Mzee akadai rejesho lake la chenji konda aligoma katu. Naweza kusema ni mkosi mzee akaanza kulia kwa hasira pamoja na utetezi toka kwangu na kiti cha nyuma konda alikaza hasa kuwa mzee hana anachodai. Ndani ya basi kukatokea shuhuda kuwa haya mabasi makubwa wahudumu wake ni wezi sana hasa njia za Mbagala na Gongolamboto. Ila pamoja kugoma kwake tukaja kumshinda konda ikabidi amlipe mzee wa watu ila chozi kalitoa. Nikasema kweli maisha magumu zama zile mtu mzima kulilia ten ni nadra sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app