Kwanini watu wengine huogopa sana Sindano?

Kwanini watu wengine huogopa sana Sindano?

Yn mm sindano.siogopi..nilikuwa naogopa zamani..
Ukishakua mama sindano ht huna haja ya kuogopa maana utachomwa mwanzo.wa clinic mpk unajifungua..
Zipo za tetenus....kutolewa kwajili vipimo mbali mbali...yn there is no way ukakimbia sindano mama...
Mm hata kichwa kikiniuma sana nikiona panadol haifanyi kazi...namwambia hubby hebu nichome sindano bana nirelax zangu..maana unaweza umwa kichwa kisisikie kidonge ...
 
Mimi binafsi naiogopa saana Sindano licha ya kuwa nimechoma saana.toka enzi zile za sindano za kuchemsha ukiingia tu chumba cha sindano Yale maandalizi tu mi huwa hoi.
Mara nesi kachukua kibanio kaibua syringe kwenye sufuria yenye maji yanachemka na kutoa mvuke,Mara kachukua bomba la sindano , kaunganisha kisha kichupa cha dawa ananyonya dawa alafu ana test kuona kama dawa inapita kwenye sindano. Mara anachukua pamba iliyo na spirit anapangusa kwenye kalio kisha anapeleka sindano anachoma na kukamulia dawa.
Akimaliza anapitisha pamba tena na kukupa poleeee. Daaah sasa muda wote wa maandalizi mpaka mwisho nilikuwa nakua hoi kimawazo mpaka Leo sijazoea sindano sizipendi. Sasa enzi hizo unakuta ili uandikiwe sindano njama zinaanzia nyumbani tukifika pale ww kaa kimya mm (kaka/mjomba/mama) ntaeleza kuwa umetapika Mara tatu,huna hamu ya kula unapenda kukaa juani. Rohoni hupendi wao wanaamini sindano ndo tiba sahihi kwako. Kumbuka umeandikiwa kama 5 hivi moja kila simu halafu uzipendi na hazizoeleki.
 
...dohh hiki ni kikwazo kwangu hata ile ya kupima malaria huwa najifikiria mara mbili...naogopa sindano sababu zinauma
 
Back
Top Bottom