kweli kuna wabunge waajabu!

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,051
653
Jioni hii nimesikitika kumuona mbunge bungeni anasema maendeleo ni pamoja na jengo la bunge, hapa ni sawa na Jk aliposema kuwa na magari mengi ni maendeleo hakika Tanzania ina watu wapuuzi sana sikuwepo Tanzania ila NIMEJIONEA MENGI SANA NA YA KUSIKITISHA MAISHA MAGUMU LAKINI VIONGOZI WANALETA UTANI. ninaposikia Bunge na kujionea maisha ya WATANZANIA NAUMIA SANA.
Tuliowapa uongozi ebu fikirieni basi maisha yetu.
 
Kuna mwingine mwana mama yeye anaunga mkono kununuliwa pikipiki- ambulace za kuwabeba mama wajawazito ambao wana matatizo ya kujifungua. Najaribu kufikiri mama mwenye matatizo ya kujifungua akiwa kwenye pikipiki na shindwa kupata picha. Kiongozi anaye ahidi hizi bajaji na pikipiki za kiambulace jaribu kuangalia gharama ya gari analolitumia utachanganyikiwa, hivi vipaumbele vya viongozi wetu ni nini hasa?. Huyu mbunge kilaza kapelekwa nani pale bungeni.
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 
22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.
Uwezo Tunao, mbona hii posti yako unaipeleka kila thread?! is it something personal?.
 
Hawawezi fikiria maisha yetu kwa sababu wameingia hapo kwa pesa zao. Tulinunuliwa wali na nguo tukawapigia so its payment time. Inasikitisha basi tu.
 
Kwani hukuiona ile "spin' aliyofanya Msigwa kuchukua mwanafunzi mmoja aliyepata daraja la kwanza ku-justifie kufeli kwa zaidi ya asilimia 50? Just in case you didn't know, ni Tanzania pekee ambapo unaweza kuropoka chochote kile mchana kweupeeee and get away with it. Karibu bongo mkuu. Kwetu sisi IGNORANCE twaaita AMANI!:twitch:
 
Mnafiki hajifichi leo hii katika kikao cha jioni naibu spika katoa tangazo linalowataka wabunge wa ccm na cuf kutoka zenj wakutane.
Zitto kawaumbua kwa kumjulisha naibu kuna wabunge wa chadema zenj mbona hawajahusishwa dhana ya umoja iliyokuwa ikisemwa jana imeishia wapi ?
 
Kuna mwingine mwana mama yeye anaunga mkono kununuliwa pikipiki- ambulace za kuwabeba mama wajawazito ambao wana matatizo ya kujifungua. Najaribu kufikiri mama mwenye matatizo ya kujifungua akiwa kwenye pikipiki na shindwa kupata picha. Kiongozi anaye ahidi hizi bajaji na pikipiki za kiambulace jaribu kuangalia gharama ya gari analolitumia utachanganyikiwa, hivi vipaumbele vya viongozi wetu ni nini hasa?. Huyu mbunge kilaza kapelekwa nani pale bungeni.
ni kwel nimemsikia yule mbunge ngumbalu yani kama kipofu ameongea upupu mwanzo mwisho ,wabunge viti maalum ccm wanatuangusha coz wengi ni kuunga mkono hoja asilimia mia zote hata kama ni ujinga..na ndio washangiliaj mjengon kwa hoja za kipuuz..namsifu zitto kwenye mchango wake kaongea ki2 cha msing sana addressn wabunge vijana wapiganie nchi yao na waache ushabik kweny maslah ya taifa..alieniharibia siku ni yule mbaba bonge tena na suti amevaa anaisifia serikali ya ccm kwa maendeleo eti nw tuna bunge jipya n wabunge wanapiga makofi..who need bunge jipya..we need maendeleo yanayoonekana na kufanya wananch wapige hatua.
 
Kuangalia kipindi cha bunge ni kama ze komedi, hasa wale akina mama wa viti maalum!
 
Jioni hii nimesikitika kumuona mbunge bungeni anasema maendeleo ni pamoja na jengo la bunge, hapa ni sawa na Jk aliposema kuwa na magari mengi ni maendeleo hakika Tanzania ina watu wapuuzi sana sikuwepo Tanzania ila NIMEJIONEA MENGI SANA NA YA KUSIKITISHA MAISHA MAGUMU LAKINI VIONGOZI WANALETA UTANI. ninaposikia Bunge na kujionea maisha ya WATANZANIA NAUMIA SANA.
Tuliowapa uongozi ebu fikirieni basi maisha yetu.

.....ndio shida ya kupeleka bungeni vilaza!!!!
 
kweli mkuu yani wabunge wa viti maalum ni janga.....very vilaza yani ndio shida c**pi ikikupeleka mjengoni...yani sm of michango yao ni balaa na kichefuchefu kuisikia na ndio wanaorudisha nyuma ...coz lazma wawatetee waliowapa viti vya bure..
Kuangalia kipindi cha bunge ni kama ze komedi, hasa wale akina mama wa viti maalum!
 
ndugu mtanzania mwenzangu nikweli usemayo,hakuna ndoa mbili kwa mwanamke mmoja,hawa CUF wamesha funga ndoa na CCM sasa hawana tena nguvu ya upinzania sasa ndoa na CHADEMA wanaing'ang'ania yanini??.na huo muafaka wa ZANZIBAR kwani chama pinzani ni CUF tu mbona hawa kuwataka kushirikisha vyama vingine CUF wanauchu na madaraka ndio maana wameingia kwenye muafaka bila kushirikisha wenzao sasa wanataka tena kuingia kwenye kambi ya upinza lengo nikudhoofisha tu upinzani.
 
Jengo la bunge nalo ni maendeleo au ni moja ya miradi iliyotufilisi? hatujiulizi ndani ya miaka hamsini tumekuwa na majengo ya bunge matatu (kabla ya kuhamia Dodoma tulikuwa na karimjee hall, Dodoma jengo la zamani na sasa jengo jipya. yaani tunafanya kazi ya kujenga majengo ya bunge kana kwamba hakuna shughuli zingine za maendeleo. majengo yoyote ya umma yanapojengwa lazima yajengwe katika viwango ambavyo matumizi yake yatakwenda zaindi ya karne moja
 
Kuna mwingine mwana mama yeye anaunga mkono kununuliwa pikipiki- ambulace za kuwabeba mama wajawazito ambao wana matatizo ya kujifungua. Najaribu kufikiri mama mwenye matatizo ya kujifungua akiwa kwenye pikipiki na shindwa kupata picha. Kiongozi anaye ahidi hizi bajaji na pikipiki za kiambulace jaribu kuangalia gharama ya gari analolitumia utachanganyikiwa, hivi vipaumbele vya viongozi wetu ni nini hasa?. Huyu mbunge kilaza kapelekwa nani pale bungeni.

Nilishangazwa na kauli hii alipoitoa JK kwenye kampeni yake kama ahadi. Nilijiuliza kama kweli hawa viongozi wanaelewa hela za nchi hii ni za nani, na ni nani ana haki ya kuzifaidi?

Iweje mnunue V8 (Mil 180) kwa ajili ya viongozi serikali kwenda kazini kila siku na muone mgonjwa anastaili ambulance ya Pikipiki (5 mil)?

Niliposikia Waziri anatangaza kuwa hizo ambulance ziko njiani niliishiwa na nguvu, hata hao wabunge ndio wale wale kwa sababu nilitegemea wao ndiyo waulize iweje wagonjwa wapelekewe Pikipiki na viongozi (wazima wa afya) watembelee V8?

Ambulance ni haki yetu ya msingi kama watanzania na si halali kuziona kama favour kutoka kwa mkuu wa kaya. Na ambulance si hizo BAJAJ kwasababu hata kitanda hakiwezi kuenea!

Kuangalia kipindi cha bunge ni kama ze komedi, hasa wale akina mama wa viti maalum!

hapo ndugu umenena! wengi wa viti maalum ni wauza sura tu. wameingia bungeni na bashasha lakini hata mchango mmoja hawajatoa. kazi yao mashindano ya mavazi na vikukuuuu! jamani changieni hoja basi tuwasikie! msitege watu, mtakwisha!
 
hawa jamaa sijui kama wanafikiria hawana hata uchungu kweli Pikipiki leo iwe ya kubebea wagonjwa? Shule kibao kuna mmoja anasema kuwa kufeli kwa form 4 hata hivyo inasaidia kwani wale waliofeli si sawa na Darasa la saba.....pumbavu sana watu wasiokuwa na uchungu na maendeleo.
 
Back
Top Bottom