Hekima huwa mshindi kuliko hasira wakati wote inanishangaza sana kama wewe mwanaume unaweza taka kufanya kitendo kama hicho,hivyo wanafanya wanawake wanaume huwa tunajenga fikra huru na hai zenye uwezo wakusimamia maamuzi mahali popote na kwa yoyote,leo huyo binti kakuambia hivyo kwa sababu ni huyo mzee,je akikutana na kijana wa rika lake asiye na mbele wala nyuma na akadungwa mimba na ikakataliwa na pengine apate magonjwa na pengine aje awaambukize nyie hapo nyumbani.
Shughulikia mzizi wa tatizo na siyo matokeo ya tatizo,mpe huyo bint yako elimu ya kujitambua ajue Kusema NO na awe na uwezo wakuisimamia,popote nakwa yoyote,kwa hiyo unataka kusema mkeo akipigwa sound huko akija kukuambia utajifungasha kwenda kwa huyo jamaa na siyo kumuweka sawa mkeo na labda nikuambie jambo moja kiwa siyo rahisi kwa ndoa ya huyo mzee kuvunjika kama ukifanya unachotaka.
Kwa sababu ya umri wao na pia hawajafanya sex na katika jamii hii ya kitanzania,mwanaume kutongoza siyo ajabu hata kidgo...kwa hiyo niseme tu kuwa fanya maamuzi kama mwanaume achana na maamuzi hayo ya wanawake,jenga fikra huru kwa huyo binti,je usipokuwepo siku nyingine na akakutana na mwingine?