Kweli ATCL wanastahili kutumbuliwa


Heeeeeeeeh...Watanzania tuko wa aina nyingi kwa mawazo na maoni.......si rahisi kumshinda Mtanzania kwa kejeli.....
 
Sina haja kukwambia nimetembea wapi na nakuhakikishia hakuna ulazima hayo mashirika yamilikiwe na kuendeshwa na serikali.

Ona mkenge wa kwanza wa hapa kwetu serikali wakaamua kununua taslimu. Ndo ujue serikali haijupaswa kudili na hayo mambo maana wao faida sio ishu. Wanateketeza tu pesa yetu.

Kujitangaza utalii sio lazima ndege. Idadi ya watalii huku imeendelea kukua na shirika halipo. Unataka uthibitisho gani zaidi? Kenya wanalo shirika na idadi imepungua Mombasa hadi wakaanza kulalamika Znz wanawachukulia watalii.

Kama haitoshi, wanalo shirika (japo hawamiliki %100) na bado watalii wanaspend zaidi wakiwa huku kuliko wakiwa huko kwao wenye ndege. Narudia tena. Hoja ya kusema shirika likimilikiwa na serikali kuna faida za ziada km utalii si ya maana sana.
 
Ni kweli uamuzi wa kuweka route moja ya usiku sio mzuri. Lakini isingekua busara kila mara CEO anapofanya uamuzi mbaya atumbuliwe. Apewe mwaka mzima wa fedha au hata miaka miwili...akikosea ajisahihishe. Baada ya kipindi hicho tuangalie financial statement ya ATCL..kama ametengeneza faida basi aendelee...kama katengeneza hasara na maelezo yake hayajitoshelezi...basi atumbuliwe.
 
Hakuna ambacho sijakujibu. Hao ET kuwa wanyoofu haiondoi ukweli kuwa Ethiopia inaongozwa kiimla zaidi. Na pengine ndio maana wanafanikiwa na hilo shirika.

Umesema hakuna nchi inafikiria kuachia shirika lake. Unatania labda. Uliza mswisi akuambie kwanini kauza lake Lufthansa.

Mimi nasisitiza tuna nafasi ya kuwaiga waliofanikiwa. Na hakuna ubaya Taifa stars kuiga ufaransa kwenye mafanikio. Kanuni za kufanikiw ni zilezile kwa tajiri na maskini. Wenye kuwahi kuzifuata ndio wanaofanikiwa mapema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…