Kweli hii au ni usanii tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli hii au ni usanii tu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 5, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Maana huyu mama naye jina lake limo katika waliochukua shilingi bilioni 133 za EPA.

  Mke wa Ballali arejea

  na Mwandishi Wetu
  TAnzania Daima~Sauti ya Watu

  HATIMAYE mke wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Dk. Daudi Ballali, Anna Muganda, alirejea nchini juzi akitokea Marekani akiwa na siri nzito alizoachiwa na mumewe kabla hajafariki dunia Mei 16, mwaka huu.

  Habari za uhakika zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili zinaeleza kuwa Anna aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, majira ya jioni akiwa ameambatana na watoto wake wawili, waliotajwa kwa jina moja moja la Octavio na Raquel.

  Mmoja wa watu walio karibu na familia ya marehemu Dk. Ballali, alieleza kuwa Anna atawasilisha mambo kadhaa mazito aliyoachiwa na mumewe kwa wakili wa familia yao, Nakazaeli Tenga.

  Aidha, mjane huyo, ataongoza vikao vya familia vitakavyozungumzia utata uliojitokeza kuhusu mirathi ya marehemu Dk. Ballali. Vikao hivyo pia vitahudhuriwa na mwanasheria wa familia, ambaye atakuwa na kazi ya kufafanua baadhi ya mambo ya kisheria.

  Habari za ndani zaidi ambazo gazeti hili limezipata, zinaeleza kuwa Anna pamoja na watoto wake watatoa msimamo wa nani mrithi halali wa mali za marehemu Dk. Ballali.

  “Ndugu, mke wa marehemu Dk. Ballali na watoto wake wamekuja kuweka wazi juu ya masuala yao kupitia mahakama na ukweli kuhusu mirathi hiyo iko kwao na si kwingineko,” kilisema chanzo chetu hicho kilicho karibu na familia hiyo.

  Kurejea nchini kwa mama huyo pamoja na watoto kunaelezwa kuwa kumetokana na utata ulioibuka hivi karibuni baina ya ndugu wa karibu wa marehemu Dk. Ballali na baadhi ya waliokuwa washirika wake kibiashara.

  Baadhi ya ndugu waliotajwa kujiingiza katika mzozo wa kugombea mali za marehemu Dk. Ballali, ni mdogo wake, Natalis Ballali na dada yake, Elizaberth Ballali.

  Mali zilizoibua mzozo ni pamoja na gari lenye namba za usajili T466 ANB aina ya Scania pamoja na tela lake lenye namba T 759 ANV pamoja na gari jingine aina ya Scania lenye namba za usajili T487 ANB na tela namba T774 ANV. Magari hayo yanafanya kazi ya kusafirisha mizigo mikubwa kutoka Tanzania kwenda Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kusini.

  Mali nyingine zinazopiganiwa na wanandugu hao ni mashamba moja likiwa na ekari saba lililo eneo la Mbweni, Bagomoyo, la Mabwe Pande lililoko wilaya ya Kinondonii lenye ukubwa wa ekari 7.76, la Mpinga ekari 10, lililoko Bagamoyo pamoja na mengine mawili yaliyo wilayani Bagamoyo ambayo ni Kerege 1 lenye ukubwa wa ekari tano, kerege 2 (17.72) na kerege 3 (2.33).

  Pia katika mlolongo huo yapo matrekta mawili, moja likiwa na namba za usajili T657AKA na jingine T460 AJE. Mali hizo zote ziko chini ya usimamizi wa kampuni ya Mainline Cargo inayomilikiwa na mwekezaji kutoka nchini Afrika ya Kusini, Marty Dom.

  Katika madai yao juu ya mirathi hiyo, mdogo wake Dk. Ballal, Natalis anadai kuwa ndiye aliyeachiwa wosia na marehemu kaka yake kusimamia mali zote.

  Katika barua aliyoandika Juni 30 mwaka huu kwenda katika kampuni ya Mainline Cargo iliyopo jijini Dar es Salaam, aliitaka kampuni hiyo kuacha kujishighulisha na usimamizi wa mali za marehemu Dk. Ballali kwa madai ya himaya ya kampuni ya Trans Ruaha Corporation LTD ambayo yeye alijitambulisha kuwa ni mwenyekiti wake.

  Natalisi, katika barua hiyo aliwalaumu ndugu zake kuwa si waaminifu na wapenda fedha bila ya kufanya kazi na wana wivu, hivyo kumtaka mkurugenzi wa kampuni ya Mainline Cargo aendelee kumuamini na kusisitiza kuwa yeye ndiye msimamizi halali wa kampuni hiyo.

  Anaeleza kutomtambua dada yake kuwa si mrithi wa kampuni hiyo kama alivyo jitambulisha kwa mkurugenzi huyo.

  Hata hivyo, katika barua ya Elizabeth iliyopewa jina la wosia uliotolewa na Dk. Ballali kabla ya kufa, kwenda kwa mkurugenzi huyo na meneja kampuni ya Trans Ruaha, Onesimo Kiwanga, alimtaka mkurugenzi huyo kukubali kuwa yeye ndiye mrithi wa mali hizo.

  Barua hiyo inamnukuu Dk. Ballali akieleza kuwa hayupo katika hali nzuri lakini amekuwa akiongea na Elizabeth mara kwa mara anapopata nafasi ili aandike kila kitu kama alivyotamka kwa maneno yake mwenyewe.

  “Nataka Elizabeth asimamie shughuli za Trans Ruaha pamoja nanyi nyote, nataka afungue akaunti mpya kwa jina la Trans Ruaha. Atafungua akaunti mpya, nataka ifanyike hivyo kwa sababu, fedha za Trans Ruaha zitasaidia kulipia gharama zote zinazonikabili hasa hapa Marekani.

  “Nilijaribu kukupigia hata wewe Marty Dom, lakini kwa bahati mbaya nahisi hukuniamini. Baada ya kuugua kwa miezi sita iliyopita hali ilikuwa ngumu hata kwa dada yangu Elizabeth, nahisi hata yeye hamkumuamini. Nilisikitika sana baada ya kuona mmeshindwa hata kumuamini dada yangu, mlihisi kama si mtu wa kuaminiwa.

  “Basi naomba muamini katika hili la akaunti mpya, ili aweze kulipia ankara zote, inabidi asafiri kuja Marekani baada ya kukamilisha jambo hilo. Baadhi ya ankara ninazodaiwa huku Marekani zinafikia kiasi cha dola 18,000 hadi 20,000, hivyo Elizabeth atashughulikia na kusimamia mambo yote muhimu, maana anazo taarifa zote zinazotakiwa,” inasema sehemu ya barua hiyo ikikariri maneno ya Dk. Ballali.

  Hata hivyo madai yote ambayo yalitolewa na ndugu hawa wawili yamepingwa vikali na watoto wa Dk. Ballali, kwa madai kuwa bado wanaitambua kampuni ya Mainline Cargo kwa kushirikiana na kampuni ya Trans Ruaha kuwa ndiyo inayostahili kusimamia mali hizo hadi hapo hatua za kisheria zitakapo halalisha mirathi hiyo kutoka na wosia wa marehemu.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Huyo mama na huyo Wakili Tenga maisha yao yako hatarini. Kama kweli wana ushahidi mzito basi wausambaze haraka sana katika vyombo vya habari vinavyoaminika Tanzania.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  wao wanazungumzia mali kiduchu alizoaacha balali, yaani vigari vichache, wanatuzuga hawa, tunataka watuonyeshe yaliko yale mabilioni ya epa, na wale walioshirikiana na marehemu ndugu yao
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Jamani wana JF, kama watanzania wa kawaida tuna desturi ya kuheshimu marehemu, maadam mkewe karudi na wosia rasmi, hayo sasa ni mambo ya kisheria na bado yako kwenye ngazi ya kifamilia. Nawaombeni mwacheni marehemu Daudi Balali apumzike kwa amani.

  kama katika huo usia rasmi, marehemu ba amefanya confession yoyote kuhusiana na EPA, hiyo ni issue nyingine nzito tena tete kisheria kuhusiana na ushahidi wa kauli za mtu aliyeshakufa.

  By the way, up to now, hakuna kesi yoyote ya EPA iliyofunguliwa mahakamani, maana yeke issue ya EPA bado ni hadithi tuu. Ndio maana hata Tume ya EPA haikuona umuhimu wowote wa kumuhoji marehemu Balali hivyo ina maana pamoja na jina lake kuchafuliwa sana, he died a clean man. Please let his soul rest in eternal peace-Amen
   
Loading...