IFANYE KWARESMA 2025 KUWA YA TOFAUTI KIROHO
🟪🟪 Kwaresma ni kipindi maalum sana kiroho, ni safari ya kwenda nyikani na Bwana Yesu kwa muda siku 40.
🟪🟪 Kipokee kipindi hiki kama fursa ya Kiroho kwani ni kipindi cha kufunga, Kusali, Kutubu, na Kufanya matendo ya Huruma kwa wahitaji.
🟪🟪 Jiandae kiroho kwa kufanya toba halisi.
🟪🟪 Usiingie kwenye mfungo huu maalum ukiwa moyo wako una makwazo ama manung'uniko yeyote achilia kila jambo lililo gumu na ubaki huru.
🟪🟪 Weka nia maalum ya mfungo kwa kutenga na kumwambia Mungu akupe msaada hasa changamoto nzito na ngumu ambazo kwa upande wako unaziona huziwezi.
🟪🟪 Kama huna changamoto yeyote ya kiafya mfano kama si mjamzito ama husumbuliwi na ugonjwa wowote tafadhari jinyime kwa kutokula chakula.
🟪🟪 Usifunge kwa kujionyesha kwa watu kwamba na wewe umefunga, funga kwa kusudi ama nia uliyoikusudia ili Mungu akupe msaada wake.
🟪🟪 Kumbuka kipindi hiki hutokea mara moja tuu kwa mwaka hivyo ifanye kama fursa ya kiroho ambayo mara tuu baada ya kumaliza mfungo utavuna na kujiwekea akiba kubwa ya kiroho.
🟪🟪 Uwapo kwenye mfungo waombee na watu wengine kwani ukifanya hivyo Mungu atapokea maombi yako haraka na kwa urahisi.
🟪🟪 Saidia wahitaji hasa kwenye kipindi hiki cha Kwaresma, watu wote Mungu amewaumba kwa mfano wake hivyo unavyowasaidia tambua kwamba unagusa mboni yake.
🟪🟪 Omba kwa imani na Mungu ataisikia sauti yako
🟪🟪 Omba kwa kumaanisha na Mungu ataenda kukutendea sawa sawa na mapenzi yake
🟪🟪 Safari hii ya siku 40 itakuwa ni historia kwenye maisha yako kwani ukifunga na kuomba kwa imani Mungu ataenda kuruhusu mambo makuu mnoo yatendeke maishani mwako.
🟪🟪 Nakutakia Mfungo mwema wa Kwaresma na Mungu akubariki sana 🙏🏿🙏🏿🙏🏿