Kwanini wazazi wengi wabinafsi sana?

Kwanini wazazi wengi wabinafsi sana?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Huwa najiuliza mara kwa mara ni kwanini wazazi huwa wabinafsi sana linapokuja kwenye swala la watoto wao wenyewe? Ninachomaanisha ni kwamba wazazi wengi huwalazimisha watoto wao kufanya mambo ambayo wao wenyewe hawawezi/hawataki kuyafanya!

Nitatoa mfano wazazi wengi huweka picha za watoto wao kwenye social media nyingi kama facebook &Co. lakini ya kwake haiweki au anaiziba, sasa ni kwanini anaweka picha ya mtoto halafu ya kwake haweki?

Ni nani kamwambia kwamba yule mtoto masikini ya Mungu anapenda kuwekwa kwenye kila mahali na kuonekena na Dunia nzima?
Huwo ni mfano tu lakini pia kuna mambo mengine sana ambayo wazazi/Mzazi hutaka mtoto ayafanye lakini yeye hataki kuyafanya sasa ni kwanini wanakuwa (Wazazi) wabinafsi namna hii?
 
Kwa mujibu wa maandiko mali,mke,watoto ni mapambo na matamanio ya ulimwengu,
Mtu mwanaume/mwanamke anapoweka chochote ktk nilivyotaja hapo juu ni muunganiko wa kifikra za kibinaadamu za kuonyesha ulimwengu na walimwengu kua amejaaliwa mke mzuri,watoto wazuri,nyumba/gari nzuri.

Pia muda mwingine kwa mzazi kuweka chochote kinachokuhusu ktk social media tunaweza kuchukulia kua ni njia moja wapo ya kuonyesha UPENDO na KUJALI juu ya familia yako.

Any way sidhani kama inawezekana kuweka kikao na mtoto wako mujadili nini anakipenda na nini hapendi itakua ngumu.

By the way kwa mtazamo wangu hakuna ubaya wa kufanya hivyo,, Hata mtoto nae ni mzazi wa baadae atafanya yake.

UBINAFSI NI WEWE MZAZI una kipato kizuri lakini unashindwa kuwapatia watoto wako elimu bora,makazi bora n.k

Ukiwa Bar unachoma nyama kilo 3 lakini nyumbani watoto hawajui walikula nyama lini.
 
Makamee, umeandika Yote niliyotaka kuandika. Hapa imebidi kuandika hiki ninachoandika ili kukuthibitishia wewe na wengine kwamba tupo tulio na mawazo kama ya kwako. Ungekuwa mgombea ungepata kura yangu.
 
We nawe. . .
Nilidhani utakuwa unaongelea kitu cha maana kama wazazi kula vizuri nje wakati watoto hawali vizuri nyumbani, wazazi kujipendelea mayai/maziwa nyumbani wakati watoto wanaamkia viporo, kuvaa vizuri wakati watoto wanavaa masambara, kutumia hela nyingi kwenye starehe binafsi wakati watoto wanaishi maisha ya kupungukiwa. Huo ndio ubinafsi.

Kum-show off mtoto kwenye social media ni kuonyesha fahari ya mzazi. Na hivyo vitu unavyosema mzazi anamwambia mtoto afanye na yeyr hafanyi ni vipi? Ina maana unataka mzazi asimhimize mtoto kusoma kwakuwa yeye hasomi? Mzazi asimkataze mtoto pombe sababu yeye anakunywa? Acha kuwa na mawazo mgando!!!!!
 
Back
Top Bottom