Kweli Magufuli atataifisha mashamba ya Mwinyi, Mkapa, Mangula na Sumaye au hapa Uongo Tu?

Mgufuli hana "blank cheque" ya kufanya chochote anachotaka au kuahidi ndani ya CCM. Anayo Ty ruhusa ya kutamka mengi kwenye kampeni kama "kuibadilisha CCM" ikiwa ni mkakati wa ushindi. Ndiyo siasa hiyo. Kazi kwa watakaoamini au kutoamimi.
 
Hebu ngoja tuchukue mfano mmoja ambao uko dhahiri! UDA iliuzwa kwa njia za ufisadi mkubwa kwa bwana mmoja wa Shinyanga. Na huyu bwana wa Shinyanga inajulikana wazi ni rafiki na msiri mkubwa wa Ridhiwani Kikwete (na wengine wamekwenda mbali na kusema UDA inamilikiwa na hawa wawili! Je Magufuli akipata urais ana ubavu wa kuchokonoa chochote kuhusu ufisadi wa UDA? Atamchokonoa mtoto wa mtu aliyemtupia urais kwenye bakuli?
 
Mimi nasubiri mahakama ya mafisadi nione Mwakyembe anafikishwa mahakamani
kwa mabehewa hewa na ufisadi wa bandarini.....hapo ntamuona Magufuli kweli 'mchapakazi'

Na yeye mwenyewe.. Kivuko, billion 86 na nyumbani za serikali
 
JokaKuu

Ni maneno ya siasa za kampeni. Hata aliyepo aliyasema hayo mwaka 2005 na huko huko alikosemea Magufuli! Sijui kwa niji wananchi hawana kumbukumbu hii.
 
Last edited by a moderator:
ni rahisi zaidi kutaifisha nyumba alizouza yeye mwenyewe kuliko mashamba asiyojua asili yake
 
Ardhi yote ya Tanzania chanzo chake ni Raisi.!

yah na nyumba zimejengwa kwenye ardhi kwahiyo ningefurahi arudishe na zile alizouza kwa mazabe

Magufuli jembe ninaamini kabisa atafanya hivyo
 
Hapo sasa! Hapo sasa! Ni kuwa ccm ni mtandao uliojengwa na mafisadi na hao mafisadi hawawezi kudhuriana! Kama akishinda KAZI inaanza pale atakapokuwa anaunda serikali yake. Mr X ni fisadi lakini alimsaidia sana kwenye kampeni, atamwacha? Kampuni Y ni ya serikali na ilinunuliwa kifisadi na mtoto wa rais aliyempigia debe, atathubutu kumnyang'anya?

Hatathubutu hata kidogo. Kwa kusema hivyo ina maana hakutakuwa na mabadiliko yoyote. Badiliko litakuwa jina la Rais tu basi
 
Hapana usiseme uongp, hajasema atataifisha na pia hajasema atachukuwa mashamba yote.

Magufulia anasema mashamba makubwa yasiyoendelezwa atayarudisha kwa wananchi walime.

Hivi kwanini mnapenda kusema uongo?

Hao uliowataja kama wana mashamba makubwa na yamekaa hawayaendelezi amma waanze kuyaendeleza amma watapewa wananchi. Hawapo exceptional.
Hata mimi nimesoma hili andiko nikashangaa kwa sababu mtu anayepotosha ninaamini anaelewa kile ambacho Magufuli amekuwa akisema kwenye mikutano mbali mbali.

Kuna baadhi ya watu wanatafuta kila aina ya uchafu ili kujaribu kuzuia sauti ya Magufuli isisikike na kama ikisikika wafanye kila jitihada ili isielewe.
 
Ahaa. Unaona sasa mtego alioutega? Kumbe ameweka condition na wala sio wenye mashamba makubwa utabidi yagawiwe kwa wananchi? Unajua maana yake ni nini? Ni kwamba akiupata 'urahisi' tukimuulizw vipi mzee yale mashamba ni aje? jibu ni rahisi tu

Atasema wenyewe wanayaendeleza, basi. Utataka nini zaidi? Ni sawa na wezi wa Epa tulipoambiwa walirudisha pesa lakini haijulikani ni nani na ngapi zilirudi!


Hakuna mtego hapo mbona sheria ipo siku nyingi hiyo?

Lowassa ana ardhi haifanyii lolote kuikaguwa inabidi uwe na helicopter, kumbuka hilo.

Mengi ana ardhi kubwa kuliko eneo la Dar.

Sumaye mpaka leo ana hodhi ardhi na ana ugomvi na wanakijiji wanaomzunguka, kulima halimi kaiweka tu.

Wakae chonjo.
 
Unaposema "Wakati Halima Mdee akilipigania suala hili kwa kipindi 2010-2015 chote cha bunge lililopita, Dr. Magufuli alikuwa kimya. Hakuwahi kulizungumzia kwa namna yeyote ile."

Napenda nikuulize wewe mleta mada ulitaka Magufuli azungumze nini katika hilo? Ninachojua mimi, Magufuli amekuwa waziri wa ardhi na makazi tangu 2006-2008. Kwahiyo kuanzia 2010-2015 waziri wa ardhi na makazi alikuwa nani, au kuna tofauti gani kati ya waziri wa ujenzi na waziri wa ardhi na makazi?
 
dk magufuli ni mlaghai kama ilivyo kawaida ya wanaccm?
Anaweza kuwa si mlaghai kama Lowassa. Mkurya sijui yule atapenda kazi kama anavyosema. yule kama asemavyo hajui sana siasa na ndo watu wengi wa Tanzania wamesikika wakisema. porojo TZ hazitakiwi ili tuondoke japo hatua chache. Kikwete alimzuia mengi sana ili angalau asikanyage wakubwa. Mpeni sasa Magufuli acheni ushabiki na upenzi kama walivyofanya wakina mama kwa Mjomba JK! achaneni na huyo swahiba wa Mjomba JK. kwanini muungane na vita binafsi ya hao maswahiba
 
Mimi nasubiri mahakama ya mafisadi nione Mwakyembe anafikishwa mahakamani
kwa mabehewa hewa na ufisadi wa bandarini.....hapo ntamuona Magufuli kweli 'mchapakazi'

Hata usijisumbue kumsubiri.Lilimshinda ghorofa la Tanesco ataweza nini? Na kilichozuia ghorofa ya Tanesco ni Jengo la Ubungo Plaza.Ukivunja Tanesco na Ubungo Plaza inabidi literemke.Sasa hapo ndo alipoprove kuwa huwa anakurupuka
 
Back
Top Bottom