Kwanini watu husomewa mashtakta kwenye Mahakama zisizoweza kusikiliza kesi zao?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Unakuta anasomewa kesi ya mauaji kisha hatakiwi kujibu sababu mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kuna ulazima wa kufanya hivyo, au ni kupotezeana wakati?
 
Ni matakwa ya kisheria haswaa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, kwamba inapaswa kesi ipitie ktk mchakato uitwao 'committal proceedings' ambapo lengo lake ni kurahisisha mchakato wa usikilizwaji kesi kwa kufanya taratibu za awali za usikilizwaji wa kesi kabla ya kuanza kusikilizwa na hatimaye kuamuliwa ktk mahakama yenye mamlaka mahususi kufanya hivyo.

Hata hivyo changamoto si hiki kinachoitwa 'committal proceedings' bali ni suala la upelelezi kutokukamilika kwa haraka na ndani ya muda maalumu kisheria.

Juhudi zimegonga mwamba za kujaribu kuuondoa mchakato huu kwa kupitia kwa hoja ya kwamba unachelewesha haki na kuwa kinyume na misingi ya kisheria, mfano katika kesi ya Zepherine Galeba dhidi ya mwanasheria mkuu...
 
Huwa najiuliza sana hili swali hebu nitege hapa
Naangalia sana kesi kama hizi kwenye mahakama za nje lakini huwa naona zinasikilizwa moja kwa moja kwenye mahakama husika
 
Ni matakwa ya kisheria haswaa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, kwamba inapaswa kesi ipitie ktk mchakato uitwao 'committal proceedings' ambapo lengo lake ni kurahisisha mchakato wa usikilizwaji kesi kwa kufanya taratibu za awali za usikilizwaji wa kesi kabla ya kuanza kusikilizwa na hatimaye kuamuliwa ktk mahakama yenye mamlaka mahususi kufanya hivyo.

Hata hivyo changamoto si hiki kinachoitwa 'committal proceedings' bali ni suala la upelelezi kutokukamilika kwa haraka na ndani ya muda maalumu kisheria.

Juhudi zimegonga mwamba za kujaribu kuuondoa mchakato huu kwa kupitia kwa hoja ya kwamba unachelewesha haki na kuwa kinyume na misingi ya kisheria, mfano katika kesi ya Zepherine Galeba dhidi ya mwanasheria mkuu...
Msomi tunaomba soft copy ya hii case.
 
Back
Top Bottom