.Tuliaminishwa tukaamini kua Tanzania kuna upinzani imara sijui kama bado tuna imani hiyo
.Tukaaminishwa tukaamini kuwa uzaledo ni kufunga mikanda tukaifunga sawasawa wenzetu wakailegeza wakanenepa
.Tuliaminishwa kua wazungu ndio wabaguzi peke yao, baada ya kuchomwa moto na weusi wenzetu huku tukiokolewa na wazungu hatuamini hivyo tenaq
.Tuliaminishwa tukaamini eti Nduli alipata kula nyama za watu, mpaka sasa sijui ni wa gapi bado wanamini hivyo
.Tuliaminishwa tukaamini kuwa kutoa na kupokea rushwa ni kosa kubwa ,, bado tunaamini hivyo ila mhhhh mbona wale watoaji wa..... wako huru
.Tuliaminishwa tukapinga kuwa daraja la Kigamboni ni possible,, leo tunaona aibu daraja limekamilika
Tuliaminishwa tukaamini kua kuna mchungaji anatoa misukule,, sijui kama bado tuna amini katika hili
Tuliaminishwa tukaamini eti ZZK ni msaliti nadhani tumebaki wachache tunao amini katika hili
.Tuliaminishwa tukaamini kua Tanzania ni kisiwa cha amani, tulipoanza uwa ndugu zetu albino sidhani kama tunaweza amini dhihaka hii
.Tuliaminishwa kua Mtwara na Kigoma kuhamishiwa kule kikazi ni kama adhabu,,sasa tunagombania kwenda huko
JE WEWE NDUGU YANGU ULIAMINISHWA NINI NA SASA HALI NITOFAUTI?