Kwanini watanzania wanapinga kupanda kwa bei?

Kwanini watanzania wanapinga kupanda kwa bei?

Godwine,

Hebu toa mkakati, mikakati ya vipi watanzania wataweza kuacha kupinga kupanda kwa bei.

Toa mbinu kwa wafanyakazi wa kima cha chini ambao ndio wengi kwa wale wenye ajira.
Toa ushauri kwa wamachinga, wafanye nini ili kupinga kupanda kwa bei kwao iwe historia.
Toa mbinu kwa wakulima huko vijijini nini wafanye kuinua kipato chao kuendana na ongezeko la kupanda kwa bei ya bidhaa na gharama za maisha.
Pengine una mawazo mazuri ambayo yatawasaidia wengi.

Pia toa mawazo yako ya nini serikali ifanye iweze kuleta unafuu wa maisha kwa mtanzania wa kawaida. hapa sizungumzii, maendeleo. Unafuu tu wa maisha ili mtu asiwe na sababu ya kulalamika gharama za maisha zikipanda.
hapa nazungumzia basic needs, chakula cha kila siku, ada ya shule ya mtoto/watoto, hela ya kununulia dawa mtu anapoumwa, nauli ya daladala au usafiri kutoka point A to B. Sizungumzii vitu vya anasa.

Godwine, tusaidie mkuu, tupate kuacha kupinga kupanda kwa bei kwa sababu tutakuwa tunamudu ongezeko la gharama hizo..
 
wameping wapi? mbona sijaona maandamano? kazi kuandika tu na kuongea huku mmekaa. haki haiji bila kuidai tena kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom