nadhani ungetaka watu wajitangaze hivi
mimi ni Mr. X, age 54yrs,
Nimeoa nina watoto wa nne, nina kibamia/kimbilimbi natafuta mchumba Mzuri mwenye Bla bla bla
Mkuu ushabahatika kukutana na mwenye sifa hizo nini? umesahau haka kamsemo isemayo 'nyani haoni kundule'? kwa hiyo sio rahisi mtu ajione mwenyewe kuwa yupo hivyo alivyo.
Mkuu ushabahatika kukutana na mwenye sifa hizo nini? umesahau haka kamsemo isemayo 'nyani haoni kundule'? kwa hiyo sio rahisi mtu ajione mwenyewe kuwa yupo hivyo alivyo.
Umesema vyema mkuu. Ila ulichosahau ni kwamba hiyo ndio kawaida hata katika maisha halisi huko mtaani kwetu. Sio humu JF au kwenye social media nyingine yoyote tu.
Hatahivyo, mbona hata sisi wanaume ni hivyo hivyo mkuu? We are not an exception to this practice. Sijawahi kuona mwanaume humu JF au huko uraiani anayetafuta mwenza/mpenzi huku aki-display yale madudu yake. Hiyo inabakia kuwa siri yake na wale watu wake wa karibu.
Ndio maana kuna ile concept ya kumchunguza mpenzi/mke/mume mtarajiwa. Kuna baadhi ya mambo/tabia normally mtu hataki watu wengine wazijue. Labda wajiongeze wenyewe na kuzigundua. Na hata baada ya kuzistukia, mlengwa anaweza azikane au akuambie nishabadilika tayari au sasa niko kwenye mchakato wa kubadilika. Inawezekana hapa ndio ile busara ya kusema ukimchunguza sana bata hutamla inapokuja (japo mimi sikubaliani nayo 100%).