Kweli CCM Tunachukiwa!

Kweli CCM Tunachukiwa!

akikuambia nchi itayumba na ccm tunazika Leo leo

Na haya ndo yanayosababisha akina kikwete wahangaike kutafuta watu wa kulinda maslahi yao mapana ikiwemo mgao wao pale stanbic
 
Hawachukii chama wanachukia watu waliokiteka nyara chama kinachoogoza serikali.Kuwa na kadi ya chama haitoshi bila kutimiza kanuni na ahadi za chama.Watu huko nyuma waliokuwa safi nao sasa wameenda na mkumbo wa rushwa na wizi,ufisadi,uongo n.k Kwa lugha sahihi CCM ISIYO YA MWL NYERERE INAVUNA KILE ILICHOPANDA.Hawana ushawishi wa hoja kwa wananchi,wana tumia misuli ghiriba,rushwa,kama mbinu rasmi.
 
Pumzika salama C.C.M, tulikupenda sana, lakn Rushwa na ufisadi viliwapenda zaidi, mlikuja kwa KIJANI na mnarudi kwa MANJANO, NYUNDO tutatumia kugongelea JENEZA lako na JEMBE tutatumia kufukia KABURI lako! MUNGU ibariki CHADEMA MUNGU ibariki Tanzania, C.C.M PUMZIKA KWA AMANI, PEOPLES POWER LOWASSA POWER,

haka kagonjwa kalimuua jirani kamehamia huku kwetu mi kama mlinzi wa huu mwili naanza kupata kazi kubwa ya kupambana na hawa virus aina ya fisad na rushwa
 
jana mimi nimemnyima fundi kazi kisa alikua anaitetea sana ccm nikaona bora aende zake nikamchukua mwengine asiyetetea utawala dhalimu!
well done.Kumpa Kazi mtu asiyejipenda yeye mwenyewe anawezaje kupenda Kazi aliyopewa and so kuifanya kwa ufanisi?
 
well done.Kumpa Kazi mtu asiyejipenda yeye mwenyewe anawezaje kupenda Kazi aliyopewa and so kuifanya kwa ufanisi?

Kuipenda ccm ni kulidumbukiza taifa ktk mikono isiyosalama....yalitaka kupitisha katiba mbovu....yamefisadi nchi na sheria zikapindishwa..jk anadiriki kusema escrow si pesa ya umma..wapuuzi kwa kulindana...nchi haiwezi kuongozwa hivyo
 
Juzi nilikuwa narudi home Bunju B, kumbe suruali niliyokuwa nimevaa ilikuwa na kipeperushi cha mgombea mmoja hivi jimbo la Kawe, nilikuwa nasoma wasifu wake na kutunza japo sikupiga kura sababu sina kadi, wakati natoa hela ili nimlipe konda, kikadondoka, kuna mzee mmoja alikuwa amekaa, mimi nimesimama akakiona, alipokiokota akasema kwa sauti ''we ni mzee kuzidi mimi?'' nikamjibu hapana, akaniuliza mbona unashabikia mambo ya kizee wakati nakuona wewe ni kijana, nikamuuliza kwanini akanijibu unashabikia CCM wakati vijana wenzio wanataka mabadiliko au wewe ni mfaidikaji wa CCM, basi daladala zima likawa linanishambulia mpaka nikaamua kushuka Kwa wagogo nikasubiri gari lingine, looh!!! aisee hatupendwi balaa
 
Ukifanya uchunguzi mdogo sana utakuta. Chadema inapendwa na wachagga ,wapare kidogo na wamasai wamehamia baada ya jamaa kukatwa.ukichunguza tena kidogo utagunduwa kuwa chadema inapendwa kaskazini na kwenye miji mikubwa kwa kiasi kidogo Kama mwanza,dar ,mbeya nk. Mkuu Tanzania ni zaidi ya hizo sehemu nilizokutajia.wala usitishike tena nimesahau kwa mf.kaskazini kwa sasa wambulu wamechukizwa sana na kiongozi wao Dr.Slaa kunyanyaswa wamerudi ccm wote.kwahiyo wala usiwe na shaka hizi kelele za hapa jf wala zisikuumize kichwa wapiga Kura wametulia wanasubiri mtanange.

Ebu twambie pemba kuna mbunge wa ccm au diwani
 
Kwanzia juzi sinywi tena castle lite ina chupa kama rangi ya magamba!!!Nahamia kwenye mbuyu
 
Tatizo ccm imewazalau wapenzi wake nao wametafuta chama kingine wewe Baki uendelee kuwa kapi kama makapi mengine
 
kama kweli mnataka kukiokoa chama mpeni nape likizo bao la mkono limekwaza wengi
 
Pamoja na mapungufu yake mimi nadhani ccm bado ni bora mara elfu ya UTATA no no! UKAWA. Beware of lowasa.
 
Nimeshuhudia majuzi nikisafiri kutoka Moro kwenda Arusha ambapo katika Bus la abiria 60 palikuwa na mjadala mkali sana na wachangiaji wakiongea kwa hisia kali.

Kati ya abiria takriban 25 waliokuwa wakichangia/kujadiliana ni watu wawili tu walioonyesha kuipenda CCM. Waliobaki walikuwa wankiponda chama chetu vibaya sana. Nilijaribu kufurukuta kwa kueleza mazuri ya CCM lakini nilizomewa hadi nikajinyamazia.

Najiuliza ni nini CCM imewakosea Watanzania hata kuchukiwa ghafla hivi?! Inafikia hatua mtu unaona aibu kujitambulishia CCM. Kijana mmoja (abiria) alisema mtu akimfananishia CCM atamshitaki kwa kosa la kumkashifu (yaani akimhusisha na CCM).

Wanachama wenzangu nasi tuamke tukitee chama chetu.

Katika mjadala wenu hamkukumbuka japo lami safi toka mlikoazia hadi kumalizia safari ambayo ni sehemu ya zaidi ya KM 17,000 tulizojengewa awamu hii? Hamkuona shule nyingi njiani? Chakula mlichokula njiani kwenye hoteli nzuri hamkusifia kuwa ni sehemu tu ukilinganisha na akiba kubwa ya chakula kilichopo kwenye maghala ya serikali?
 
Chama kirudishe dira ya kisasa, maadili na mshikamano.
 
Katika mjadala wenu hamkukumbuka japo lami safi toka mlikoazia hadi kumalizia safari ambayo ni sehemu ya zaidi ya KM 17,000 tulizojengewa awamu hii? Hamkuona shule nyingi njiani? Chakula mlichokula njiani kwenye hoteli nzuri hamkusifia kuwa ni sehemu tu ukilinganisha na akiba kubwa ya chakula kilichopo kwenye maghala ya serikali?

Acha kudanganya watu, lami imechakachuliwa utadhani hatuna wataalam kwa sababu wanaambiwa warudishe 10%, Shule hakuna huduma ni shule kama unabisha nitajie mtoto mmoja tu wa kigogo anae soma shule mokawapo ya shule hizo za kata. hazifai ndio maana hawawezi kupeleka watoto wao hapo! Chakula kipi unasema hujui no cha walala hoi hadi sasa hawajalipwa au haukuona wanaandamana mtwara! acha porojo kama unategemea kuwapa kura mungu atusaidie kadi yako ipotee. tukutane trh 25 October naamini utakuwa umebadilika!!!
 
Siipendi ccm toka moyoni..
 
Attachments

  • 1439215366161.jpg
    1439215366161.jpg
    7.4 KB · Views: 415
Back
Top Bottom