Kwa upande wangu kwenye boxing huwa nampa nafasi aliyemzidi mwenzie urefu hata kama hawajazidiana sana kwa sababu mrefu inakuwa rahisi kupiga sehemu zenye point na kujikinga yule mfupi asizifikie na mara nyingi ina kuwa hivyo mfupi inabidi afanye kazi ya ziada ya kutupa ngumi nyingi ili amchoshe ndio aweze piga sehemu za point vinginevyo labda jamaa awe hajui mbinu. huo ni uelewa wangu mimi. ndio maana sijashangaa jamaa kushinda
Boxing sio sawa na Segere au Kigodoro wewe pimbi eti mwenye kukata viuno vingi ndio mshindi. Na pia Boxing sio sawa na Mchakato wa kugombea kuteuliwa kupitia Magamba eti mwenye hela za kuhonga ndio mshindi.
Mpaka sasa hivi najiuliza na sipati jibu inakuwaje mywether kapigwa round zote kumi na mbili lakn atawazwe kuwa mshind na man pacquio aliyeweza kumudu na kumkimbiza mywether round zote kushindwa mpaka sasa sijajua vigezo na sababu ya kutokea hvyo.
Hapo kijana wa kifilipino kaonewa, ni mpango mzima wa kuja kuaanda mechii ya marudiano mwezi wa September 2015. Mpango mzima ni kama tume za uchaguzi za nchi za kiafrika zinavyowabeba viongozi walioko madarakani. Kumbuka story ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya Mhe Kivaitu???
Watu wengi humu wanalaumu kwa msukumo wa hisia zao na chuki zao dhidi ya bondia fulani...hawajui BOXING ni kitu gani??..hawajui hook ni kitu gani ?? Hawajui point zinahesabiwa vipi na kwa kigezo kipi.....hawajui kwanini PACMAN anatumia sana jab....hawajui kuwa defence skills ni moja ya nguzo muhimu kwa bondia.....hawajui kuwa si kila konde analorusha bondia basi huesadiwa point.....kwa kifupi hawajui lolote kuhusu BOXING...Chuki zimetawala vifua vyao mpaka wamepoteza uwezo wao wa kuchanganua mambo.....najua kinachowauma wengi ni show off za Mayweather na mabulungutu ya fedha..huku wao wakiwa hawana mbele wala nyuma......ninachotaka kuwakumbusha ni kuwa HARD WORK PAY.....