Kwanini wasanii wanaijeria wanatukimbiza huko youtube

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,052
4,075
Leo nilikuwa napitia huko youtube nimegundua wasanii wetu watachukua muda mrefu kufikia level za wasanii wa naija. Kwanini tunaachwa mbali sana nyimbo za wasanii wetu ukizisikia zinavyolia kila mtaa unaweza usiamini utachokiona huko youtube viewers ni wachache sana

Wakati wenzetu ukisikia nyimbo inalia mtaani utakuta inatembea viewrs 50m wanakwama wapi wasanii wetu. Unaweza kukusanya video zote za msanii wa muda mrefu lakini utakuta hamfikii hata chipukizi wa naijeria aliyetoa nyimbo moja

Tunawasanii hawazidi saba ndio ambao tumekuwa tunawategemea ndo mana wanashindwa kushindana na msitu huu wanaijeria
 
Kama umeishi au unafuatilia mambo utagundua Nigeria Ni maarufu sana duniani kama Zanzibar ilivyomaarufu kuliko Tanzania. Kuna baadhi ya raia wa mabara mengine wanajua afrika ni nchi sio bara wengine anaoijua afrika ukiwaambia wakutajie nchi zilizopo Africa lazima lazima Nigeria kwanza Sasa hiyo tu inawabeba wasanii wake achilia mbali uwezo walionao
 
idadi yao kubwa, uchumi na mziki wao kupenya mapema duniani kunawafanya wawe mbali kisanaa zaidi yetu, tuna safari ndefu sana kuwafikia hawa wanaija
 
me nafikiri kwanza ni wingi wao na upendo kati yao na wananchi wanao support kazi zao, kingine ni exposure walionao yani wale jamaa wametapakaa nchi nyingi sana na kutapakaa kwao pia kunasababisha mziki wao kupendwa na watu kwasababu wanakuwa na club zao
 
Nigeria kwao wapo zaidi ya mil 200 ,TZ tupo zaidi mil 60,hamuwezi kuwa sawa.
Wingi wa watu sio sababu mziki wetu unasikilizwa na afrika mashariki yote ndio mana nimekutajia wasanii wakuwahesabu wanaoweza kuleta ushindani kidogo na naijeria artist huko youtube
 
Mbn me naona sisi ndio tumekomaa na YouTube lakini ukija kwenye platform kubwa kama itune , audiomack na zinginezo wametuacha mbali mnoo
Basi kwa hili wengi tulikuwa hatujui hadi youtube wanaija wanatukimbiza sisi tuna wasanii watatu kama sio wanne wanaoweza kufikisha viewers 50m kwa nyimbo moja
 
Basi kwa hili wengi tulikuwa hatujui hadi youtube wanaija wanatukimbiza sisi tuna wasanii watatu kama sio wanne wanaoweza kufikisha viewers 50m kwa nyimbo moja
hapo kibamia mtoe kabisa, hana wimbo wowote wenye views million 50
 
Back
Top Bottom