Kwanini watanzania wanapinga kupanda kwa bei? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini watanzania wanapinga kupanda kwa bei?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Godwine, Dec 25, 2010.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani hivi kwanini watanzania tunapinga kupanda kwa bei? au hatutaki maendeleo?
  kupanda kwa bei kunaonyesha tunaenda na wakati? jamani hivi kweli mtagoma kwa kasababu kadogo tuu ka kupanda bei na kupanda kwa gharama za maisha?
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Godwine,uko serious kweli,au.....
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona anataka ongeza idadi ya post au labda haelewi impact ya kupanda kwa umeme kuwa production cost itapanda na bidhaa zote kuwa juu at the same Salary
   
 4. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  alie tuma post hii ni mnafik,mzandiki,kizabizabina,msaliti,t bag wa prisom break,mwanga tena wa mchana kweupee. I hate you fisadi papa we!
   
 5. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Msimshangae huyu kavimbiwa tu na mamisosi ya Christmas!
   
 6. N

  Nataka Member

  #6
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya ndio maisha bora ya walala hoi ,wafanyakazi , wakulima na wala sio kwa wanasiasa wenye 12mil. Income
  Tusherehekee Migao ya Umeme na Bei za Juu kwa bidhaa zote. Hiyo ni Bora sana kwa Wazalendo pia pendekeza kuongezwa kwa Bei mara dufu maana ni bora tuongeze mishahara ya viongozi wetu ili bei zizidi kupanda maaana wahitaji hizo kwaajili ya muda wanaotumia na sio vinginevyo MUNGU Ibariki...........
   
 7. l

  liganga4 Member

  #7
  Dec 26, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  nadhani antukumbusha nafasi tuliyo kuw nayo tarehe 31 oct 2010. gharama za mabango, wasanii nk. tuliatakiwa kuchagua gharama nafuu au gharama za juu tukachagua gharama za juu. tumekubali kuchakachuliwa.
   
 8. G

  Godwine JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwanini unasema same salary kwani mshahara hautakiwi kupanda nadhani tunatakiwa kujipanga ili kukabiliana na mfumuko wa bei na si kubweteka
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Godwine,

  Ni kwa sababu wakati gharama za maisha zinapanda, kipato cha wengi hakipandi na hivyo kukosa uwezo wakulipia nyongeza za bei za bidhaa na vitu vyengine ambavyo vinapanda bei kila jua linapochomoza. Ukweli ni kuwa mlalahoi ameshachoka kufunga, kukaza "mkanda".
  Matokeo ya haya ya kupanda kwa bei na gharama za maisha hapa TZ inachangia kujenga jamii inayozungumzwa kwenye hiyo post chini.

  pitia post hii Je ni kweli watu weusi ni wajinga,wabinafsi na wachoyo??? huko kuna vitu vya kujifunza.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/101037-je-ni-kweli-watu-weusi-ni-wajinga-wabinafsi-na-wachoyo.html
   
 10. G

  Godwine JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  unadhani kwa mwananchi wa kawaida nini anachoweza kukabiliana nalo ni kupinga kupanda kwa bei au kujalibu kuongeza kipato chake?
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  ni kuiba tu, kuwa wabinafsi kwa kasi zaidi,kwa ari zaidi na kwa nguvu zaidi kama wanavyofanya viongozi wao.
  mkuu soma hiyo post niliyoweka link.
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Godwine,

  Ungetusaidia sana ungetuambia kwa nini wewe hupingi kupanda kwa bei?
  Bila shaka wewe hujabweteka kwa hiyo hela haikupi shida,unamudu maisha hata kama bei zita-sky rocket! sasa tusaidie maujanja na sisi ili tuongeze vipato vyetu.
  Kwa mfano wewe binafsi unafanya kazi au shughuli gani kuweza kumudu gharama za maisha?

  Tuko tayari kupokea ushauri wako. Hakuna anayependa dhiki ya maisha!
   
 13. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  mkuu kwanza we ni raia wa nchi gani? Unajua kuna kupanda kwa bei(inflation) ya wastani kama asilimia 5 hivi ikizidi hapo ni tatizo na ndio inasababisha thamani ya sarafu yetu kushuka kila mara.
   
 14. G

  Godwine JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mimi ni mtz mkuu lakini katika hoja yangu natamani kupanda kwa bei kwasababu ni namna mojawapo ya kuwafanya wafanyabiashara wavutiwe na kupenda kuwekeza katika biashara fulani kwani ni hatari kubwa kwa bei kutopanda au kushuka kwa wafanya biashara . pia kushuka kwa thamani ya fedha kunafanya ulipaji wa mikopo ya muda mrefu kuwa nafuu.......kwa mfano kama ulikopa shs 1 milioni mwaka 2005 kwasasa ni laisi kulipa na vilevile kupanda kwa bei ni changamoto ya nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi kwa ujumla
   
 15. G

  Godwine JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Unanifurahisha sana.
  mlalahoi hajui mkate ataupata wapi leo unazungumzia biashara gani?
  wamachinga si unawaona kama upo mitaani, wanajitahidi kuzunguka huku na huko kutafuta hela,
  wakulima ndio hivyo, wanajitahidi lakini mwisho wa siku wanakuta wako sufuri.
  sasa hawa unawowazungumzia ni akina nani?
  Makamba? watoto wa Kikwete? Lowassa? bakhresa?

  walalahoi huko benki wakaoneshe hati gani mpaka wapate mkopo?
  wewe mwenyewe unafanya nini mkuu? mbona unabania hayo maujanja? yamwage hapa ili tuchangamkie maisha, na sisi tuache kupinga ongezeko la bei.. au ndio unatutania??

  Godwine ,unazungumzia umma wa watu kama 35milioni hapa, ukiondoa wachache ndio wanaomudu kukaa kimya bei zinapopanda.
   
 17. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mmesahau kwamba bei hupanda kwa walala Hoi tu?
  Walala Hai walipiwa bills na walala hoi.........
   
 18. G

  Godwine JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  natambua hilo inabidi kufika wakati watanzania kujiunga kwenye vikundi na kuandika proposal za miradi na kuomba fedha kwenye taasisi za fedha na si kusimama mwenyewe
   
 19. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaka acha kucheza na maisha ya Watu. Vijihela vyako ndo vinakufanya unakuwa na dharau ya kuongea hayo???? Shame on you!!!!!\
  Unataka kusema kipato cha Mtanzania wa kawaida kinaendana na upandaji wa bei?????

  NAOMBA UACHE DHARAU ZAKO ZA KUTUKNA HATA WAZAZI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKO WENYE KIPATO AMBACHI HAKILINGANI NA GHARAMA ZA MAISHA...

  Take care of your words

   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
   
Loading...