Kweli maisha magumu jamani...

nziriye

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
1,051
361
Nimegundua maisha magumu jamani wa-tz wenzangu ,yani kuna matendo yanatokea nchini kwetu hadi yanatia huruma,maisha magumu hadi inafikia kipindi watu wanafanya vitu out of their conscious,sikia kituko cha leo ktk daladala...nimepanda ktk daladala na m-baba mmoja ameforge kitambulisho cha shule ya sekondari anajadai anasoma biafra sasa konda akamuuliza biafra ipo wapi ,khe jamaa hajui ,?yani abiria wote wanashangaa,ndugu hivi mkwere angekuwa anajua wananchi wake wanatabu kama hizi au anajionea sawa?loh wengine wamegoma kulipa nauli mpya ,doh jamani tabu tupu yani ni bora kuwa mbwa ulaya nadhani kuna some of probs. zitapungua ,jamani hivi ni wa-tz wote wanatabu au ?
 
Hahah hahha hii kali duh,

Mr ,usicheke ndugu yangu ,hali inatisha ,we mbaba mzima halioni hata aibu ,mie ningependa siku moja mkwere akakae mbagala then apande daladala toka huko hadi ikulu then jioni arudi tena mbagala from there atagundua maisha ni magumu jamani ,lol.
 
ukitaka kuona vituko duniani panda gari la Mbagala kuna kila aina ya visa I miss those days
 
duh,inachekesha na inahuzunisha.pato la siku akilipigia mahesabu halitoshelezi bora afanye cost-cut kwa kuforge ID.
 
ukitaka kuona vituko duniani panda gari la Mbagala kuna kila aina ya visa I miss those days

hongera ndugu kwa kutoka huko ktk adha ya usafiri,anyways its better to pray for those who are there at mbags,hali nguumu ,kikwete mgumu yani ful mivurugano jamani.
 
Na bado, itakula kwetu for the next 5 years. Hakuna mikakati madhubuti ya kuweka hali sawa. Ni majibu ya kiuoga oga tu. Hata kama umechaguliwa na wananchi kama maisha mabovu basi utafute tundu lakutokea kama Mubarak et al.
 
Nyamazeni!! Si mlikuwa mnamshangilia aliposhinda??? Vuneni sasa mlichopanda., kelbu!!
 
ukiona maisha magumu ujue nchi inaendelea

ofcz wenye nchi ndio wanaoendelea
 
Pale stand ya Bagomoya (karibu na nyumbani kwa mkwere) utamkuta mama mmoja kiukweli amechoka na maisha huku akiwa na mtoto wake mgongoni na mwingine kimsingi alipaswa kuwa ameanza shule lakini ndiyo hivyo tena, utamkuta huyu mama amaomba "SAIDIA NDUGU ZANGU UKIJALIWA KUWA NA MIA UKIJALIWA KUWA HAMSINI MAISHA MAGUMU" kweli inasikisha sana na ndiyo hali ilivyo kwa walio wengi
 
Na bado, nilishangaa watu wanasema, Rais Wetu makini!!! Makini eh!!! bado watu wataanza kutembea kwa miguu Bagamoyo-Posta
 
hii ccm inatupeleka pabaya, mpaka miaka minne iishe cjui hali itakuwaje, jaman mwaka 2015 mabadiliko ya dhat lazima
 
Vituko gani mzee? tushushie mauzoefu wako mzee hiyo ya mbagala...

Mimi nilishawahi kupanda 'dcm' la mbagala kuna mama mmoja wa makamo nilikaa naye siti moja.
Sasa wakati wa kudaiwa nauli yule mama akajifanya mwehu yaani kama chizi kabsaa.
hatimaye konda akamsamehe.
Nilishuka naye kituo kimoja ndipo nilipogundua kuwa yule mama ni mzima wa afya.
Nilihuzunika sana.
 
Nauli ya mbagala ni 500 hivyo kwa siku ni buku bado kula...wakati mshahara ni elfu 60 kwa wadosi,haibaki chenji hapo kama hamna kitu mukichwa
 
Back
Top Bottom