Kwanini wanawake wengi siyo walezi wazuri hasa kwa watoto ambao wamewakuta kwa waume zao

Genio the great

Senior Member
Aug 29, 2022
161
495
Hellow Wana jamii, Leo nimekaa nimetafakari Kuna jambo limenikosesha majibu ya moja Kwa moja nimeona nililete kwenu

Hivi ni kwanini wanawake ni ngumu sana kulea watoto ambao hawakumzaa wo?????

mfano umeoa mwanamke wakati huo tayari wewe una mtoto mwingine hata kama ulikuwa umempa taarifa kwamba Nina mtoto yaani malezi ambayo atakuwa ana mtreat mtoto ni mabaya sana

Yaani katika wanawake 10 ukimkuta anayeishi na mtoto wa mume ambaye sio wakwake Kwa amani ni 1 tena hata huyo mmoja anaweza akawa anaigiza hasa kipindi ambacho baba wa mtoto atakuwepo

Lakini ni jambo la kawaida sana Kwa mwanaume kuoa mwanamke mwenye mtoto tayar na akaishi na mtoto yule akimlea kma mtoto wake wa kumzaa Kwa kumpatia mahitaji muhimu na ni ngumu kumkuta anamnyanyasa.

Na huku uswahili ndio Kuna sentensi kabisa wanasindikizia inayosema

"UKIPENDA BOGA PENDA NA UA LAKE."

Hebu kama unafahamu chochote kuhusu huu utamaduni sema neno ikiwezekana jamii zetu zipone maana ni ugonjwa unaoua ndoto za baadhi ya watoto kisa tu wanaishi na wamama walezi.

Mama Yuko tayari mtoto wakwake akasome au aangalie hata Tv lakini yule wa mume wake aoshe vyombo n.k
sddefault.jpg
 
Unajua tayari kuna zile hisia zimeshajengwa kwenye vichwa vyetu kwamba mama wakambo lzm awe mnyanyasaji tu kwahiyo hata awe anafanya kumuelekeza mtoto njia sahihi maybe kumkanya au kumfundisha kikazi vya nyumbani watu tu wataona mtoto ananyanyaswa. Mtu akikukubali ww na wanao manake amechukua majukumu yakua mama sio umuwekee mawazo negative muda wote kwamba atamnyanyasa ww mpe na uwe unafuatilia je kuna unanyasaji maana unawezakuta hata huyo mtoto alifungwa moto na mama yake huko ili anayemlea aonekane mbaya.
 
Chanzo cha unyanyasaji ni uzembe wa mume husika.

Eti unaenda kazini mwanao anateswa unarudi hujui kama anateswa.mimi nitakuoa lakini chumbani lazima nikwambie ni kwa namna gani mwanangu/wanangu ni muhimu kukuzidi.

Yaani manyanyaso kwao itakuwa ni sehemu mojawapi ya usaliti kwangu.
 
Hii Sheria nimeipenda na imenichekesha sana. Yaan kumnyanyasa mwanao ni sawa na usaliti
 
Unajua kuhudumia mtoto na kulea mtoto ni vitu viwili tofauti, kuhudumia kunahitaji pesa tu hakuhitaji kuinteract na mtoto mara kwa mara ila kulea kunahitaji upendo na kuinteract na mtoto mara kwa mara, upendo ni feelings na huwa haulazimishwi ila pesa ni property ambayo unaweza kumpa tu mtu kwa sababu yoyote

Sasa ni rahisi kuiona chuki ya mwanamke kwa watoto wasio wake kwa sababu jukumu lao ni kulea ambako kunahitaji kuinteract na watoto mara kwa mara, ila mwanaume anaweza kuwa hawapendi watoto ambao siyo wake ila chuki yake haiwezi kuonekana, sababu jukumu lake ni kuhudumia tu ambalo halihitaji yeye kuinteract na watoto mara kwa mara

Lakini laiti kungekuwa na uwezekano wa kuswitch majukumu, mwanamke awe anahudumia watoto halafu mwanaume awe analea watoto basi si ajabu hata wanaume wangefanya haya haya ambayo wanafanya wanawake, after all wanaume wengi huhudumia watoto wasio wao kutegemeana na mapenzi wanayoyapata toka kwa mama zao na si kwamba eti wanapenda kufanya hilo
 
Unajua kuhudumia mtoto na kulea mtoto ni vitu viwili tofauti, kuhudumia kunahitaji pesa tu hakuhitaji kuinteract na mtoto mara kwa mara ila kulea kunahitaji upendo na kuinteract na mtoto mara kwa mara, upendo ni feelings na huwa haulazimishwi ila pesa ni property ambayo unaweza kumpa tu mtu kwa sababu yoyote

Sasa kwa wanawake ni rahisi kuiona chuki kwa watoto wasio wake kwa sababu jukumu lao ni kulea ambako kunahitaji kuinteract na watoto mara kwa mara, ila mwanaume anaweza kuwa hawapendi watoto ambao siyo wake ila chuki yake haiwezi kuonekana, sababu jukumu lake ni kuhudumia tu ambalo halihitaji yeye kuinteract na watoto mara kwa mara

Lakini laiti kungekuwa na uwezekano wa kuswitch majukumu, mwanamke awe anahudumia watoto halafu mwanaume awe analea watoto basi si ajabu hata wanaume wangefanya haya haya ambayo wanafanya wanawake, after all wanaume wengi huhudumia watoto wasio wao kutegemeana na mapenzi wanayoyapata toka kwa mama zao na si kwamba eti wanapenda kufanya hilo
Mmmmh mbona kma nmekupata nusu nusu kama swala ni Kwasabab wanainteract nao mbona watoto wao wa kuwazaa wanainteract nao pia kwann hawafanyi hvyo Kwa watoto wao Ili hiyo sabab iwe na nguvu. Au interaction hiyo inakuwa na impact upande mmoja tu??
 
Sasa ambacho hujaelewa hapo ni nini, umeshasema watoto wake wa kuwazaa hao naturally lazima awapende, ila ambao siyo wa kwake hawezi kujilazimisha kuwapenda maana upendo ni feeling haulazimishwi huja automatically tu
 
Wafugaji wanaelewa, kukuta akiwa na vifaranga vyake hudonoadonoa vile vya mama mwingine, unafikiri ni kwa nini?

Ni asili ya kimaumbile ya ulimwengu, ukiona mama anapatana na watoto wa jambo ujue ni mzuri wa kuficha hisia zake, au hakumpenda mume yuko hapo kwa interests tu tofauti.
 
Back
Top Bottom