Kwanini watu wanailaumu TANESCO na si Watawala?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,731
Hii nchi yetu ina raia wapumbavu na ambao uwezo wao wa kuwaza mambo unatia shaka sana. Yani unakuta mtu anajiita msomi na anailaumu TANESCO kwa mgao wa umeme, yaani kuficha uzezeta wake anaamua kutoa lawama kwa TANESCO.

Hivi kwa akili hata za Chekechea TANESCO wanaweza kujiaumulia kuendesha migao ya umeme bila baraka za huko juu? kwamba TANESCO ndio wanao sababisha migao ya umeme? Migao inaenda mwaka wa tatu sasa kwamba shida ni TANESCO? akili za kipumhavu sana hizi, Mungu tusaidie waja wako.

Raisi na CCM yake ni watu wa kulaumiwa na wala sio TANESCO, sasa wajinga wajinga humu kutwa nzima na post za kuilaumu TANESCO kwa migao ya umeme.

Watawawala ndio wameshindwa kutawala, TANESCO haina shida, shida iko kwa watawala, hakuna kitu ambacho TANESCO wanajiamulia kufanya bila huko juu kujua.

Migao inapangwa huko Ikulu, na ratiba Mama anayo kabisa, na yeye ndio anapaswa kubeba lawama zote, na ifike wakati tuache ujuha tujitambue ndio maana tunafanyiwa maigizo na wakina Makonda kwa sababu walisha tuona hatunazo.
 
Kumbuka Jomo Kenyata aliwahi mwambia Nyerere kwamba kule Tanzania Nyerere anatawala Maiti, Jomo Kenyata aliona mbali sana, na alikuwa sahihi kwa kiwango cha kustajabisha.Nchi imejaa idadi ya watu ambao uwezo wa kuwaza ni janga kubwa sana sijajua shida ni nini.

Migawo ya umeme Tanzania mtu wa kwanza kubebe lawama ni Raisi yeye ndie mkuu wa nchi binafisi sioni sehemu ya kulaumu tanesco.
 
Kudadeki. Unajua umeniwahi nilikuwaga nataka niandike uzi huu nikawa nasahau.

Watanzania ambao ni wajinga hupenda kushughulika na mwishirizio wa tatizo na siyo chanzo cha tatizo. Na huu ndio mtaji wa wanasiasa.

Kwa mfano, wanasiasa wakiona TANESCO wanalalamikiwa badala ya wao, basi wao wanasiasa wanatulia kimyaaaa!

Kumbe ilikuwa inatakiwa kukomaa na serikali kwa kututia hasara kutokana na tatizo la umeme ili wawe imara katika kupanga na kutekeleza upatikanaji wa umeme nchini.

Katika hali ya kawaida, baraza la mawaziri linaundwa na rais na mawaziri, ambapo hujadili mambo mbalimbali ya kitaifa. Sasa iweje tatizo la umeme ilaumiwe TANESCO ikiwa yupo waziri wa nishati na huwa anawasilisha hali ya umeme na mipango yake ndani ya baraza la mawaziri ambapo na rais yumo!

TANESCO ni watendaji, hawawezi kujiamulia tu wakate umeme bila viongozi wa serikali kujua kinachoendelea.

Binafsi naona, unapokata umeme ni sawa na kucheza na usalama wa taifa kuanzia nyanja ya kiuchumi mpaka kijamii. Yaani TANESCO waamue tu kukata umeme bila mama kujua, hii haipo!
 
Mpumbavu mwenyewe!!
Lawama tunatoa kote ila tanesco ndio shirika lenye dhamana na umeme huo lazima maneno yawe mengi kwao
 
Kudadeki. Unajua umeniwahi nilikuwaga nataka niandike uzi huu nikawa nasahau.

Watanzania ambao ni wajinga hupenda kushughulika na mwishirizio wa tatizo na siyo chanzo cha tatizo. Na huu ndio mtaji wa wanasiasa.

Kwa mfano, wanasiasa wakiona TANESCO wanalalamikiwa badala ya wao, basi wao wanasiasa wanatulia kimyaaaa!

Kumbe ilikuwa inatakiwa kukomaa na serikali kwa kututia hasara kutokana na tatizo la umeme ili wawe imara katika kupanga na kutekeleza upatikanaji wa umeme nchini.

Katika hali ya kawaida, baraza la mawaziri linaundwa na rais na mawaziri, ambapo hujadili mambo mbalimbali ya kitaifa. Sasa iweje tatizo la umeme ilaumiwe TANESCO ikiwa yupo waziri wa nishati na huwa anawasilisha hali ya umeme na mipango yake ndani ya baraza la mawaziri ambapo na rais yumo!

TANESCO ni watendaji, hawawezi kujiamulia tu wakate umeme bila viongozi wa serikali kujua kinachoendelea.

Binafsi naona, unapokata umeme ni sawa na kucheza na usalama wa taifa kuanzia nyanja ya kiuchumi mpaka kijamii. Yaani TANESCO waamue tu kukata umeme bila mama kujua, hii haipo!
Kabisa watawala wanashangilia kuona walivyo safe, na jinsi sisi wajinga tunavyo itupia lawama Tnaseco, kumbe tunatupia lawama watu wasio sahihi na kuwaacha wanao paswa kutupiwa lawama.
 
Back
Top Bottom