Kwaresma 2018 Special thread...

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,688
106,806
Wapendwa katika Kristo
Tumsifu yesu Kristo...

Nawakaribisha waumini wote wa kanisa Catholic na wengine wote wanaoshiriki mateso ya bwana Yesu kristo kwa kufunga na kujielekeza mbele zake MUNGU kipindi hichi cha KWARESMA.
Nawaalika sasa tuweze kutiana moyo, kukumbushana, kufundishana kupitia uzi huu.
Kama una document za kidini weka hapa, nyimbo, picha, sala, miatari ya biblia weka hapa...

Wako katika kristo Da'Vinci..

Tunakimbilia..........
 
Kwaresma ni nini......?

Kwaresma ni kipindi ambacho waamini wakatoliki tunajiandaa kwa ajili ya kuadhimisha mafumbo ya pasaka. (Kifo mateso na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo) Katika kipindi hiki sisi waamini tunaalikwa kutazama tulikotoka yaani kuanzia siku ya ubatizo wetu na kujihoji kwa kina kabisa kama bado vile viapo vyetu tulivyo apa siku ya ubatizo wetu tuna vishika bado ama la! Siku ya ubatizo tunapewa nguo nyeupe na mshumaa unaowaka sasa ni wakati wakujiuliza, Je! Ule mshumaa bado unawaka au umezima kutokana na mapungufu yetu? Kama umezima niwakati sasa wa kuuwasha mshumaa tena, pia kama nguo ile nyeupe tuliyo pewa siku ya ubatizo imechafuka ni wakati sasa wa kuifua kwa kiti cha kitubio. Kwa ujumla ni wakati wa kuingia ndani ya moyo wako na kutazama kama kweli bado tunashika sheria na maagizo ya Mungu. Kwa hakika kwaresma ni muda wa kujitakasa, na kujuta na si hivyo tu bali kuwa jirani zaidi na Mungu kwa kutenda matendo mema kama vile kuwasaidia watu, kufunga na kusali.

Reference..
1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
Mathayo 4 :1

2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
Mathayo 4 :2
 
Kwanini tunaanza kipindi cha kwaresma siku ya jumatano ya majivu na siyo jumapili?

Wapendwa mnao nisoma hivi sasa naomba sasa nieleze hii kwaresma ilitoka wapi na ilianzeje anzeje. Mpendwa unaye nisoma hivi sasa Kanisa la mwanzo halikusherekea sherehe kama vile Krismasi , pasaka n.k ila kulikuwa na kusherekea ufufuko wa Bwana mara moja kwa wiki.

Lakini baadae mama kanisa alitafakari na kuona umuhimu wa kusherekea kwa namna ya pakee mafumbo ya Imani yetu. Hapo wapendwa Pasaka ambayo ndiyo hasa kumbukumbu ya kifo na ufufuko wa mkombozi wetu Yesu Kristo ilipewa kipaumbele na kuitwa mama wa sherehe zote. Hakika ikawa ndiyo sherehe ya muhimu kuliko zote.

Na ilipofika karne ya pili wakristo wote walisherekea ufufuko wa Bwana. Sherehe hizi za Pasaka zilianza usiku wa vigilia ya pasaka na kumaliziwa na Ekaristi Takatifu. Kuhudhulia mkesha wa pasaka ilikua ni kitu muhimu sana kiasi kwamba mwandishi maarufu wa kipindi hicho, yaani Tertulian aliandika na kuwashauri wasichana wasiolewe na wapagani kwani itakuwa ngumu kumruhusu kwenda kwenye mkesha huo.

Miaka mia mbili baada ya Kristo, Wakristo walipenda kunufaika na matunda ya kiroho yaliyotokana na kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, walianzisha utamaduni wa kujiandaa walao kwa siku tatu kabla ya sherehe yenyewe, katika siku hizo tatu wakristo hao walisali, wakatafakari na kufunga.

Tena wakasema Pasaka isiandaliwe tu ila inabidi isherekewe pia, ndipo sasa majuma saba yakawekwa ili kusherekea sherehe hiyo yaani, siku Hamsini ambazo waliziita pentekoste. Katika siku hizo watu hawakuruhusiwa kufunga na watu walibatizwa katika kipindi hicho. Hakika katika siku hizo hamsini Pasaka ilisherekewa kweli kweli.

Mwaka wa 350 baada ya Kristo, wakristo waliona siku tatu tu kwa ajili ya maandalizi ya sherehe kubwa kama Pasaka hazitoshi hata kidogo hivyo waliamua kuongeza siku za maandalizi ya sherehe hiyo kubwa kabisa ya Pasaka, Mpendwa uliyeuliza swali pamoja nanyi wapendwa mnao nisikiliza hivi sasa hivyo ndivyo kwaresma ilivyo anza.

Wapendwa mnaonisiliza hivi sasa, naomba tuelewe kuwa mfungo wetu ni wa siku Arobaini, kwanini Arobaini? Kwasababu kwa Wayahudi arobaini ilikuwa ni namba kamili, Mda wa kutosha mtu kuweza kufanya jambo Fulani. Ndiyo maana utasikia Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini, Yesu alifunga siku arobaini n.k. na nukuuu, “kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.” Math 4:1-2 N.k

Hivyo wapendwa tukirudi kwenye swali letu kwanini jumatano ya majivu tunaanza kwaresma na siyo jumapili. Jibu hapa ni hili naomba tuelewane vyema kwani tunaingia katika mahesabu. Tukihesabu kutoka jumapili ya kwanza ya kwaresma mpaka jumapili ya pasaka tunapata siku 42.

Lakini ikumbukwe na kujulikana kuwa kutoka mwanzo jumapili hazikuhesabiwa kama siku za kufunga kwani zilikuwa zinatawaliwa na mambo yanayo husu ufufuko hivyo ilikuwa ni kama siku ya ufufuko yaani pasaka ndogo.

Na kabla hatujaifikia pasaka yenyewe kuna jumapili sita hivyo hizo jumapili sita zilitolewa na hivyo kubakiwa na siku 36 tu ambazo hazijafika arobaini na hivyo ili kupata arobaini kulikuwa na ulazima wa kuongeza siku nne na ndiyo kisa hasa cha kuanza kipindi cha kwaresma jumatano ili tupate siku nne za kujazia pale kwenye thelasini na sita yaani siku hizo ni jumatano, alhamisi, ijumaa na juma mosi.

Narudia tena. Tukihesabu kutoka jumapili ya kwanza ya kwaresma mpaka jumapili ya pasaka tunapata siku 42. Lakini ikumbukwe na kujulikana kuwa kutoka mwanzo jumapili hazikuhesabiwa kama siku za kufunga kwani zilikuwa zinatawaliwa na mambo yanayo husu ufufuko hivyo ilikuwa ni kama siku ya ufufuko yaani pasaka ndogo.

Na kabla hatujaifikia pasaka yenyewe kuna jumapili sita hivyo hizo jumapili sita zilitolewa na hivyo kubakiwa na siku 36 tu ambazo hazijafika arobaini na hivyo ili kupata arobaini kulikuwa na ulazima wa kuongeza siku nne na ndiyo kisa hasa cha kuanza kipindi cha kwaresma jumatano ili tupate siku nne za kujazia pale kwenye thelasini na sita yaani siku hizo ni jumatano, alhamisi, ujumaa na juma mosi.

Wapendwa bila shaka nimeeleweka mpaka sasa kwanini tunaanza kipindi cha kwaresma jumatano ya majivu na siyo jumapili.

Wapendwa mnaonisiliza hivi sasa, pamoja nawe uliyeuliza swali naomba nisikuache bila kukwambia hili kuwa kwaresma ilikua na uhusiano mkubwa sana na wakatekumeni, miaka ya 350 baada ya Kristo mama kanisa aliamua kuwa wakatekumeni nilazima wafundishwe mda wa kutosha waliudhulia mafundisho nakuelezwa misingi ya mafundisho ya imani yao na walionesha nia yao yakutaka kuwa wakristo kwa kujitahidi kuishi maisha yasiyo ya dhambi.

Na hivyo ubatizo ulitolewa siku ya vigilia ya pasaka na kisha kumalizia kesho yake yaani siku ya pasaka kwa sakramenti ya ekaristi Takatifu, kwa vile maadhimisho ya ubatizo yalikuwa ndiyo hasa kiini cha vigilia ya Pasaka basi kwaresma kikawa kipindi muhimu sana kwa wakatekumeni ambapo kusema kweli ilikua ni hatua ya mwisho kabisa kabla hawajapokea sakramenti.

Katika siku hizo arobaini mkufunzi wao alikuwa ni Askofu mwenyewe na walitakiwa kujaribiwa kwa mtihani kama wameelewa kile wanachotakiwa kukiamini. Mtihani huu ulifanyika siku ya juma tano ya wiki ya nne. Iliitwa siku ya mtihani Mkuu. Na pia ilikua ni siku ya kuhakikisha huyu mkatekumeni anajua kanuni ya imani pamoja na sala ya Baba yetu kwani sala hizi ndizo zinazotoa mhitasari wa mafundisho makuu ya kanisa katoliki.

Na hili kuthibisha kuwa hiki kipindi kizima kilihusiana sana na wakatekumeni siku ya vigilia masomo yaliyo chaguliwa yalihusu, mwanga, maji, imani na ushindi wa Kristo kwa kifo na ufufuko wake.

Sasa naomba niendelee kufafanua, kwaresma kama nilivyosema hapo mwanzoni kuwa ni matayarisho ya pasaka. Hiki kipindi kinaanza kutoka jumatano ya majivu mapaka Misa ya alhamisi kuu ya jioni yaani (the last supper mass).

Katika kipindi hiki kuna mambo ya kuzingatia mosi, aleluya haitaimbwa kipindi chote cha kwaresma mpaka vigilia ya pasaka. Pili jumatano ya majivu ni siku yakufunga kwa kanisa zima na tatu waamini nilazima wajue kuwa kipindi cha kwaresma ni wakati wakujikumbusha viapo vyetu vya ubatizo tena, Wakati wa kwaresma kuanzia jumatano ya majivu mpaka jumamosi kabla ya dominika ya Matawi kumbukumbu za watakatifu haziazimishwi, isipokuwa kwa kufuata maelekezo ya vitabu vya Liturujia.

Kama haitoshi, kwa sababu maalumu tu, au kwa manufaa ya kichungaji Misa inayofaa kwa ajili ya shida mbalimbali inaweza kuadhimishwa. Misa za ahadi na marehemu zimekatazwa katika kipindi hiki. Pia, Ee Mungu twakusifu na utukufu husemwa au kuimbwa katika sherehe, sikukuu na katika maadhimisho ya pekee tu. Alafu , Breviari katika siku za juma ,Antifona ya Mwaliko, Tenzi za Kipindi cha masomo, masifu ya Asubuhi na Masifu ya jioni na antifona za vipindi vya mchana ni kadiri ya wakati wa kwaresma.

Si hivyo tu bali pia, hairuhusiwi kupamba altare kwa maua ;kinanda na ala nyingine za Muziki zinaweza kutumika tu kwa ajili ya kusaidia kuimba , ikibidi. Isipokua katika Dominika ya nne ya kwaresma: Ambayo kitaalamu inaitwa Dominika ya Furahi yaani Laetare katika lugha ya kilatini , na katika sherehe na sikukuu, Aleluya lakini ya katazwa

Mpendwa unayenisikiliza hivi sasa, ikumbukwe kwamba kwaresma ina jumapili tano, yaani jumapili ya kwanza ya kwaresma jumapili ya pili ya kwaresma jumapili ya tatu ya kwaresma, jumapili ya nne ya kwaresma na jumapili ya tano ya kwaresma.

Mpendwa uliye niuliza swali pamoja nanyi nyote mnao nisikiliza hivi sasa, ni hitimishe jibu la swali langu kwa kukwambia kwamba kwaresima ni mda wa kujipatanisha na Mungu, mwanzoni mwa kanisa watu waliotenda makosa makubwa walitengwa na kanisa, yaani jamii ya kanisa haikuwatambua.

Na hatakama watu hawa walikiri makosa na kujuta kanisa halikuwapokea haraka. Kwanza walitakiwa wafanye kitubio cha wazi hasa kama dhambi yao ilikuwa ni ya wazi na inajulikana na wote. Na mda wa hicho kitubio haikua tu labda kwa siku moja au la ilikua ni mda mrefu. Kipindi cha kwaresma kilikua ni kipindi cha matayarisha hayo.

Siku ya alhamisi kuu wakati wa Misa ambayo iliongozwa na Askofu, wote waliokuwa wametengwa na kanisa walitokea mbele ya watu wakiwa wamevaa magunia kuonesha kukili kwao wakiwa na majivu vichwani mwao wakionesha nia yao ya kubadilika yaani Metanoia. Askofu alikutana nao nakuwakumbatia kama alama ya kuwakaribisha tena katika kanisa.

Wapendwa huu utaratibu ulianza kupotea taratibu lakini umaana wa kwaresma kama kipindi cha matayarisho kwa ajili ya mapatano na mwenyezi Mungu pamoja na binadamu wenzetu na kanisa kiujumla unabaki. Hivyo wapendwa kwa pamoja tuingie katika kipindi hiki tukiwa tumeiweka mioyo yetu wazi kwa Mungu ambaye anatupenda, tumwambie tumekosa na tunaomba msamahaa.

Hivyo wapendwa mnaonisikiliza pamoja nawe uliyeuliza swali ni hitimishe swali la ndugu yetu aliyetaka kujua kwanini kwaresma inaanza jumatano na siyo jumapili kwakumwambia tunatakiwa kufunga siku arobaini hivyo ukihesabu Tukihesabu kutoka jumapili ya kwanza ya kwaresma mpaka jumapili ya pasaka tunapata siku 42.

Lakini ikumbukwe na kujulikana kuwa kutoka mwanzo jumapili hazikuhesabiwa kama siku za kufunga kwani zilikuwa zinatawaliwa na mambo yanayo husu ufufuko hivyo ilikuwa ni kama siku ya ufufuko yaani pasaka ndogo.

Na kabla hatujaifikia pasaka yenyewe kuna jumapili sita hivyo hizo jumapili sita zilitolewa na hivyo kubakiwa na siku 36 tu ambazo hazijafika arobaini na hivyo ili kupata arobaini kulikuwa na ulazima wa kuongeza siku nne na ndiyo kisa hasa cha kuanza kipindi cha kwaresma jumatano ili tupate siku nne za kujazia pale kwenye thelasini na sita yaani siku hizo ni jumatano, alhamisi, ujumaa na juma mosi.

Wapendwa bila shaka nimeeleweka mpaka sasa kwanini tunaanza kipindi cha kwaresma jumatano ya majivu na siyo jumapili sababukuu ndiyo kama nilivyoeleza tayari.

Mwishoni kabisa napenda kukwambia ndugu uliyeuliza swali pamoja nanyi nyote mnao nisikiliza hivi sasa, kuwa kanisa letu Takatifu katoliki la mitume lina mpangilio mzuri ambao hufuatwa hivyo jaribu kufuata utaratibu huo daima, ambao ukienda sehemu yoyote duniani utaukuta kwani kama nilivyosema kanisa hili ni moja na Takatifu lililo chini ya Mitume.

NJIA YA MSALABA KWA KIFUPI
Baada ya kifo cha Yesu watu wengi walipenda kwenda Yerusalemu kuigi. Wengi walipenda kupita njia aliyopita Yesu wakati wa mateso. Hivyo maujaji wengi walipenda sana na kufurahia sana jambo hilo hivyo walivyorudi walipenda kuendeleza yale waliyoyaona kule Yerusalemu, walitaka liwe tukio endelevu na la kudumu.

