Kwanini watu wengine huogopa sana Sindano?

Kwanini watu wengine huogopa sana Sindano?

Mwene chungu

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
915
Reaction score
754
Salute!...

Niombe kujua kama kuna sababu zozote kisayansi zinapelekea hali hii kutokea.Nimeona kuna watu wazima (wasio watoto) kuangua vilio kabla na wakati wa kuchomwa sindano hata kama maumivu yake siyo ya kudumu.

Lakin hili linaenda sambamba na wanafunzi wanapoadhibiwa (chapwa) wapo ambao huogopa sana fimbo na wengine huwa huwaogopi hata kidogo!.Je ujasiri au uoga huu una sababu zozote za kisayansi?
Screenshot_2017-07-16-15-51-58.png
Screenshot_2017-07-16-15-50-46.png


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Nimemuona Leo mwanajeshi mmoja analia kama mtoto mdogo!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kawaida sana..mimi huwa silii wakati wa kuchomwa sindano
 
Ya tako au paja ni shida sana!!!!!...
Ile siku nilikuwa najifungua sasa kuna sindano ya paja pale... Aiseeee!!! Haikuwa kazi rahisi kama sio uchungu ningeweza kuahirisha kujifungua maana walinuchoma kabla mtoto hajatok...

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka mara ya mwisho kuchomwa sindano nlikuwa darasa la 3, kiukweli bora unirundikie vidonge kopo zima siyo sindano

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mimi hata kupima malaria uwa nachukia kuchomwa kidole.ila afya inatupa jeuri kweli.
Ukiacha sindano za kupimwa HIV.sikumbuki lini nilichomwa sindano

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ukweli sipendi sipendi sipendi kabisa kuchomwa sindano sijui ya tako sijui ya wapi, nachukia sana basi tu shida

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom