Nnauye: Mbowe wataje watakaohamia chadema; Lema awasilisha rufaa ya kurasa 985 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nnauye: Mbowe wataje watakaohamia chadema; Lema awasilisha rufaa ya kurasa 985

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, May 7, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimemtaka Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataja hadharani wabunge 70 kutoka na mawaziri saba wa CCM, ambao wameomba kujiunga na chama hicho cha upinzani ili kuuthibitishia umma kama alichochokisema kina ukweli.

  Juzi, akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC, Unga Ltd jijini Arusha, Mbowe alisema idadi hiyo ya wabunge na mawaziri wanatarajia kujiunga Chadema siku za usoni na kutangaza chama hicho tayari kimevuna wanachama 10,400 kwa mkoa wa Arusha na Manyara.

  Wanachama hao ni kutoka Ngorongoro (2,500), Monduli (2,000), Longido (800), Arumeru (1,200) Arusha mjini (2,600) na Simanjiro (1,300).

  Jana, akizungumza na Mwananchi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kama Mbowe ana uhakika na anachokisema ni bora angesubiri kitokee halafu ndiyo azungumze vinginevyo awataje wanachama hao ili umma umuamini."Anachokizungumza hakina msingi na hoja zake hazina mashiko.

  Anachokizungumza angekaa nacho kwanza ili kitokee na hivi sasa wananchi wa Arusha wana matatizo hawahitaji kujua na nani anatoka wapi na kwenda wapi," alisema Nape.Alisema chama makini hakiwezi kujitangaza kuwa kinachukua wanachama wa chama kingine, bali ni kutafuta wanachama wapya kwani Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40.

  "Ninamshauri Mbowe aache kukurupuka na aache uongo, awataje hao anaowazungumzia na akiendelea na tabia ya aina hii itamshushia heshima,"alisema Nape na kuongeza;"Siasa za aina hii amuachie Dk Slaa kwani Mbowe yeye ni mwenyekiti wa chama na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni anaheshimika.


  "Nape alisema ni muhimu Mbowe akaacha kukurupuka kwa kutoa hoja bila mpangilio kwani heshima aliyonayo itashuka akiendelea na hali hiyo.Juzi mbowe alitumia mkutano huo kuwatoa hofu wana Chadema wanaotilia shaka wimbi la viongozi na wana CCM wanaojiengua na kujiunga na chama hicho kikuucha upinzani kuwa Chadema iko imara na hakiwezi kuhujumiwa wala kupenyezewa mamluki kama baadhi wanavyodhani.

  Mbowe alitamba kuwa ameongoza harakati za upinzani kwa zaidi ya miaka 20 sasa, ambayo imeanza kuzaa matunda kwa Watanzania kukiamini Chadema hivyo hawezi kukubali kuruhusu mtu yeyote yule anayetumia njia ya wazi au ya kificho kukidhoofisha.

  Nassari, Heche matataniKatika hatua nyingine, jeshi la polisi mkoani Arusha linawasaka kwa mahojiano mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), JohnHeche kuhusiana na kauli walizotoa kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Unga LtD.

  Habari zilizopatikana kutoka ndani ya jeshi la polisi na baadaye kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa zimeeleza kuwa kwenye orodha hiyo ya viongozi wanaosakwa pia yumo aliyekuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Bananga aliyehamia Chadema hivi karibuni.

  Akizungumza kwa njia ya simu jana, Kamanda Mpwapwa alisema viongozi hao walitoa maneno yanayoelekea kuwa ya uchochezi ambayo hayawezi kuachwa bila wahusika kuhojiwa kujua walichomaanisha.

  "Kwani wewe hukuwepo pale uwanja jana (juzi) wakati viongozi wa Chadema walipokuwa wakihutubia? Walitoa maneno ambayo lazima tuwahoji kujiridhisha walichomaanisha na hili ni jukumu la kawaida la kiuchunguzi la polisi," alisema Kamanda MpwapwaKaimu Kamanda huyo ambaye amaeteuliwa kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara katika uteuzi na mabadiliko yaliyofanywa juzi na Inspekta Jenerali wa polisi nchini (IGP), Said Mwema alisema hatua zaidi dhidi ya viongozi na mwanachama huyo mpya wa Chadema itajulikana baada ya kuhojiwa.

  "Siwezi kukanusha wala kuthibitisha iwapo tutawafungulia mashtaka kwa kauli hizo tunazozichunguza, uamuzi utategemeana na maelezo yao na taarifa za uchunguzi tunazoendelea kukusanya," alisema Mpwapwa.

  Katika mkutano huo wa hadhara, viongozi kadhaa wa Chadema walioongozwa na Mbowe walihutubia na kutoa kauli mbalimbali huku Nassari akitumia fursa hiyo kuzungumzia utendaji wake ndani ya bunge mara alipoapishwa baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Aprili Mosi, mwaka huu.

  Mbunge huyo kijana aliueleza umati mkubwa uliohudhuria mkutano huo uliolenga kuzindua oparesheni ‘Vua gamba, vaa gwanda' kuwa jeshi la polisi linapaswa kuongeza juhudi katika upelelezi na uchunguzi wa mauaji wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, Kata ya USA-River, Msafiri Mbwambo aliyechinjwa kwa nyuma na kitu chenye ncha kali.

  Nassari alisema uvumilivu wa wana Chadema kuendelea kusubiri kwa muda mrefu uchunguzi wa mauaji hayo ya kinyama unakaribia kufikia kikomo kwa sababu wauaji walitumia simu kumwita marehemu hivyo, ni rahisi kwa vyombo vya dola kufuatilia namba hiyo na kutambua wahusika kirahisi.

  Pengine kauli inayowezekana kumponza hadi kuitwa kwa mahojiano polisi ni madai yake kuwa iwapo vyombo vya dola na serikali vitaendeleza ukandamizaji dhidi ya wanaopigania haki, usawa na ustawi wa jamii kama inavyoshuhudiwa sehemu mbalimbali nchini, basi watatangaza Arusha kuwa eneo linalojitegemea yeye akiwa Rais na aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema akiwa Waziri Mkuu.

  Hata hivyo, Mbowe alifuta kauli hiyo aliposimama kuhutubia akisema Chadema inahitaji kuunganisha na kukomboa nchi yote bila kuacha kipande chochote akisema kauli ya Nassari ilitokana na hamasa ya kisiasa jukwaani.

  Kwa upande wake, Bananga yeye alitumia fursa hiyo kuwaomba radhi wana Chadema wote aliowakwaza kwa vitendo vyake alipokuwa CCM na papo hapo akamshukuru Rais Jakaya Kikwete na mtoto wake, Ridhwani kwa kile alichodai kukamsirisha na kumpa mwanya wa kufikiri sawa sawa na kujiunga Chadema alichogundua ndicho chama chenye dhamira ya kweli ya kukomboa taifa.

  Heche yeye aliueleza umati huo kuwa ataanza oparesheni hiyo katika mikoa ya Kusini kwa lengo la kukisambaratisha CCM na kukiimarisha Chadema huku akisema, Rais Kikwete ameonyesha dharau kubwa kwa umma unaolalamikia maisha magumu na kupanda kwa gharama za maisha kwa kuzidisha ukubwa wa baraza la mawaziri kwa kuteua mawaziri watano zaidi ya waliokuwepo awali.

  Katika hatua nyingine, maelfu ya wakazi wa Karatu, jana walijitokeza kumpokea Mbunge mteule wa viti maalum wa Wilaya ya Karatu, Cecilia Pareso.Pia katika mkutano huo, Chadema walitoa tamko la kuitaka Serikali kuwafikisha mahakamani mawaziri wote waliondolewa kutokana na ubadhirifu la sivyo chama hicho, kitaandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima.

  Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema alisema haiwezekani mawaziri wabainike wamesababisha upotevu wa fedha za zaidi ya Sh9 trilioni, wakaondolewa uwaziri tu huku mamia ya watu ambao wametuhumiwa kwa wizi wa simu wanaozea magereza. "Tunasema hivi, hawa mawaziri wote waliobainika kusababisha hasara kwa taifa lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na kuvuliwa ubunge," alisema Lema.

  Alisema Sh9 trilioni zinatosha kutengeneza barabara za lami katika mikoa yote nchini, au kujenga nyumba za walimu wote wa shule za sekondari na msingi.

  LEMA AWASILISHA RUFAA YA KURASA 985 WAKILI

  Method Kimomogoro amekamilisha na kuwasilisha mahakamani rufaa ya kupinga hukumu iliyomvua ubunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema huku akiainisha hoja 18 za kupinga kukata rufaa.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu za kimahakama zilizopatika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, rufaa hiyo iliwasilishwa Ijumaa ya Mei 4, mwaka huu tayari kwa ajili ya kuwasilishwa kwa msajili wa Mahakama ya rufaa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajiliwa.

  Akizungumza ofisini kwake jana, Wakili Kimomogoro alithibitisha kukamilisha na kuwasilisha rufaa hiyo mahakamani tayari kwa ajili ya kupangiwa jopo la majaji wa kuisikiliza.Pamoja na hoja za rufaa, kitabu hicho cha rufaa chenye kurasa 985 ina mwenendo mzima wa shauri, vielelezo na viambatanisho vyote vilivyowasilishwa Mahakama Kuu.

  "Kimsingi ni rai yangu kuwa mtukufu Jaji Rwakibarila (Gabriel) hakutolea uamuzi mambo na hoja za msingi zinazofanya hukumu yake kukosa hadhi kisheria, kuitwa hukumu, hayo ni miongoni mwa hoja za msingi nilizoanisha kwenye rufaa niyowasilisha mahakamani juzi," alisema Wakili Kimomogoro.Kwa mujibu wa hati ya rufaa hiyo, hoja ya kwanza hadi nne zinapinga uamuzi wa Jaji Aloyce Mjulizi aliyesikiliza shauri hilo katika hatua za awali kwa kutupa pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa utetezi kwenye kesi ya madai namba 13 iliyofunguliwa na wapiga kura watatu waliopinga ushindi wa Lema.

  Miongoni mwahoja hizo ni kuwa wadai, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo kwa sababu hakuna haki yao iliyovunjwa kisheria kama wapiga kura.Wakili Kimomogoro aliyemwakilisha Lema na mawakili wa Serikali, Timon Vitalis na Juma Masanja walidai aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian ndiye alikuwa na haki kisheriakulalamikia ushindi na maneno ya kashfa yanayodaiwa kutolewa dhidiyake na Lema.

  Hoja ya tano hadi 18 zinapinga hukumu ya Jaji Rwakibarila ambapo katika suala la hukumu yake kukosa hadhi kisheria, wakili Kimomogoro anadai hakutolea maamuzi athari za wadai kushindwa kuwasilisha mahakamani CD zinazomwonyesha Lema akitoa maneno ya kashfa na udhalilishaji walizodai kuwa nazo katika hati yao ya madai.

  Kimomogoro anadai Jaji alikosea kwa kutotumia hata kesi moja kama rejea kati ya kesi kadhaa zilizotajwa na mawakili wa pande zote mbili za wadai na wadaiwa.

  Jaji Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga pia anadaiwa kukosea kisheria kwa kukubali na kuegemea ushahidi wa mdomo pekee katika hukumu yake bila kuwepo ushahidi wa mazingira, Video wala maandishi kuunga mkono ushahidi wa mdomo.

  Mrufani pia anadai Jaji alikosea kwa kutumia viwango na vigezo tofauti kwa mashahidi wa upande wa wadai na utetezi kwa kukataa ushahidi wa Leman na mashahidi wake kwa madai kuwa walikuwa na maslahi kwa sababu ni wanachama na viongozi wa Chadema lakini akakubali ushahidi wa wanachama na viongozi wa CCM kutengua matokeo.

  Hoja nyingine ni kuwa hata kama Lema angetiwa hatiani kwa madai yaliwasilishwa mahakamani, bado Jaji hakustahili kutumia kifungu cha 114 cha sheria za uchaguzi kuripoti uamuzi wake kwa Mkurugenzi wa uchaguzi kwani makosa hayo hayahusiani na vitendo vya rushwa wala jinai ambavyo humzua aliyehukumiwa kupiga kura wala kugombea uongozikwa miaka mitano.


  KWA HISANI YA GAZETI LA MWANANCHI
   
 2. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kikwete wataje wauza madawa za kulevya....
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mwache aendelee kusubiri list yeye anasubiri nini kujivua gamba na kuvaa gwanda?
   
 4. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Yaani huyo Nape! Kwani yeye yupo CDM? nadhani labda angekuwa CDM angekuwa na mandate ingalau kidogo ya kumuhoji mbowe not otherwise! Yeye ana mamlaka gani ya kumuamuru Mbowe awataje? Hiyo ni dili kati ya chairman Mb0we na hao wahamaji, yeye hayamuhusu!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,519
  Trophy Points: 280
  vuvuzela
   
 6. k

  kombo mkuya Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we Nnauye umeshaishiwa na sera so ni bora ukaka kimya ili ulinde heshima yako,mbona una kiherehere sana au na wewe ni mmoja wapo unayetaka kuhamia CHADEMA?huna jipya NAPEEEEE...
   
 7. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Mbona kuna tetesi kuwa hata yeye yupo amebuku nafasi CDM?...
   
 8. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Swali kwa Nape: Je wewe ukiwa na Mh. sana Sita na Mwakyembe mlimtaarifu mtangulizi wako Chiligati kuwa mnaanzisha CCJ?
   
 9. k

  kombo mkuya Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vaa gwanda nape.mbona una hofu sana bwana mkubwa au na wewe ni mmoja wapo unaogopa kutajwa?chama kimekufa hicho.soma alama za nyakati mbona wenzako wameanza we unaogopa nini nape?
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kaka pongezi kwa zile 5 za jana
   
 11. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  ni huyu nape mwenye kipaji cha unafiki haaaaa yuleyule aliecheka ccm iliposhindwa arumeru, yuleyule aliegombania demu na rostam hahaha HONGERA
   
 12. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Yeye huyo dogo Nape atulize boli asiwasemee wanachama wengine, kama kuhama ni uamuzi wao binafsi, yeye akitaka kuhama kwani sharti adhibitishe kwa mtu cha maana asubiri tu kama hilo litatokea. kama hao wanachama wanaotaka kuhama wengine wanadaiwa na chama hilo suala lingine ambalo inabidi ashirikiane na chama hicho watakachohahamia ili aweze kulipwa madai ya chama;

  WALIZOEA WAO KUHADAA WANACHAMA HEWA KWA KUANUNULIA KADI KISHA KUDAI WAMERUDISHA NA KUHAMIA CCM. CHADEMA WANAOHAMA SI WANACHAMA WA KAWAIDA NI MAKADA, MADIWANI, WAKUU WA WILAYA BAADAE WABUNGE. NAPE SUBIRI UONE GHARIKA.
   
 13. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Nape anza na mwenyekiti wako kikwete, mbowe wamrukia wa nini? Hukumbuki kuwa kikwete ana orodha ya wezi wakubwa wa nchi hii, wakwepa kodi wakubwa wa nchi hii, wauza unga madawa ya kulevya wakubwa wa nchi hii? N.k n.k? Je, umewahi mhimiza hata siku moja awataje? Acha unafiki TOA KWANZA BORITI KWENYE JICHO LAKO!
   
 14. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Hivi huyu Nape wa CCM na yule nape wa CCJ ni ndugu? mimi nawachanganyaga sana maana majina yao yamefanana sana hata sura nashindwaga kuwatofautisha!
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nape aseme tu hajui nini kinaendelea kwenye chama chake maana wako busy kunyukana. Na sasa subirini bomu la Comoro!
   
 16. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Tangu lini vuvuzela Nape ana authority ya kumchagulia ama kumshauri Mbowe cha kuongea.Huyu Nape ana matatizo ya akili.Akija hapa mtaona atavokuja na taarab zake.
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  NAPE sumaye aliwahi kukamata kiwanda madawa ya kulevya kunduchi.jee umeuliza judgement yake imetoka?wahusika wapo wapi?
   
 18. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Chama kinamfia Nape so sad
   
 19. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mbowe sio mjinga hawezi kutaja hao wabunge na mawaziri...anaijua ccm fika..hao wabunge na mawaziri wanaotaka kuhama ccm wakitajwa tu hadharani ujue wameisha...either watapotea...watawekewa sumu, watapata ajali hawatamaliza 2012..

  hao polisi wanawahoji cdm kwa sababu ya maneno waliyoyasema kwenye mkutano wao...hellooo!!! polisi walikua wapi wakati wa uchaguzi arumeru...mkapa, lusinde na wengineo waliotoa lugha chafu...i dont recall mkapa kua kituo cha polisi anahojiwa...huu uonevu sijui utaisha lini haki ya Mungu!! :confused3:
   
 20. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Nepi bwana, kilaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaza.
   
Loading...