ulimi waupanga
JF-Expert Member
- Aug 31, 2014
- 470
- 1,162
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda sasa, Wanasayansi wanadai Jua ni moja kati ya nyota zinazoipatia mwangaza na nishati Dunia. Wanaendelea kudai Jua limesimama wima na Dunia iko kwenye mwendo ikilizunguka jua, kudhibitisha ilo wamekuwa wakitoa nadharia mbalimbali kama vile mtu akiwa kwenye gari jinsi anavyoona miti inatembea wakati gari alilomo ndo linatembea. Kwa kusoma kitabu cha Enoch anadai alionesha na malaika wa mungu kuhusu siri za uumbaji wa ulimwengu yakwamba Jua linaizunguka Dunia na mwezi pia unaizunguka Dunia na pia mwezi na Jua vinalingana ukubwa sema mwanga wa Jua ni x7 ya mwanga wa mwezi. Nimekuwa na maswali machache juu nadharia ya wanasansi wetu kuwa Dunia inazunguka Jua:
I) Kama ni kweli kwa nini nyota za Usiku tusione zinatembea kama lilivyo Jua? Maana Dunia inazunguka muda wote.
ii) Kwa nini mwezi husionekane umesimama ili kuapprove point ya mtu alopanda gari lililo kwenye mwendo maana wanadai na mwezi nao unaizunguka Dunia ina maana vyote viko kwenye mwendo. Mfano fanya jaribio ukiwa kwenye basi chungulia nje wakati mna overtake basi jingine utaliona kama limesimama lakini kiukweli liko kwenye mwendo.
iii) Kwa vile tuko kwenye uso wa Dunia na hatujafunikwa na chochote dhidi ya upepo( yaani hewa iliyo kwenye mwendo) kwa nini tusihisi effect ya kukatiza kwenye upepo wakati tukizunguka na Dunia kama inavyotekea ukipanda gari lililowazi?
Mwenye ufafanuzi wa haya tafadhali tusaidiane maana nikitafakari sana naona Enoch yuko sahihi.