Naomba kufahamu kwa nini zinaa inakuwa dhambi?
Vitabu vyote vya dini vinapiga maarufu zinaa.
Hata mila karibu zote zinakataza zinaa.
Naamini hakuna kinachotokea bila sababu, lazima kuna sababu ya msingi kuikataza zinaa.
Kama kitendo cha watu kukutana kimwili kingekuwa kibaya. Mbona watu walio kwenye ndoa wanafanya mapenzi na sio shida!!?
Kwa nini ukifanya nje ya ndoa au kabla ya ndoa ndio inakuwa dhambi?
Je, kuna uhusiano wa dhambi ya kuzini na mapadre kutooa?
Je, kuna uhusiano wa dhambi ya kuzini na maustaaz kuwakwepa wanawake ( maustaaz wa tiba)?
Kuna madhala yoyote kwenye ulimwengu wa kiroho unaosababishwa na kufanya ngono?
Kuna vitu kama utakaso, janaba nk
Ebu intelligent anaejua anipe somo kidogo
1. Mkuu, Dhambi (Uasi kwa Mungu i.e. usifanye hiki, usifanye kile n.k. amri 10 za Mungu) ZOTE nyingine hufanyika nje ya mwili wako lakini Dhambi ya ZINAA (Uzinzi) hutendeka ndani ya mwili wako mwenyewe.
2. Kama unaamini kwamba Mungu ndiye wa kwanza/chimbuko aliyewaumba wanadamu
basi kwa upendo wake kwetu ss wanadamu, aliamua kutushirikisha kazi hiyo ya uumbaji. Kwa maneno halisi ni kwamba alitupatia uwezo huo wa kiMungu wa Uumbaji kwa kupitia Tendo la ndoa/kujamiiana. Kwa mantiki hiyo kujamiiana ni ni Tendo Takatifu mno linalopaswa kufanyika kwa Heshima zote na kwa Utaratibu maalum.
3. KiTendo cha kujamiiana ni kitendo ambacho hupelekea Kupatikana kwa binadamu/Mtu mpya(Mtoto). Binadamu/Mtu huyo mpya hutokea kwa kuchanganya gene/vinasaba nusu ya Me na nusu ya Ke(wanasayansi watanielewa) kwa hiyo, huyo mtoto atakayezaliwa atakuwa na pedigree au Ukoo unaoeleweka.
4. Jamii takriban zote zinapinga zinaa kwa sababu kujamiiana hovyo(Bila utaratibu) mara nyingi (kama mimba itatungwa)huwa inaleta shida katika Ukoo wa mhusika esp. unapokosekana Ukweli na Uhakika ni mtoto wa nani au tuseme ni Mtoto wa Ukoo gani (Damu ya nani?) Mara nyingi jambo hilo la kukosekana uhalisia wa ni Ukoo wa nani/ni Damu ya nani limeleta shida kubwa sana katika ukoo anakolelewa mtoto.
Utasikia oh, litoto hili jizi,mara mtoto huyu haambiliki, mara, ukoo au mizimu ya ukoo wake haipatani na mizimu ya ukoo wetu n.k. Yote hayo lakini hujitokeza pale wahenga waliposema Majuto ni Mjukuu. Kusahihisha kosa hilo huwa ni ngumu sana. Je, mtoto huyo akifa atazikwa wapi n.k.
Kwa hiyo ili kuepukana na madhila hayo kama yalivyoorodheshwa hapo juu, bora tu Uache Zinaa - Oa uishi na mke wako kwa amani, mkajilie Tunda mnavyotaka kwa Starehe zenu. Asante.
Hakuna Uhusiano wowote wa dhambi ya kuzini na mapadre kutooa. Mapadre ni watu kama watu wengine ni Wakristu.
Zingatia kwamba kuoa ni kitendo cha hiari baina ya watu wawili(Me na Ke) ni Ahadi/Kiapo (ndo maana kuna mashahidi). Padre ameamua kutokuoa.