Hivyo vituo muhimu vilichaguliwa na hatimaye wakaanza kufuatisha wakikumbuka namna Yesu alivyopita huko Yerusalemu kutoka hukumu mpaka kifo chake pale juu msalabani. Hivyo ndivyo kifupi njia ya msalaba ilivyo anza.

Hakika nikipata muda nitakuwa radhi kufafanua zaidi.
 
Wapendwa katika Kristo
Tumsifu yesu Kristo...

Nawakaribisha waumini wote wa kanisa Catholic na wengine wote wanaoshiriki mateso ya bwana Yesu kristo kwa kufunga na kujielekeza mbele zake MUNGU kipindi hichi cha KWARESMA.
Nawaalika sasa tuweze kutiana moyo, kukumbushana, kufundishana kupitia uzi huu.
Kama una document za kidini weka hapa, nyimbo, picha, sala, miatari ya biblia weka hapa...

Wako katika kristo Da'Vinci..

Tunakimbilia..........
Milele Amina.
 
MASOMO YA MISA, FEBRUARI 14, 2018
KIPINDI CHA KWARESIMA
JUMATANO YA MAJIVU

SOMO 1
Yoe. 2:12-18

Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya. N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia Baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, na hao wanyonyao maziwa; bwana arusi na toke chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.

Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu, na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee Bwana, wala usiutoe urithi wako upate aibu, hata mataifa watawale juu yao; kwani waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?

Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 51:1-4, 10-12, 15 (K) 1

(K) Uturehemu, Ee Bwana, kwa kuwa tumetenda dhambi.

Ee Mungu, nirehemu,
Sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu. (K)

Maana nimejua mimi makosa yangu,
Na dhambi yangu I mbele yangu daima.
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,
Na kufanya maovu mbele za macho yako. (K)

Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
Usinitenge na uso wako,
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. (K)

Unirudishie furaha ya wokovu wako;
Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,
Na kinywa change kitazinena sifa zako. (K)

SOMO 2
2 Kor. 5:20 – 6:2

Ndugu zangu, basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.

Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Zab. 95:8

Msifanye migumu mioyo yenu; msikie sauti ya Bwana.

INJILI
Mt. 6:1-6, 16-18

Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampatai thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.

Amini, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amini, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa nafunga, Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
 
JE, KWARESMA NI KWELI SIKU 40? MBONA ZIPO SIKU 46?

Ukijaribu kuhesabu kwa umakini kuanzia Siku ya JUMATANO YA MAJIVU hadi SIKU YA PASAKA utakuta zipo jumla ya Siku 46.
SWALI: JE, KWARESMA NI KWELI SIKU 40?
JIBU: NDIYO.
SWALI: KIVIPI?
JIBU: Jumla ya siku ni kweli zipo 46 kama ifuatavyo:
Jumatatu = 6
Jumanne = 6
Jumatano = 7
Alhamisi = 7
Ijumaa = 7
Jumamosi = 7
Jumapili = 6
JUMLA = 46

Katika kuhesabu Siku za Mfungo, siku zote za Jumapili huwa zinatolewa katika Mfungo yaani Jumapili zote 6. Kwahiyo katika zile siku 46 ukizitoa Siku 6 za Jumapili, zinabaki siku 40 za Kufunga.

SWALI: Kwanini hizo siku za Jumapili zitolewe?
JIBU: Ni kwasababu Siku ya Jumapili yoyote ile tunaadhimisha PASAKA NDOGO yaani tunasherehekea na kukumbuka Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyefufuka Siku ya Kwanza ya Juma yaani Jumapili baada ya Sabato kwisha,(Rejea Mt. 28:1-15). Hivo basi, hatuwezi kufunga siku za Jumapili kwasababu ni Pasaka Ndogo na Pasaka huwa tunasherehekea. Kwenye sherehe siku zote hakuna kufunga maana Bwana Harusi tunakuwa naye tukiukumbuka Ufufuko wake ambao ndio Kilele cha Ukombozi wetu sisi Wakristo.

"BASI ENENDENI MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI WANGU" (Mt. 28:19).
 
Back
Top Bottom