Kwanini wapiga kura wameamua kuifuta CHADEMA?

Kwanini wapiga kura wameamua kuifuta CHADEMA?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,940
Reaction score
7,849
CHADEMA kikiwa chini ya katibu mkuu Dkt. Slaa mtu muadilifu wa kweli mkakati wake kama chama cha upinzani ulikua kupinga rushwa na kutaka uwepo wa utawala bora. Wakati Dr Slaa akiwa Katibu Mkuu nchi ilikua imeoza kwa rushwa kuanzia chama tawala CCM chenyewe na serikali yake hadi maisha uraiani. Hakuna kitu mtu unafanikisha bila kuhonga. Watu wengi walijiandaa kupigia kura upinzani 2015 kuondoa utawala wa wala rushwa.

Wengi walitegemea kuona Dr Slaa akiteuliwa kama mgombea wa Chadema jambo ambalo lilifanyika ila mwenyekiti Mbowe akaweka uteuzi wa Dr Slaa kibindoni badala yake inaaminika akafanya biashara ya kuuza uteuzi kwa mgombea aliyebwagwa huko CCM na kumfanya mgombea wa Chadema.

Mgombea huyo kutoka CCM, Chadema ndio walikua wanamshambulia miaka mingi kama kinara wa rushwa nchini.

Baada ya ushindi wa Magufuli kiongozi thabiti mpinga rushwa na mjenzi wa nchi Chadema badala ya kuja na mkakati na mbinu za upinzani chanya kwa maendeleo ya nchi wakaanguka kwenye mtego wa kutumiwa na nchi za nje zilizotaka kuona Magufuli anashindwa kutokana na kubana maslahi ya makampuni yao ya kinyonyaji.

Chadema wakakubali kupinga kila mradi wa maendeleo kuanzia miundombinu elimu na afya eti ni vitu tu havina maana kwao cha maana ni uhuru haki na maendeleo.

Wakataka kufanya raia wajinga sana hawaoni uhusiano kati ya miradi ya serikali ya CCM na maendeleo yao. Zaidi ya hapo chadema wakawa waongo na wazushi kuhusu haki za binadamu na kusema nchi inahitaji kukombolewa toka utawala eti dhalimu wa CCM.

Kutokana utendaji mzuri na kampeni bora kabisa toka CCM na mgombea urais wake kama wengi walivyotarajia Chadema ni kama imefutika.

Walifanya makosa makubwa ya kimkakati kwa kugeuza lengo lao kuu ni kuingia madarakani tu wakati wangeweza kua tayari kuunga mkono uongozi mzuri unapokuepo. Wamefanya chama cha siasa ni kwa ajili ya maendeleo ya viongozi wa chama badala ya maendeleo ya wananchi.
 
Wakat wa Dr slaa kikwete aliwacha upinzan kufanya mikutano, ndio maana walikuwa na nguvu.

Huyu wa sasa hataki kupigwa na anasema mbele ya camera hataki upinzani.

Wewe unasema wapiga kura ndio wameua upinzani.

Shiit
 
Chadema chini ya Slaa kilikuwa na agenda zito nyepes kueleweka kwa kila mwananchi yenye ushahidi kwa kila mwananchi usiopingwa

Rushwa na ufisadi ni vitu vilikuwa wazi sababu ilikuwa kila sehemu kuanzia mijini Hadi vijijini

Chadema ilipoacha hiyo agenda inaongelea vitu visivyokuwepo vizuri kea watu ndio wakaamua kupiga chini mwingine ohh kazi na Bata!!!! Nini hicho mwananchi kijijini anaelewa kitu hapo?

Watu hawana hospital au barabara unasema wanatikiwa wapewe maendeleo ya watu sio vitu ka hospital na barabara !!!!!

Chadema hawakujiandaa kabisa Safari hii
 
Mtatafuta kila Narrative, lakini hamuwezi kufuta uwizi mliofanya, na mmumejuaa kuwa:
1. Wananch hawawapendi - mmepiga magoti na kulala chali kuomba kura
2. Mumeua watu ili kupata kura - watu hawawapendi
3. Mmepiga mabomu- kila mtu anajua na anwasuta
4. mmechapisha kura fake- aibu
5. kumbe yule bwana hata afya siyo nzuri
6. mmetumia polisi

Hata mtumie narattive gani haya hayafutiki
 
Kuna watanzania awaipendi CCM,lakini kwa ukibaraka wa wazi aliounyesha Lissu mgombea wa Chadema wakaamua kimpiga misumali kwenye sanduku la kura.
 
Wakat wa Dr slaa kikwete aliwacha upinzan kufanya mikutano, ndio maana walikuwa na nguvu.

Huyu wa sasa hataki kupigwa na anasema mbele ya camera hataki upinzani.

Wewe unasema wapiga kura ndio wameua upinzani.

Shiit
Tulia wewe sindano chungu au sio
 
Kura halali za Lisu Ni mil7 kama una akili utajua kichofaywa na Nec
 
Mtatafuta kila Narrative, lakini hamuwezi kufuta uwizi mliofanya, na mmumejuaa kuwa:
1. Wananch hawawapendi - mmepiga magoti na kulala chali kuomba kura
2. Mumeua watu ili kupata kura - watu hawawapendi
3. Mmepiga mabomu- kila mtu anajua na anwasuta
4. mmechapisha kura fake- aibu
5. kumbe yule bwana hata afya siyo nzuri
6. mmetumia polisi

Hata mtumie narattive gani haya hayafutiki
Wewe bakia tu na shingo ngumu sisi tunaenda na jpm
 
Back
Top Bottom