Kwanini wenye akili mawazo yao hayana nafasi na wenye akili ndogo mawazo yao ndio yanatuongoza

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,670
149,840
The intelligent people in this country have only forums to express their views ana ideas whereas the unintelligent ones have forums as well as power and mandate to implement their ideas.

Mnapoona kina Lissu wanaongea lakini hawasikilizwi mjue sababu ni hiyo.

Mnapoona kina Bashite mawazo yao ndio yanatekelezwa mjue sababu ni hiyo.

Unapoona wale wachache wanaosema hapana wanaonekana hawana hoja na wale wengi wanaosema "ndioooo" ndio wanaonekana wana hoja na uamuzi wao unapita, basi mjue sababu ndio hio.

Mnapoona tuna mikataba ya "kimangungu" mjue sababu ndio hiyo

Mnapoona tuna wasomi wazuri tu lakini wanaishia kuandika papers lakini hazifanyiwa kazi basie mjue sababu ni hiyo.

Mnapoona ripoti za kiuchunguzi za wataalamu zinaishia makabatini tu mjue sababu ndio hiyo.

Mnapoona tafiti za wataalamu wetu zinaishia makabatini tu mjue sabubu ni hiyo.

Tuna safari ndefu sana sisi na pengine hata tusifike mwisho wa safari hii.
 
The intelligent people in this country have only forums to express their views ana ideas whereas the unintelligent ones have forums as well as power and mandate to implement their ideas.

Mnapoona kina Lissu wanaongea lakini hawasikilizwi mjue sababu ni hiyo.

Mnapoona kina Bashite mawazo yao ndio yanatekelezwa mjue sababu ni hiyo.

Mnapoona tuna mikataba ya "kimangungu" mjue sababu ndio hiyo

Mnapoona tuna wasomi wazuri tu lakini wanaishia kuandika papers lakini hazifanyiwa kazi basie mjue sababu ni hiyo.

Mnapoona ripoti za kiuchunguzi za wataalamu zinaishia makabatini tu mjue sababu ndio hiyo.

Mnapoona tafiti za wataalamu wetu zinaishia makabatini tu mjue sabubu ni hiyo.

Tuna safari ndefu sana sisi na pengine hata tusifike mwisho wa safari hii.

Ndio maana nafikiri ni muhimu kwa katiba ya nchi kuweka msisitizo mkubwa kwenye dhana ya "trust but verify" kwa mambo yakitaifa. Kwa mfano;

1. Uteuzi wa nafasi za kitaifa. Raisi anateua, lakini bunge linathibitisha(verify).
2. Mikataba kati ya Tz na makampuni au nchi nyingine, serikali ikionyesha nia ya kuingia katika hiyo mikataba basi kamati za bunge/bunge zipitie hiyo mikataba na kuipigia kura(verify).
3. Upigaji kura wa wabunge/kamati za bunge uwe na uwajibikaji, yaani kura ya kila mbunge iwe katika kumbukumbu na kura zihesabiwe, na kumbukukumbu hizi ziwe wazi kwa umma(verify).

Pia nafikiri mipango ya maendeleo ya Taifa isiachiwe vyama vya siasa badala yake kuwe na Tume huru maalaumu ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa. Tume iiundwe na wataalamu wa mipango ya maendeleo katika nyanja mbalimbali. Pia kuwe na wawakilishi kutoka vyama vya kisiasa, n.k. Tume hii ndio itakuwa ni mmoja wa watumiaji wakuu wa matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini.

Hii itatusaidia kuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu inayotekelezeka na itakayo stahimili mabadiliko ya uongozi wa kitaifa.
 
Umeongea mambo ya msingi sana lakini hawa wenye kujifanya wana uchungu na nchi hawawezi kuwa tayiri kupokea na kufanyia kazi huu ushauri.

Hii nchi mawazo mazuri hayafanyiwi kazi bali yale ya hovyo hovyo na yasiyo na tija ndio yanayopewa nafasi kwasababu yanatoa mwanya kwa wakubwa kufanya wanayoyataka pasipo kubanawa wala kuwajibika.
 
The problem with Africa is that those with ideas have no power, and those with power have no ideas. And "amazingly" African people will always choose/elect those with no ideas over those with ideas..
Aliyeturoga Waafrika alikufwa
 
Shida ni kwamba hata ukipeleka bungeni kumejaa wabunge wanaojua tu kusema ndiyooooooooo! Ukiwauliza wamesema ndiyo kwasababu zipi hawana jibu zaidi ya kukwambia siwezi kupingana na serikali ya chama changu
 
Mkuu, na hii nimeiongeza hapo juu kama mfano mwingine.
 
Ndio maana nafikiri ni muhimu kwa katiba ya nchi kuweka msisitizo mkubwa kwenye dhana ya "trust but verify" kwa mambo yakitaifa. Kwa mfano;

1. Uteuzi wa nafasi za kitaifa. Raisi anateua, lakini bunge linathibitisha(verify).
2. Mikataba kati ya Tz na makampuni au nchi nyingine, serikali ikionyesha nia ya kuingia katika hiyo mikataba basi kamati za bunge/bunge zipitie hiyo mikataba na kuipigia kura(verify).
3. Upigaji kura wa wabunge/kamati za bunge uwe na uwajibikaji, yaani kura ya kila mbunge iwe katika kumbukumbu na kura zihesabiwe, na kumbukukumbu hizi ziwe wazi kwa umma(verify).

Pia nafikiri mipango ya maendeleo ya Taifa isiachiwe vyama vya siasa badala yake kuwe na Tume huru maalaumu ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa. Tume iiundwe na wataalamu wa mipango ya maendeleo katika nyanja mbalimbali. Pia kuwe na wawakilishi kutoka vyama vya kisiasa, n.k. Tume hii ndio itakuwa ni mmoja wa watumiaji wakuu wa matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini.

Hii itatusaidia kuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu inayotekelezeka na itakayo stahimili mabadiliko ya uongozi wa kitaifa.
Nimetamani Ku shake hands na wewe tatizo uko mbali like si kitu ktk hoja yako.
 
Sio kwa ccm hii Mkuu, hawawezi kukubali na lengo lao ni KUTAKA KUHARIBU NCHI NA WAMESHAHARIBU MNO MNO. HATA KATIBA MPYA HAWAWEZI KUKUBALI KABISA IPITE ILE ILIYOPENDEKEZWA NA WANANCHI.
 
Hili swali watu wa chade1 wanaweza kulijibu kwa ufasaha zaidi, maana haingii akili mbowe na zero yake lakini bado anawaongoza wenye masters, pHD na hata ma professor!!
 
Huwezi amini kuna utafiti ulikuwa presented FAO 2013 ulikuwa unasema,mpk mwaka huo takwimu zinaonyesha kuwa kuwa kulikuwa na watoto milioni14 ambao walikuwa wamedumaa,maana yake na ubongo umedumaa mpaka mwaka huo.sasa piga picha hao ndo wapiga kura wa kesho.Wapiga kura wa sasaiv wengi wao ni wale walidumaa miaka ya nyuma wakati wanakua.We angalia mikoa yenye vyakula vingi na watu wamesoma kama wanawachagua ccm
 
Hili swali watu wa chade1 wanaweza kulijibu kwa ufasaha zaidi, maana haingii akili mbowe na zero yake lakini bado anawaongoza wenye masters, pHD na hata ma professor!!
Hapa hatuongelei elimu ya mtu bali tunaongelea uwezo wa mtu kiakili katika kuchambua mambo na kufanya maamuzi.
 
Back
Top Bottom