EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Kitendawili cha kodi Tanzania kitatatuliwa pale tutakapopata serikali itakayokuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu. Ni magumu ndiyo kwani nchi nzima itatikisika na kutakuwa na upinzani mkubwa sana dhidi ya mpango husika. Mwanzoni wadau wataona ngumu kumeza!hivi ni kwanini mpaka leo bajeti zetu zinategemea misaada ya nje? kwanini mpaka leo tumeshindwa angalau kucopy kwa wenzetu wao wamefanyeje kujenga uchumi wao?
mbali na kwamba sisi hatuna technolojia kama wao lakini kwanini tumeshindwa japo kuweka mifumo sahihi ya ukusanyaji kodi ili kwamba kila mtu anaepaswa kulipa kodi alipe bila kukwepa na kodi iwe rafiki kwa mlipaji?
Mapendekezo yangu kuhusu ukusanyaji kodi ambayo itasaidia kuboost mambo flani flani mbali na raslimari zingine zilizopo nchini:-
serikali iweke mfumo sahihi wa ukusanyaji kodi kwa wafanya biashara wote kama ilivo kwa watumishi wa umma ambapo imeweza kuwakata moja kwa moja kutoka kwenye salary zao,hapa kwanza kabisa ihakikishe biashara zote zinakua scientifically registered(biashara na wafanya biashara wote wasajiliwe kielekronic) tofauti na sasa ambapo mtu naanzisha biashara hakuna anaejua kama unaduka/kibanda sehem flani.
Hii itarahisisha kuzitambua biashara zote na wafanya biashara sehemu waliko,mkoa,kata,mtaa n.k japo hadi sasa leseni zinatolea kwa njia hiyo lakini mkazo uongezwe kila anaetaka kuanzisha duka/ kibanda sehemu yoyote lazima asajiliwe kielectronic na apewe control number ya kulipia kodi.
Hapa asikubaliwe kufungua chochote bila kusajiliwa katika mfumo wa ulipaji kodi.Hii itawarahisishia TRA kukusanya kwa usahihi kwasababu watu wote watakua computerized hivyo yule ambae hajalipa wataweza kumfahamu aliko na kumuface moja kwa moja.
b) majengo yote na wamiliki wote wawe computerized mtaa kwa mtaa kwa sababu hapa napo ni sehemu nyingine inayoongoza katika ukwepaji kodi, watu wanamiliki nyumba hadi 10 lakni kodi hawalipi,hivyo basi kama nchi nzima nyumba zote zitakua compurized zikawekwa kwenye mfumo kila nyumba itakua inaonekana katika mfumo hakuna atakae kwepa kodi lakini pia lazima kodi iwe rafiki kwa kila manzania.
Nyumba za kulala wageni lazima kodi yake tena kwa mwezi iwe juu kidogo sababu wao wanaingiza kila siku,vivyo hivyo nyumba za biashara na nyumba za kawaida za kuishi lazima zipangiwe kodi stahiki.Hii kama kweli ikifanyika nchi nzima mapato yatapaa kwa namna moja ama nyingine.
Nchi lazima ijengwe na watanzania wenyewe kwanza wengine wataendeleza,na katika haya yote lazima viongozi kidogo wawe wazalendo,pia kodi itakayo kua inakusanywa nchini lazima itumike effectivelly tofauti na kwenda kufanya shughuli za kisiasa zisizo na tija kwa taifa na watanzania.Kitu kingine mimi kwa upande wangu sioni sababu ya kuendelea kulipia lesseni za biashara na lesseni nyingine zozote badala yake watu wawe wanapewa bule kama ilivo kwa TIN number. Hivyo basi ulipaji ubaki tu kwenye kodi TRA badala ya kulipia vyote.kama mambo yote hayo yatasimamiwa kikamilifu ukusanyaji tra lazima kwa mwezi watusomee tr 5.
Kuendelea kuziachia halmashauri zikusanye kodi katika mukitadha huu tunao utumia ni kuendelea kupoteza mapato ambayo kama mfumo mpya wa computerized ungetumika basi kila mmoja angeweza kufikiwa kwa urahisi na yule ambae hajalipa angeweza kuonekana mara moja katika mfumo.
Lakini pia yote hayo inafaa yaende sambamba na katiba mpya kwa sababu kama katiba isipo badiika awamu flani inaweza ikatekeleza nyingne ikaja kuharibu kwa kuanzisha mifumo mipya.Pia katika masirahi mapana ya nchi lazima itikadi za vyama ziwekwe pembeni wabunge wajadili mstakabali wa nchi kuliko kujali vyama vyao.
yangu ni hayo mwenye nyongeza,masahihisho aongezee
Ili ukusanye kodi kirahisi lazima uwe na mfumo mmoja wa malipo nchi nzima yaani Centralized Payment System. Mfano ni ilivyo mifumo ya malipo ya huduma za kifedha (simu na benki). Ukifanya tu muamala papo hapo kila mtu anahesabu chake, TRA, halmashauri,nk.
Sasa hiyo mifumo itawafanya wafanyabiashara wengi ku-give up ukwasi ambao kimsingi siyo wa kwao (hujilimbizia kodi mbalimbali anazolipa mlaji na kuzifanya sehemu ya mtaji). Ukitaka ku-imagine itakuwaje rejea shughuli ya kuviunganisha vituo vya mafuta ilivyokuwa na upinzani mkali.
Hapo wanasiasa (wasio genuine) watakuja na hoja kama 'mfumo huu hautafanya kazi vijijini ambako hakuna mtandao'.
Ni hivi:
Kila biashara itakuwa na akaunti au trace/control namba yake maalumu kwenye huo mfumo wa malipo. Hapo miamala yote ya biashara hiyo ya kutoka na kuingia lazima ifanywe kwenye hiyo account au trace number hivyo mzunguko halisi wa biashara unaweza kuonekana kwa kugusa tu na kidole. Hata kodi hakuna atakayekaa kukadiria. Mfumo utaamua based on formula iliyopo.
Mfumo huu hauhitaji likompyuta la mezani bali unahitaja tule tumachine twa kushika tu mkononi yaani POS aka Point Of Sales. Rejea namna mawakala wa benki, wakatisha ushuru wa halmashauri, EFD, au maduka makubwa yanavyofanya kazi.
Pia huu mfumo hauwezi kuwa na ufanisi bila kuihusisha sekta binafsi (PPP).
Siku serikali inaleta hili pendekezo utasikia kelele kama zote kutoka kila kona. Ndiyo itajua haijui. Unakumbuka mpango wa 2016 wa kufufua sekta ya textiles kwa miaka mitatu (2016-18). Sehemu ya mpango ilikuwa kufuta mitumba kadri ya vile ambavyo viwanda vya ndani vingeongeza uzalishaji wa nguo mpya. Unakumbuka mziki wake? Serikali ikaufyata kama vile hakuna kilichotokea.
Sent using Jamii Forums mobile app