Kwanini??????

"mungu alipo muumba adamu hakumwacha pekee awe peke ake akamfanyia msaidizi.............................."
 
I Love them ladies, wao na mapungufu yao, pia na kwa uwezo walio nao. Nawapendeni sana mama zangu, nawaheshimu na kuwathamini
 
Najiuliza, lakini sipati jibu.
Kwa nini madume ya ng'ombe yakitoka malishoni hukaa nyuma na majike hukaa mbele?
Najiuliza kwa nini simba dume anaitwa King of the Jungle, lakini jike haitwi Queen of the Jungle.
Najiuliza kwanini jogoo ana umbo kubwa kuliko temba, tena yeye ndio huwa wa kwanza kuwika.
Najiuliza kwa nini wanawake wanahitaji ulinzi kutoka kwa wanaume, lakini wanaume hawahitaji ulinzi kutoka kwa wanawake.
Hivi kwa nini wanawake wana umoja wao lakini hamna umoja wa wanaume?
Sijajua kwa nini leo hii eti wanawake wanataka kuwatawala wanaume huku wakiwananga na kuwasimanga wakitumia misamiati mbalimbali ukiwemo ule wa mfumo dume?

Bujibuji mbona umeulizia vitu vinne lakini swali la mwisho ndio limeibua mjadala???NAJIULIZA
 
Back
Top Bottom