Kwanini 'Wazungu' hupambana sana ili Mgonjwa asife, lakini 'Waafrika' hujitahidi mno kufanya 'Maziko' ya Kifahari kwa Marehemu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,559
108,897
Mzungu akiwa na Mgonjwa wake Hospitalini atahangaika hata kwa 'Gharama' zake zote tu ili 'ayaokoe' Maisha yake 'asife' lakini kwa Mwafrika ( Mswahili ) Yeye akiwa na Mgonjwa Hospitalini wala 'hajali' kivile na pengine hata kutoa 'Huduma' au 'Msaada' anakuwa mgumu ila pale Mgonjwa 'akifa' tu ndipo utaona 'anavyojitutumua' kwa Kuchangia 'Mazishi' huku akitoa 'ahadi' za kila namna Mazishini.

Je, Ubongo wa Mzungu na Mwafrika ( Mswahili ) ni sawa au si sawa? Kuna Jambo 'nimelishuhudia' leo na Kuthibitisha kuwa Waafrika tuna Majanga.
 
Mkuu tatizo letu ni roho mbaya ,,
Mgonjwa anaweza akafa kwa kukosa Dawa ya malaria ya 3000 ,,lakini suku akifa yule yule aliyemnyima pesa ya kununuwa dawa akagharamia hata millions kwenye mazishi yake..

Yaani 'hakyanani' isingekuwa ni huu mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 ambapo nimepanga 'Kura' zangu zote niwape John Magufuli na Tundu Lissu kwa 'upamoja' Wao, kuna Mtu angenipeleka Segadansi ( Jela ) kwa 'Kipondo' ambacho ningempa kwa 'Unafiki' wake. Tokea Mgonjwa wao 'augue' huu ni mwaka wa Tano ( 5 ) hajawahi 'Kuchangia' chochote kile na hata alipokuwa akipigiwa Simu na 'Nduguze' kutoa 'Mchago' wake alikuwa hapokei leo 'Mgonjwa' Israeli 'ameshamtwaa' ndiyo 'anajitutumua' Kuchangia 'Pesa' na Kutoa 'Huduma' Msibani Kwao.
 
Waswahili hujua kuwa gharama za kumuhudumia mgonjwa ni endelevu mpaka atakapopona. Hivyo wengi wao hukwepa kutoa msaada kwa mgonjwa pale unapohitajika. Ila akifa mgonjwa, gharama zake ni za mara moja (mazishi) pasi na kuzingatia kama marehemu kaacha watoto au mjane.

Hilo jambo la mgonjwa kutosaidiwa matibabu pia nimewahi kulishuhudia kwa familia fulani ambapo mzee wao alikuwa yupo taabani kitandani kadhoofu. Ndugu wakiwemo pia watoto walikuwa wagumu kutoa pesa ya kumsafirisha mgonjwa kwenda kupata matibabu zaidi hospitali bora nje ya mkoa. Kila mmoja alisema hana pesa. Akatokea mtu mmoja alipomwona mzee ktk hali ile akajipiga na kutoa pesa za matibabu. Yule mzee akafariki kabla ya safari. Kilichotokea ndugu wakawa ati wagombea kununua vifaa vya maziko.
 
Acheni kukariri misiba ya kizungu ni ghali kuliko manvyofikiri
Na misiba cheap kabisa ni kwa waislam sanda ubao na vitu vyake less than 100k kaburi kuchimba 50k au mnachimba wenyewe under 400k mnamaliza msiba

Umeulewa huu 'Uzi' lakini? au pengine bado uko Kitandani na 'Basha' wako 'anakutumikisha' zaidi 'Kibaiolojia' ndiyo maana umejibu 'Kipopoma' pia?
 
It's not by chance or choice... Its by design.

Na chimbuko lake ni Ukoloni.

Waafrika ukifuatilia mila zao za asili kupitia historia na mafundisho walipigania sana uhai wa mtu. Miji yao ukubwa wake ulipimwa kwa idadi ya watu hai na wenye Afya. Na kimsingi ndivyo inavyopaswa kuwa.

Lengo la wakoloni lilikuwa ni kututawala milele.. na hii wamefanikiwa.wametufanya na sisi leo tunawaza kama wao wanavyotuwazia.. cheap fuel to drive their economy.. sisi ni disposable

Muhimu kwetu leo ni rasilimali zetu.. lakini ukweli haya madini si muhimu kama watu wanakufa ni wenye afya dhoofu.. haya madini ni muhimu kwao wao wakoloni.

Kwa sasa hata miundo yetu ya kujitawala inaheshimu mawazo yao na sio yetu.. inatufundisha ushindani shuleni.. wao wanaondoa ushindani mashuleni.. toka mdogo inatunza kuwa mashindanoni na weusi mwenzetu na kwa kufanya hivyo tunakuwa rewarded..

Ikiwa elimu ni vita na bunduki zimegawiwa mashuleni basi nina hakika ili tu kushinda waafrika wengi wangetwangana risasi bila.kufikiria mara mbili..

Mie ninaamini kabisa kabisa sisi hatupendani maana hatuko huru na hapa tuko kwenye mashamba ya mkoloni tunaendelea kumlimia huku tunajichagulia wanyampara.. na kwa nadharia hiyo the sick and the weak don't save the purpose.. tunawaacha wafe.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom