Mgodo visa
JF-Expert Member
- Nov 1, 2016
- 3,606
- 3,676
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu.
Naamini kabisa, hiki kilicho nikuta, wapo wengine kutoka sehemu mbalimbali, kimekwisha watokea.
Hizi/hivi katika picha ni Flash (usb2.0 32GB) pamoja na Power Bank (made in Korea) Nimeuziwa bidhaa hizi na kijana, aliye kuwa anatembeza biashara zake Barabarani.
Nimefika Nyumbani na kugundua kuwa, uwezo wa Flash, si kama inavyo jieleza (32GB) kwani uwezo uliomo ndani yake, hakuna nafasi ya kuweka hata kitu chochote cha 1GB...!!
Nimekuja kugundua, uwezo wa Power Bank, hauwezi kuchaji/kubusti Simu hata kwa dakika 15.
Maana yake, nimenunua MCHINA (kama wengi wanavyo niambia)
Nimejiuliza maswali mengi, hivi ni kwa nini watu, tuzidi kununua vitu mkononi, badala ya kwenda katika Maduka husika...!!?
Je kama ningenunua bidhaa hizi Dukani, si ningeweza kurudisha nilipo nunua (nikiwa na Risiti yangu Mkononi) na kuweza kupewa/kubadilishiwa bidhaa halisi kwa thamani ya pesa yangu...!!?
Hivi Watanzania/Binaadamu tutafanyiwa mpaka lini huu utapeli, ambao wakati mwingine ni wakujitakia..!!?
Wana JF, Tubadirike....Pesa kwa sasa ni Ngumu kupatikana...cha kunisikitisha, vitu (bidhaa) hizi nimefungua mimi mwenyewe kwenye Maboksi...!
Siwezi kumlaumu sana MUUZAJI...najilaumu mimi na Nafsi yangu.
Nawasilisha..!