Arusha kama miji yote duniani inaendeshwa kwa sheria. Kwa hali ilivyo sasa, kila mtu anaweza kujiamulia kufanya biashara popote pale anapotaka hata katikati ya barabara bila kuchukuliwa hatua yeyote ile. Hali hii imeachwa kwa muda mrefu kwa sababu ya weakness ya watumishi wa halmashauri na hasa madiwani waliekuweko kwa miaka 15 iliyopita. Madiwani wangeweza kabisa kuwa question ma town inspectors au Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji kwa nini hali hii inaachiwa mpaka sasa imekuwa issue kubwa, eti mpaka wamachinga watafutiwe mahala pengine kwanza as if walikuwa wakifanya biashara zao legally in the first place. Wamachinga na hasa wauzamitumba wana sehemu yao kule Crocon waende huko, wauza nyanya, mboga na matunda waende soko la mianzini, kijenge kuna nafasi tele huko. Hakuna cha nani kasema hivi au vile, ni LAZIMA waondoke Arusha iwe kama Mwanza. Mwanza wamachinga walijaribu kupambana na dola kwa siku mbili tu wakakiona cha moto, sasa hivi Jiji la Mwanza ni mfano wa kuigwa kwa usafi Tanzania nzima. Shida ilioko Arusha ni viongozi wamekuwa waoga mno kufanya maamuzi. Mkuu wa Mkoa anaonekana ni jasiri lakini kwa hili la kukithiri kwa uchafu Arusha naona linamshinda. Ukimchnganya na Meya wa Arusha alivyokuwa incompetent, mdhaifu na mwoga hali hii naona itaendelea mpaka tumpate Paul Kagame wa Rwanda aje na bakora lake hapa ndipo wamchinga, wachafuzi wote wa mazingira, mkurugenzi, meya, wataalam wa halmashauri na hata hao akina Lema na wenzake watajua kuna utawala wa sheria.