Kweli duniani hatupendani

Kweli duniani hatupendani

kamsongole

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
111
Reaction score
15
Kweli duniani hatupendani, juzi kati nimekaa na mtu wa nyanda za juu kusini tukapanga kuanzisha biashara ya kupika chakula kwenye sherehe mbalimbali.

Tukaweka mikakati kemkem na mipango mizuri, tukadhamiria kuanza kazi mara moja. Basi tukaanza kupanga nani tumshirikishe akawa anawataja watu wa kulekule.

Mimi bila hiana nikakubali, kumbe ndo najikaanga. Mara ndugu yule akaenda kuwataarifu wale ndugu juu ya mpango wetu. Nikashangaa mwenzao napigwa chini ghafla.

Mara yule hatufai tusimuweke wakati mimi ndiye nimeweka mpango mzima. Na jana tu nimetoka kuwakabidhi pesa ya chakula cha arusi ya jumapili kama katibu wa kamati hiyo.

Hivi ungekuwa wewe ungefanyaje? Kweli dunia hadaa.
 
Ndio binadamu hao ..if you didn't know now you know...
 
pole sana Kiongozi
naomba mkalishe Chini na umkumbushe kuhusu mipango yenu!
 
Ndo hivo ndugu yangu yaani hata hamu ya kuendelea na hiyo biashara sina maana ni shida kweli.
 
Hahaha...dah mi mwenyewe yamenikuta haya. Nimempa mtu aidia ili tuifanye pamoja...kaenda kumwambia rafiki yake ndo wameamua kufanya pamoja mi nimemwagwa lol
 
usijali mkuu njoo tufanye na mm ila tutakuwa tunafanyia gest
 
tafuta mtu mwingine, kama vipi fanya peke yako.
 
kweli duniani hatupendani, juzi kati nimekaa na mtu wa nyanda za juu kusini tukapanga kuanzisha biashara ya kupika chakula kwenye sherehe mbalimbali. Tukaweka mikakati kemkem na mipango mizuri, tukadhamiria kuanza kazi mara moja. Basi tukaanza kupanga nani tumshirikishe akawa anawataja watu wa kulekule, mimi bila hiana nikakubali, kumbe ndo najikaanga. Mara ndugu yule akaenda kuwataarifu wale ndugu juu ya mpango wetu. Nikashangaa mwenzao napigwa chini ghafla. Mara yule hatufai tusimuweke wakati mimi ndiye nimeweka mpango mzima. Na jana tu nimetoka kuwakabidhi pesa ya chakula cha arusi ya jumapili kama katibu wa kamati hiyo. Hivi ungekuwa wewe ungefanyaje? Kweli dunia hadaa.

Labda ukose mtaji wa kufanya peke yako. Biashara za kufanya na marafiki / ndugu mwisho wake mara nyingi sio mzuri. Jipange mwenyewe lakini uwe na wafanyakazi wako ambao wapo wengi tu mitaani. Unaweza hata kurubuni wale wenye uzoefu kwa watu wengine ukawalipa vizuri zaidi.
 
Hili nalo wazo, ngoja nijipange. Ila inaumiza at first.
 
Hahaha...dah mi mwenyewe yamenikuta haya. Nimempa mtu aidia ili tuifanye pamoja...kaenda kumwambia rafiki yake ndo wameamua kufanya pamoja mi nimemwagwa lol

Yaani wanaboa, alafu wanaongea kilugha wewe huelewi, kumbe ndo unapigwa chini. But all in all GOD is good.
 
Partnership kwenye biashara ndo matatizo makubwa sana, hata kama unamuanmini sana kuwa mwangalifu
 
kweli duniani hatupendani, juzi kati nimekaa na mtu wa nyanda za juu kusini tukapanga kuanzisha biashara ya kupika chakula kwenye sherehe mbalimbali. Tukaweka mikakati kemkem na mipango mizuri, tukadhamiria kuanza kazi mara moja. Basi tukaanza kupanga nani tumshirikishe akawa anawataja watu wa kulekule, mimi bila hiana nikakubali, kumbe ndo najikaanga. Mara ndugu yule akaenda kuwataarifu wale ndugu juu ya mpango wetu. Nikashangaa mwenzao napigwa chini ghafla. Mara yule hatufai tusimuweke wakati mimi ndiye nimeweka mpango mzima. Na jana tu nimetoka kuwakabidhi pesa ya chakula cha arusi ya jumapili kama katibu wa kamati hiyo. Hivi ungekuwa wewe ungefanyaje? Kweli dunia hadaa.

thats painfull... pole sana.
kama mtaji wako ni mzuri fanya mwenyewe
 
kumbe wewe ndo mshika mchuzi? sasa tatizo liko wapi?

Tumia ubongo sasa ushafika mjini...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom