Nimeshuhudia majuzi nikisafiri kutoka Moro kwenda Arusha ambapo katika Bus la abiria 60 palikuwa na mjadala mkali sana na wachangiaji wakiongea kwa hisia kali.
Kati ya abiria takriban 25 waliokuwa wakichangia/kujadiliana ni watu wawili tu walioonyesha kuipenda CCM. Waliobaki walikuwa wankiponda chama chetu vibaya sana. Nilijaribu kufurukuta kwa kueleza mazuri ya CCM lakini nilizomewa hadi nikajinyamazia.
Najiuliza ni nini CCM imewakosea Watanzania hata kuchukiwa ghafla hivi?! Inafikia hatua mtu unaona aibu kujitambulishia CCM. Kijana mmoja (abiria) alisema mtu akimfananishia CCM atamshitaki kwa kosa la kumkashifu (yaani akimhusisha na CCM).
Wanachama wenzangu nasi tuamke tukitee chama chetu.
.
-Chini ya CCM wanafunzi wanakaa chini
-Chini ya CCM huduma ya Maji ni shida
-Chini ya CCM rushwa na ufisadi umekita mizizi.
-Chini ya CCM shilingi imeporomoka na kufariki.
-Chini ya CCM huduma ya Afya ni shida
-Chini ya CCM Wajawazito wanajifungulia chini mahosptalini
-Chini ya CCM gharama za maisha zimepanda kukithiri.
-Chini ya CCM ajira hakuna kwa wasomi.
-Chini ya CCM viwanda vimekufa
-Chini ya CCM mashirika ya Umma yamekufa.
-Chini ya CCM Rasilimali zinatumika hovyo.
-Chini ya CCM Twiga wamepanda ndege bila kuonekana na rada.
Hawa twiga sijui walikuwa na Passport!
-Chini ya CCM waandishi wa habari wameuawa.
-Chini ya CCM maelfu ya wanavyuo hawana mikopo
-Chini ya CCM Elimu ya kuanzia shule ya Msingi hadi Chuo kikuu imeshuka kiwango cha ubora.
-Chini ya CCM maisha yamekuwa magumu zaidi
-Chini ya CCM ni asilimia Chini ya 20 ya watanzania wanaumeme wa uhakika
-Chini ya CCM foleni kwenye majiji ni shiiiiiiiida
-Chini ya CCM kilimo hskina tija kabisa na umaskini umewatafuna watanzania wengi
-Chini ya CCM wafanyakazi wameendelea kua na mafao duni na maxingira duni Huku kodi ikiwa juu
-Chini ya CCM wafugaji na wakulima wameendelea kuchapana
-Chini ya CCM mikataba yote ya madini, Gas, Alma's na kadhalika imeendelea kua Siri
-Chini ya CCM rasimu ya Katiba ya wananchi ilinyofolewa
-Chini ya CCM deni la taifa limeendelea kupanda kwa kasi ya sjabu
-Chini ya CCM ajira kwa vijana imekuwa shiiiiiiiiiiiiida
Peleka ujumbe huu Twitter, Instagram, Facebook, JF, mwanahalisi forum
-NIMEJIANDIKISHA
-Nimejipanga
-NITATUMIA KIKATIO CHANGU VIZURI